01/10/2019
Unakutana na watu unaanza kuongelea kile unachokipendelea na kukitaka wewe? Hapana bhana... hakuna anayetaka kujua wewe unataka nini. Sisi pia k**a wewe tunapendelea kuongelea na kufanya vile tunavyovitaka.
Unataka kumfanya mtu afanye unachokitaka?
K**a unataka mtu afanye unachokitaka wewe afanye.... basi usifikirie nini unachokitaka wewe bali fikiria anachokitaka yeye ndo ukitumie kumfanya afanye unachokitaka wewe. Njia pekee katika hii dunia ya kuwashawishi watu ni kuzungumzia kile wanachokitaka na kuwaonyesha namna gani wanaweza kukipata. Kumbuka hili leo ukitaka kumfanya mtu afanye kile unachotaka afanye.
Unataka kufanya biashara pamoja na mtu fulani? Au unataka mteja fulani anunue bidhaa zako? Basi jiulize utafanya nini kitakachomfanya yeye atake kufanya kile unachotaka wewe afanye?. Unataka mtu akupe kazi? Basi acha kusema nini unataka kutoka kwake… mwambie nini utamfanyia akikupa kazi, utaongeza nini kwa uwepo wako pale nk mfanye atake kukupa kazi. Unataka watu, kampuni, jamii, wafanyabiashara wengine watumie bidhaa zako? Waambie nini utawafanyia wakitumia bidhaa zako (faida gani watapata wakitumia bidhaa zako?) wala sio tu nini unataka kutoka kwao.
K**a kuna siri yoyote ya mafanikio basi ni kuweza kutambua nini ambacho mwingine anakifikiria kwa upande wake na kutambua nini unahitaji kwa upande wako wewe mwenyewe.
Somo kutoka kwa Bwana Dale Carnegie katika kitabu chake cha “How to win friends and influence people”