14/12/2023
R.I.P Rashid Nyembo (Nyembowood)
CENTRE FOR QUALITY EDUCATION
Kigogo Village Academy is a private institution owned by young Tanzanian
aiming to provide a quality education at affordable price to all Tanzanian.
14/12/2023
R.I.P Rashid Nyembo (Nyembowood)
Breaking News: Matokeo ya darasa la saba yatangazwa
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Chares Msonde
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba leo Oktoba 20,2017.
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.
Dk Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .
http://www.necta.go.tz/matokeo/2017/psle/psle.htm
Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76.
Dk Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.
Katibu Mtendaji huyo amesema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka 2016.
"Kwa masomo ya Sayansi na maarifa ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 kulinganisha na mwaka 2016.
"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30," amesema Dk Msonde.
Katibu Mtendaji, Dk Msonde amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni St Peter iliyopo Kagera, St Severine (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).
Amezitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).
Aliitaja mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, na Katavi.
WAZAZI tunajua Darasa la SABA wataanza MTIHANI WA TAIFA tarehe 06-09-2017, Mungu awabariki wafanye vizuri. Mambo muhimu ya kuzingatia:
1. Muda umekaribia hivyo mtoto afanye Revision kwenye yale mambo ya muhimu tu kwa kila somo.
2. Mzazi Jali sana afya ya mtoto wakati huu wa maandalizi. Asichelewe kulala, Ale chakula na kunywa maji safi na salama na atumie neti ya mbu wakati wa kulala. Omba Mungu kila siku naye ataendelea kukupa afya njema.
3. Siku ya mtihani ikifika: Andaa vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya mtihani, kisha afike mapema kwenye chumba cha mtihani angalau nusu saa kabla ya mtihani. Mfundishe aombe Mungu angalau hata kwa dakika moja kisha awe na imani Mungu atamsaidia. Baada ya hayo atulize akili yake kisha asubiri mtihani.
Akishapewa karatasi za mtihani:
1. Asome maelekezo yote kwa uangalifu kwenye kila ukurasa.
2. Ajibu maswali anayoyaelewa vizuri kwanza. Maswali magumu atayajibu mwisho.
3. Apange muda wa kila swali kuendana na idadi ya maswali anayotakiwa kujibu akizingatia masaa ya mtihani.
4. Kitabu chake cha kujibia mtihani ni kitu muhimu sana, asikichafue au kikilowanisha.
5. Baada ya kumaliza mtihani, ahakikishe amejibu maswali yote anayotakiwa kujibu.
6. Apitie maelekezo yote aliyopewa kwa mara nyingine na ahakikishe amezingatia yote.
7. Mwisho amshukuru Mungu kwa maombi. Kwa sababu alisoma vizuri atafaulu tu.
Nawapenda wote na naamini hayo niliyowaandikia yatawasaidia kwa namna moja au nyingine kwenye mtihani wao.(C&P)
Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.
Matokeo ya kidato cha sita nchini yametolewa leo Jumamosi, Julai 15 mwaka 2017, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385. Taarifa iliyotolewa inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647. “Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11 umepanda kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza; “Pia, ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana."Ufaulu wa masomo.Kadhalika taarifa hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa watanikiwa wa shule kwa upande wa masomo, ya Sayansi, Biashara, Lugha na Sanaa, haukuonyesha tofauti kubwa ukilinganisha na mwaka jana.Hata hivyo, ufaulu katika somo la General Studies umeshuka kwa asilimia 7.54 kutoka asilimia 71. 24 hadi 63.70.
Kupata matokeo, [url=http://41.188.136.77/matokeo/]
15/07/2017
Shule 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya kidato cha sita 2017
15/07/2017
MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2017 YATANGAZWA
FORM V SELECTION 2017
WANAFUNZI WALIOPANGIWA SHULE KIDATO CHA TANO MWAKA 2017
http://www.tamisemi.go.tz/form_five_selection_or/?page=1
09/06/2017
RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI (FTNA) MWAKA 2017
09/06/2017
RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE ) MWAKA 2017
09/06/2017
RATIBA YA MTIHANI WA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI MWAKA 2017
HUWEZI KUPANDA MBEGU MBOVU UKAVUNA MAZAO BORA , TUMECHAGUA KUZIMALIZA SHULE ZA SERIKALI.
A: Shule za serikali zinaendeshwa kisiasa kuwafurahisha wapiga kura .
1. Elimu bure kila mwezi billion 18 halafu hakuna pesa ya kuandaa mitihani, hakuna pesa ya vifaa vya kujifunzia, hakuna maabara,
2. Wanasiasa ndiyo wasemaji wa mwisho , maDC, RC, maDAS, madiwani, wabunge wanafanya ziara za kushughulikia walimu badala ya kushughulikia matatizo ya walimu
3. Darasa la saba wanafaulu wote mpaka wasiojua kusoma na kuandika, kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ni bure bure hakuna mitihani ya kupanda
4. Wanasiasa wamepandikiza ujinga kwa wazazi walaumu walimu badala ya kushirikiana nao kusaidia watoto/wanafunzi
5. Syllabus zinabadilishwa na wanasiasa walimu wa shule za serikali wanapewa wazifanyie kazi bila mafunzo yeyote
6. Watoto wa shule za serikali wazazi hawana habari nao kazi kubeti, kucheza vituko, kukariri bongoflava na kuwinda walimu, ni maarufu kumfukuza mtoto asiye na nidhamu muache mpaka ahitimu.
B: Shule za private zinaendeshwa kitaalamu
1. Elimu bora yenye gharama, vitabu vingi , walimu wanalipwa vizuri, maabara nzuri , chakula safi , mabweni safi , mitihani mingi , yaani matumizi ya pesa yenye tija.
2. Wanasiasa marufuku kupeleka porojo zao kwanza watoto wao wapo huko lazima heshima itawale, siyo rahisi mwalimu wa private kuingiliwa na Dc, RC, DAS, diwani, mbunge kwenye mambo ya professional
3. Ni marufuku kupokea kilaza hata k**a darasa la saba mtoto amefaulu lazima apimwe upya na kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne kuna mitihani ya mchujo, private siyo sehemu ya kilaza kabisa vilaza peleka shule za kata
4. Wanasiasa hawana nafasi ya kuchonganisha wazazi na walimu wa private yaani shule za private walimu na wazazi ni kitu kimoja wanafunzi/watoto wanatazamwa pamoja tena ushirikiano wao umetukuka... Hapa wazazi wengi ni wanasiasa kwa hiyo ni wakarimu kwa walimu wa private si wajua tena private ndiyo watoto wao walipo.
5. Syllabus zikibadilishwa ma