16/07/2015
❄ SIKU YA EID INAPOSADIFU IJUMAA ❄
Zimekuja Hadith kadhaa sahihi toka kwa bwana Mtume صلي الله عليه وسلم na Athar toka kwa Swahaba wa Mtume, kuhusu Siku ya Eid kiangukia Ijumaa. Na baadhi ya Hukumu muhimu k**a ifuatavyo:
1. Imepokewa na Imaam Ahmad, Abuu Dawud, An-Nasaai, Ibnu Maajah, Ad-Daarimy na Al-Haakim: kutoka kwa Zayd bin Arqam رضي الله عنه kwamba MU'AWIYAH BIN ABIY SUFIYAAN رضي الله عنه alimuuliza:
"Je, uliwahi kushuhudia -pamoja na Mtume صلي الله عليه وسلم- Eid mbili zilokutana ndani ya siku moja? Akajibu: Ndio. Akasema (Mu'awiyah) Mtume alifanyaje? Akajibu: Album swali Eid kisha akatoa Rukhsa ya kutosali Ijumaa, akasema hivi: Atakaye kuswali Ijumaa na Aswali.
2. Imepokewa na Al-Haakim, Abuu Dawud, Ibnu Maajah, Ibnu Al-Jaaruudy na Al-Bayhaqy kutoka kwa Abiy Hurayrah رضي الله عنه amesema ya kwamba: Mtume صلي الله عليه وسلم alisema:
"Hakika siku yenu ya leo zimekutana Eid mbili (Eid na Ijumaa) basi anayetaka Swalat ya Eid itakuwa imemtosheleza na Ijumaa (hatolazimika kuswali Ijumaa) ama sisi Tutaswali Ijumaa"
3. Imepokewa na Ibnu Maajah na Twabarany kutoka kwa Ibn Omar رضي الله عنهما amesema:
"Zilikutana Eid mbili zama za Mtume صلي الله عليه وسلم akawasalisha Watu (Eid) kisha akasema: Anayetaka Kuja kuswali Ijumaa na aje, na Anayetaka kurejea NYUMBANI na arejee"
4. Imepikewa na Ibnu Maajah kutoka kwa Ibn Abbas رضي الله عنهما amesema kwamba: Mtume صلي الله عليه وسلم alisema:
"Zimekutana Eid mbili ktk siku yenu ya Leo, basi atakaye (Eid) iatakuwa imemtosheleza kutokana na Ijumaa, ama sisi tutaswali Ijumaa in shaa Allah"
5. Imepokewa na Abuu Dawud na Ibnu Khuzaymah kutaka kwa A'twaa bin Abiy Rabaah amesema: Tulisalishwa na (Abdullah) Ibn Zubeir, Swalat ya Eid asubuhi ktk siku ya Ijumaa. Kisha (baadaye) tukaja (Msikitini) ili Kuswali Ijumaa, hakujitokeza kuja kuswalisha. Basi tukaswali pekee yetu. Wakati huo Ibn Abbas alikuwa TWAAIF, tulipokuja Twaaif tukamsimulia kisa hiki. Akasema "Alipatia Sunnah"
✴ BAADHI YA HUKMU MUHIMU ✴
① Atakayehudhuria Swalat ya Eid basi anaruhusiwa kutoswali Ijumaa na badala yake ataswali Adhuhuri. Ila k**a ataamuwa kuswali na Ijumaa itakuwa bora zaidi
② Yule ambaye hakuhudhuria Swalat ya Eid basi hana Rukhsa ya kuacha Ijumaa siku hiyo. Ila k**a hatopata pahala inaposwaliwa Ijumaa siku hiyo basi ataswali Adhuhuri
③ Inampasa Imaam wa Msikiti Kuisimamisha Swalat ya Ijumaa siku hiyo, ili wataotaka kuhudhuria wahudhurie na pia wale ambao hawakuswali Eid yapate Ijumaa
④ Ikiwa Hakutoswaliwa Ijumaa basi si Rukhsa kuadhini siku hiyo kwa ajili ya Adhuhuri, labda k**a itakuwa ni adhana ya Ijumaa
⑤ Si Kweli kwamba anayeswali Eid siku hiyo basi Haswali Ijumaa na Adhuhuri. Bali ukweli ni kwamba Adhuhuri inamuwajibikia
Allah ataqabali Funga na Dua zetu. Allahumma ameen
http://www.elmiyah.com/index.php/component/k2/item/177-iddi-na-ijumaa
<div class="_5pbx userContent" data-ft="{"tn":"K"}"> <div id="id_55a76cd2b630a3c...