23/01/2026
FIKRA ZA LUGHA YA KISWAHILI
Mwana wa Afrika, panda mbegu zako zenye hekima ya hatima ya lugha ya Kiswahili. Ili kufuata njia na kutimiza maono ya waasisi wa bara letu. Ninazungumza hivi kwa sababu Nimekuwa nikifuatilia mienendo ya tabia na mtazamo wa baadhi naona kubeba upotofu kuhusu lugha ya Kiswahili kwa sababu ya kusumba za kikoloni ambazo zinaishi katika fikra zao. Hali hii ichukulie kwa uzito, kabla ya kizazi kijacho hakijakufikia.
Maana kutafuta mti ulioteuliwa na fikra potofu za kuamini lugha za kigeni ni kulaani afrika wako. Amka! ichunguze na kuifuata njia inayotazamwa na dhamiri ya mama Afrika. Maana hekima nisemayo hutembea mahali penye sauti tulivu iliyobeba hatima tukufu ya mama Afrika. Sio pale penye kelele za hila.
Kumbuka Maisha yanakuwa na maana unapogundua kwamba kila kitu kuwa kizuri unapokiangalia kwa upendo. Unapoanza kuyaona maisha si kwa kile tu yanakupa, bali pia kwa yale yanayotokea katikati, na hata wakati kila kitu kinapobadilika, ndipo unaanza kuelewa uzuri wake.
Kwa hiyo ni wakati ambapo Afrika hatuitaji kupotea katika hofu, shaka au kuwafurahisha wabaya na kuzurura gizani wakati babu zetu na waasisi wa bara letu la Afrika waliandika maono vibaoni ili kila mmoja asome, Pia walishaonyesha njia itakayotufanya kuwa wamoja, njia ambayo ni lugha ya Kiswahili ♥️. Vilevile waliamini kuwa lugha hii ndio itakayowafanya waafrika kupika chakula kizuri na chenye lishe kwa mama Afrika. Sasa ili Afrika ijitukuze na kutumia vipawa na uwezo wake haina budi kutumia lugha ya Kiswahili katika kufanya tafiti na kubuni teknolojia za asili kuanzia vikaushio vya sola, vichujio vya maji, droni za kilimo, hadi zana za afya za kidijitali.
Aidha kupitia umoja wa waafrika, Afrika itazungumza na kufikiri namna ya kubadili hesabu kuwa mashine, dhana kuwa vielelezo na data kuwa maamuzi ili kuondoa utegemezi kutoka nje.
Pia watahitaji kuenda mbali nakufanya TEHAMA kuzungumza lugha ya Kiswahili na kuweza kuunda programu zinazosaidia biashara za ndani, shule, vyuo au hospitali.
Hizi Akili zetu bora zitazungumza na kufikiri kwa kutumia lugha ya Kiswahili zitajikita katika kujenga viwanda, mfano kutengeneza mashine za ndani za kuchakata kakao, siagi ya shea, muhogo,kahawa, na mazao mbalimbali kuwa bidhaa zenye kustawisha Afrika na ulimwengu.
Hapa nazungumzia lugha ya asili ya mwaafrika yenye kubeba asili na urithi wetu ambao ni lugha ya Kiswahili itakayoibua waafrika kuwa wabunifu wa kuboresha maisha ya waafrika.
Mwana wa Afrika kumbuka bara halijengwi na wale wanaochapisha zaidi, bali na wale wanaounda zaidi,wanobuni vitu na kugundua. K**a tuonavyo mataifa mengine k**a china,korea, ujerumani, n.k.
Hebu turudi Kwenye lugha zetu za asili, tuache ubinafsi na kasumba za kikoloni ambazo hazitatusaidia k**a waafrika, tujikite katika uwekezaji wa kubuni na tafiti zenye tija hakika Afrika itajitukuza.
“Mungu ibariki Afrika, Kiswahili lugha yetu”.❣️