07/04/2023
Katika miaka million 250 hadi miaka million 66 iliyopita dunia ilipita katika kipindi kinajulikana k**a Mesozoic Era, katika kipindi hiki dunia ilikua haitawaliwi na binadamu tena bali ni kipindi kilichotawaliwa na viumbe wakubwa wajulikanao k**a Dinosaurs.
Hichi kipindi kilikua kipindi cha ajabu sana katika historia ya dunia maana kulikua na wanyama wakubwa sana, mfano: hata Mijusi unayoiona hii leo enzi izo ilikua ina umbo kubwa labda k**a umbo la kulingana na mamba, Vyura walikua wakubwa kupindukia, pamoja na wanyama wengine wengi na hii wanasayansi wanasema ilisababishwa na dunia kipindi hicho kuwa na mimea mingi na Oxygen kubwa sana na k**a inavyojulikana kisayansi, mwili ukipata Oxygen nyingi hukua kwa wingi.
Wanasayansi wanasema kwamba katika kipindi hiki licha ya kuwa na wanyama wakubwa na kutisha bado viumbe wa jamii yetu sisi binadamu waitwao mamalia bado waliweza kuishi lakini kutokana na viumbe wakubwa na hatari waliotawala dunia kwa kipindi hicho ilipelekea hawa mamalia waweze kujificha kwenye mashimo kwa kipindi kirefu cha maisha yao, na hali hii ya kujificha kwenye mashimo iliwasaidia sana siku ya kiama ilipofika....
Moja kati ya nadharia inayoaminika zaidi ya kiama cha Dinosaurs ni ile inayoitwa (K-Pg) inayosema kwamba kuna kimondo kikubwa sana kutoka angani kilidondoka na kuangamiza zaidi ya asilimia 75 ya viumbe vyote duniani pamoja na miti kwa kipindi hicho na hii ni baada ya ule mtikisiko uliosababishwa na kimondo icho kusababisha mito mkubwa, volcano, Tsunami, Matetemeko na kadhalika. Baada ya Dinosaurs wote kuangamizwa pamoja na viumbe wale wakubwa na hatari kuangamizwa hiyo sasa ndio ikawa mwanya wa wale viumbe wadogo Mamalia kutoka katika mashimo waliokua wamejificha ndani yake na kuanza kuitwala dunia, kulingana na wanasayansi wanavyosema; Binadamu alitokana na jamii ya hawa mamalia baada ya Dinosaurs kuangamizwa walitoka na kuanza kuitawala dunia kwa mamilion ya miaka na waliendelea kubadilika kutokana na kupitia mabadiliko mbalimbali ya kisayansi.
Kuna vithibitisho vingi sana vya uwepo wa Dinosaurs duniani mfano: Baadhi ya mifupa ya Dinosaurs, Meno yao, Mayai na kadhalika
Like, share and comment.
05/04/2023
Wanasayansi wanaamini kwamba sayari ya mars hapo zamani ilikua k**a dunia kabisa. Ya kwamba kulikua na mito, bahari, miti, viumbe hai na kadhalika. Hii ni baada ya rovers zinazotumwa kuchunguza sayari hii kugundua baadhi ya njia za mito, maziwa na Bahari zilizokauka.
Wanasayansi wanasema kwamba Mars ilipoteza uwezo wake wa kuwa k**a dunia baada ya kupoteza anga lake zito ambalo lilikua linailinda sayari hii dhidi ya mionzi mikali na hatari ya Jua japokuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina kujua ni sababu gani zaidi zilizopelekea tukio hili
Baadhi ya watu mbalimbali wanaamini kwamba zamani mars ilikua na viumbe ambao ni k**a sisi binadamu na waliweza kuharibu sayari yao wenyewe baada ya kupigana vita kali ya Nuclear kitendo kilichoteketeza kila kitu na kuharibu anga zito lililokua linailinda sayari hii. Yani ni k**a ambavyo Urusi na Ukraine waamue kutumia asilimia ndogo tu ya Nuclear zao kitendo kitakacho kausha dunia yote na kuangamiza kila kitu na kuifanya dunia kuwa k**a Mars.
Like, Share and Comment
Genius and Fun
04/04/2023
Haya ni moja kati ya mawe yalioishi kwa miaka mingi sana hapa duniani, yanapatikana nchini Canada na umri wake unakadiriwa kuwa ni miaka billion 4.
