Fatma halifa

Fatma halifa

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Fatma halifa, College & University, Fatmahalifa12@gmail. com, Dar es Salaam.

04/08/2016

ukíjífαnчα mjuαjí ѕαnα

Photos 09/06/2016

Ishi vile upendavyo, usiangalie watu watasema nini, kwani watu hawakosi maneno, kila jambo watasema. Usiogope kusemwa, songa mbele

Photos 23/05/2016

K**a mwanaume hakupigii simu au hata ujumbe mfupi wa maneno kukujulia hali ila wewe ndio wa kufanya hivyo kila siku ni kwa sababu hataki kukupigia simu wala kukutumia sms.

K**a hataki kukupa 'attention' na kudai yuko busy kila siku ni kwamba hataki kuonanana na wewe.

K**a ataku 'treat' k**a takataka ni kwa sababu hakujali.

Mwanaume ambae umekuwa nae katika mahusiano kwa muda mrefu kidogo anapokuambia kuwa "subiri kwa sasa sipo tayari" kwa kifupi ni kwamba hakupendi.

Usiendelee kucheza mchezo wake uletao hasira, 'don't keep playing his confusing game', usimtafutie sababu za kuendelea kumuamini!

Ngoja nikuibie siri mwanaume anapotaka kuwa na mwanamke hudumu naye pasina uongo, sababu au 'complications' zozote!

Acha kuendelea kusubiri ahadi zake za sungura na fisi, anachukulia faida uwepo wako, afanye yake na mwisho wa siku anaolewa mwingine. Weka utu wako mbele, na thamini ndoto zako!

Hauhitaji mtu ambae hajui ni nini anakitaka, hauhitaji mtu ambae hajui thamani uliyonayo k**a mwanamke.

Unahitaji mwanaume ambae anatambua thamani yako na anakupigania kila siku. Acha kuendelea kuumiza moyo wako kwa mtu ambae hayupo k**a ulivyomtegemea.

Mwanaume ambae anamlaumu kila mtu katika mambo yake isipokuwa kujilaumu yeye mwenyewe hafai k**a ukoma!

Photos 23/05/2016

SIFA KUMI ZA MPENZI WA KWELI

1.Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.

2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .

3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri

4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.

5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha maisha yako, atakulinda daima.

6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)

7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako k**a rafiki au mpenzi mbele ya wengine, hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.

8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.

9. Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata k**a atalazimika kufanya maamuzi magumu .

10. Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.

TUNAKUMBUSHANA KM UNAE MPZ HUYU USIMWACHE KWANI KUMPATA TENA UNAWEZA KUZEEKA USIMPATE.........

Photos 22/05/2016

Nimeona ni vema ku share na nyinyi story hii inayo gusa moyo, hasa kwa wewe uliye Mkristo.

Mchungaji mmoja alijibadili na kuwa omba omba katika viunga vya kanisa alilokuwa akitarajia kutangazwa jumapili hiyo k**a ni mchungaji mpya wa kanisa lile akitokea mji mwingine.

Alitembea kuzunguka lile kanisa akiwa amevaa nguo kukuuu zilizochanika chanika huku akipishana na watu waliokuwa wakiingia kanisani. Ni watu watatu tu ndio waliomsalimia.

Wengine wote hawakutaka hata kumuangalia mara mbili, walipitiliza moja kwa moja na kuingia kanisani.

Aliwaomba watu msaada wa chakula au hela ya kula hakuna hata mmoja aliyempa chochote.

Akaenda katika malango ya kanisa na kukaa katika ngazi akaweka chombo chake ili aguswae atoe msaada lakini hakuna hata mmoja alietoa hata senti moja.

Akainuka na kwenda mbele kabisa ya kanisa, akakaa benchi la kwanza kabisa, mzee wa kanisa akamwambia aondoke pale na akakae nyuma kwa vile ile sehemu ni ya watu maarafu (VIP).

Akaenda nyuma ya kanisa na akakaa benchi la mwisho kabisa lilikowa halina watu, maana wote walionekana kulikwepa. Akiwa amekaa akawa anasikiliza matangazo ya wiki kutoka kwa mzee wa kanisa.

Akasikiliza wageni wapya wakitajwa na kukaribishwa katika kanisa ila hakuna hata mmoja aliyemkaribisha kwa kuwa nae alikuwa mgeni mazingira yale.

Akaendelea kuwatizama watu waliokuwa wakimuangalia na kutoa mshangao ambao ulikuwa na tafsiri kwamba hatakiwi mahala pale.

Baadae kiongozi wa kanisa akaenda pale mbele kutangaza jambo la muhimu. Akasema kwamba anayo furaha kumtambulisha mchungaji mpya mbele ya waumini wote.

Waumini wakasimama na kutizama huku na huku wakiwa wanapiga makofi. Yule ombaomba akasimaa kutokea kule nyuma na kuanza kutembea kuelekea mbele ya aisle.

Kufikia hapo watu wakaacha kupiga makofi na kanisa likawa kimya wote wakimtizama yeye...akatembea mpaka madhabahuni na kuchukua kipaza sauti. Akasimama pale kwa dakika kadhaa, akakohoa kidogo na kunukuu mistari kutoka kitabu kitakatifu cha Mathayo 25:34-40 akaanza

"Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika, nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitizama, nalikuwa kifungoni mkanijia...Ndipo wenye haki watakapomjibu wakisema, Bwana ni lini tulikuona una njaa, tukakulisha au una kiu, tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha? Au u uchi tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa au kifungoni tukakujia?

Na mfalme atajibu, akiwaambia, AMIN AMIN NAWAAMBIA. KADIRI MLIVYOMTENDEA MMOJAWAPO WA HAO NDUGU ZANGU WALIO WADOGO, MLINITENDEA MIMI"

Baada ya kunukuu hayo, kwa masikitiko na uchungu mwingi moyoni mwake akajitambulisha mbele yao kwamba yeye ndiye mchungaji mpya wa kanisa lile na kuwaeleza ni nini amejifunza kutoka kwao asubuhi ile.

Wengi wakaanza kulia huku wameinamisha vichwa vyao chini.

Akawaambia "Leo naona ni mkusanyiko wa watu, ila sioni kanisa la Mungu. Dunia inayo watu wengi wa namna yenu, tunaleta mazoea hata kwenye ibada sasa, kimsingi Mungu tunaemuabudu hayupo mioyoni mwetu. Wakristo mnatakiwa muwe wanafunzi wa Yesu kristo wa kufuata mafundisho na kutenda mema k**a yeye alivyofanya. Lini mtaamua kuwa wanafunzi wa Yesu!?

Baada ya kusema hayo akaahirisha ibada mpaka jumapili inayofuata baada ya kutimiza neno la Mungu kupitia vitendo.

___________________________________________

Basi wewe uliye mkristo, zitafakari njia zako, kwenda kanisani kila Jumapili haitoshi, tuishi katika misingi ya kweli ya ukristo huku tukiwa na moyo wa kuwasaidia wale wote wasiojiweza.

Mwenyezi Mungu atubariki, tuishi vema sawasawa na vile yeye apendavyo.

Kwanini tusiseme 'Amen'.

Credits: Ben Carson

Photos from Fatma halifa's post 22/05/2016

Tuwasiliane marafiki zangu, niwapendezeshe k**a mnavyoona, kazi yangu ni nzuri, +255655688516

Photos 21/05/2016

Nasuka mitindo yote, karibuni sana

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address

Fatmahalifa12@gmail. Com
Dar Es Salaam