02/10/2022
IFAHAMU TOYOTA VITZ
Na Samweli Azori
Miongoni mwa magari yaliyopata kufahamika kwa uharaka na urahisi zaidi hapa Tanzania kabla ya TOYOTA IST, Basi ni Toyota Vitz
Toyota Vitz ni gari maarufu sana hapa kwetu Tanzania, na hii ni kutokana na utumiaji wake mzuri wa mafuta pamoja na Uwezo wa wengi kuimudu, kuwa tegemezi na kutumika maeneo mbalimbali.
Toyota VITZ , inashindana na Nissan March, Mazda Demio, Honda Fit, na Suzuki Swift.
IMETENGENEZWA LINI ?
Toyota VITZ imeanza kutengenezwa mnamo mwaka 1999, Toyota Vitz inauzwa Japan pekee kwa jina hilo tu, lakini katika masoki ya magari nchi zingine, inafahamika k**a Toyota Yaris.
MATOLEO
Toyota Vitz inakuja na matoleo matatu, Ambapo , toleo lake la kwanza lilifahamika k**a XP10 lilitengenezwa kuanzia 1999 mpaka 2005, toleo la pili yaani XP90 lilitengenezwa kuanzia mwaka 2005 – 2010 na toleo la tatu amnalo ndilo lipo hadi sasa in linalojulikana k**a XP130 ambalo limekua likizalishwa kuanzia mwaka 2011 hadi sasa.
BEI ZAKE :
Bei zake huanzia TZS 9MIL na kuendelea , kutegemea na mwaka husika.
ENGINE ZAKE
TOYOTA VITZ Ina aina tatu za Engine anbayo ni 1.0-liter (990cc) 1KR engine, 1.3-liter (1290cc) 1NR engine, na 1.5-liter (1490cc) 1NZ engine.
Zinapatikana kwenye mfumo wa uendeshaji wa 2WD na 4WD, Toyota Vitz engines zina mfumo wa gearbox wenye either gearbox ya automatic yenye gear 4 , yenye CVT, au gearbox yenye ya gia 5- manual ( manyu )
UTUMIAJI WAKE WA MAFUTA
Toyota Vitz inayokuja na engine yenye ukubwa wa 1.0-liter engine inatembea wastani wa 20.8 Km kwa Litre moja ya Petroli wakati Toyota Vitz SMART STOP yenye 1.3L engine inatembea wastani wa 23.5 Km kwa Litre moja ya petrol na Toyota Vitz yenye 1.3L engine inatembea wastani wa 20.6 Km kwa Litre , Na Toyota Vitz Yenye 1.5L engine inatembea wastani wa 18.8 Km kwa Litre ya Petrol.
UPATIKANAJI WA VIPURI VYAKE PAMOJA NA BEI
Spare parts kwaajili ya Toyota Vitz Zinapatikana kwa wingi sana hapa Tanzania. Kwasababu asilimia kubwa huwa zinaingiliana na Toyota zingine k**a vile Toyota Platz na Ractis,
Ahsante kwa kusoma
Samweli Azori
+255 762 542 464
Dar es salaam,
Tanzania.