11/07/2026
Ukikosa usijilaumu sana na kuona kuwa wewe ndio una matatizo sana kwasababu...
Wapo waliokosa na wanazo changamoto kubwa zaidi yako lakini bado wanaendelea kupambana kimya kimya๐ฅ
Usichoke na kuona kuwa umechelewa sana, endelea kutengeneza kesho yako kwa kuongeza Juhudi.
Pia ukifanikiwa kupata na kutimiza malengo yako,usidharau wala kuwabeza waliokosa.
Kwasababu wapo watu waliopata na kufanikiwa zaidi yako ila wapo tu kimya wametulia.๐คท
Maisha yanatufundisha hadithi nyingi sana za kupata na kukosa mithili ya kitabu kilichosheheni hadithi tamu na chungu.
Wakati wewe uko ukurasa wa 50 wa mafanikio yako kuna mwingine yuko ukurasa wa 150.
Mungu akupe hekima na uvumilivu wa kuendelea kusonga mbele bila kuchoka, kwasababu dunia ina watu wengi sana wanaokatisha tamaa ๐ kuliko wanaokutia moyo๐
K**a umeipenda makala hii.
React kisha mtumie na mtu mwingine ili tuendelee kujifunza zaidiโจ๐
-IF YOU REST YOU RUST-
๐ช
_(Abu Salmaan)_