29/05/2026
Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mwanaume ashindwe kurudia tendo la ndoa mara baada ya kumaliza mara ya kwanza, zikiwemo:
Uchovu wa mwili – kazi nyingi, kukosa usingizi au nguvu kidogo.
Umri – kadri umri unavyoongezeka, muda wa kuweza kurudia huongezeka.
Msongo wa mawazo na stress – huathiri hamu na uwezo wa kufanya tendo.
Magonjwa k**a kisukari, shinikizo la damu au matatizo ya homoni.
Matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.
Matumizi ya baadhi ya dawa za matibabu ambazo huathiri nguvu za kiume.
Kiwango cha chini cha homoni ya testosterone.
Kutopata msisimko wa kutosha baada ya kumaliza mara ya kwanza.
Ni kawaida kwa mwanaume kuhitaji muda wa kupumzika kabla ya kuweza kurudia tendo. Muda huo hutofautiana kati ya mtu na mtu.