Je ulishawahi kujiuliza kua, hapo ulipokaa ni nini kilikuepo miaka 1000 iliyopita, au ni watu gani walikua hapo, au ni viumbe gani vilikuepo hapo na kadhalika!?....
02/04/2023
Hii ndio Crater kubwa duniani kati ya zile Crater zilitengenezwa baada ya vimondo kudondoka katika uso wa dunia,
Jina la Crater hii ni 'Vredefort Impact Crater', inapatikana South Africa, ina ukubwa wa diameter 300Km.
Kimondo kilichosababisha Crater hii kinakadiliwa kuwa na ukubwa wa diameter 10km na kilidondoka takriban miaka billion 2.02 iliyopita, katika kipindi ambacho hakukua na binadamu yoyote hapa duniani na hata viumbe Dinosaur 🦕 bado walikuwa hawajaanza wanatawala dunia.
31/03/2023
Hivi ulishawahi kusikia kuhusu Neutron star?
Neutron star ni nyota iliyoundwa baada ya nyota yenye uzito kwanzia mala 1.4 hadi 3 zaidi ya jua letu kuishiwa mafuta yake na kulipuka (Supernova) na hatimae kubakiza kile kiini cha ndani kinachoundwa zaidi na chembe chembe ziitwazo Neutron. Neutron star ina ukubwa wa kwanzia diameter 10km hadi 20km lakini uzito wake ni zaidi ya mala 1.4 ya uzito wa jua letu.. yani ni k**a ulichukue jua letu alafu ulikandamize uliweke litoshe katika ka kijiji tu,, Neutron star inatoa mionzi mikali na mingi sana ukilinganisha na jua letu maana mionzi ambayo inatolewa na neutron star kwa sekunde 1 ni sawa na mionzi inayotolewa na jua kwa mwaka mzima, pamoja na hayo, neutron star inatengeneza magnetic field zaidi ya mala million ukilinganisha na magnetic field zinazotengenezwa na dunia
Neutron star ya karibu zaidi inaitwa J185635-3754, na ipo umbali wa takriban 400 light years (Yani mfano ukisafiri kwenda katika hii nyota kwa kutumia chombo kinacho safiri kwa spidi ya mwanga utafika baada ya miaka 400), ni umbali mrefu eeh??. Shukuru mungu nyota hiyo ipo umbali huo maana ingekua karibu, basi hakuna mtu ambae angeweza kuishi hapa duniani, mfano tu hiyo neutron star ingekua umbali wa 10 lights years! Yani ingeharibu anga la sayari zote kwenye mfumo wa jua, vifaa vingi vya ki electriki hapa duniani visingefanya kazi kabisa... sasa kwa mfano moja ya hii Neutron star ikaingia katika mfumo wa jua letu(Solar System) hapa ndio litakua balaa zito maana kwanza hatutapata hata muda wa kujua k**a Neutron star imeingia katika solar system yetu, kwasababu kutokana na electromagnetic field zinazolushwa na hizi neutron star kila kifaa cha electronic kitazimika yani kwanzia simu, Tv, satellite, ndege na vingine vyote,,, sayari zote zitaacha obiti zake yani mfano sisi tunaweza kurushwa mbali na jua hivyo kusababisha kila kitu kuganda au tukarushwa karibu na jua kila kitu kikaungua,,, matetemeko kwa wingi, volcano na vinginevyo,,, mionzi yake mikali itaua kila kitu duniani yani hizi neutron stars zinatoa mionzi mikali kiasi kwamba ukiisogelea kwa umbali hata wa kilometer 400000 mwili wako utayeyuka k**a maji au uji,,, pia kutokana na Gravity yake kuna uwezekano mkubwa wa sayari zote kufanyiwa Supergatefication, yani hapa namaanisha sayari zote zitavutwa k**a tambi na kumezwa na hii Neutron star k**a vile black hole zinavyofanya
Kuna vitu vingi angani ni vizuri kuvitazama tu kwa mbali lakini ni hatari sana k**a vikikusogelea.
Genius and Fun
30/03/2023
Ukiangalia ukuaji wa Ai (Artificial Intelligence) kwa hivi sasa Unafurahisha pamoja na kushtua kidogo.
Ai ni program za kompyuta au Machine ambazo zinaweza kufanya kazi ambazo zilikua zinahitaji akili na uwepo wa binadamu tena zinakamilisha kwa spidi na Ubora wa hali ya juu sana.
Ai zimetengenezwa kufanya kazi k**a vile Ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na hii ni baada ya Wanasayansi ku scan jinsi ubongo wa binadamu unavyofanya kazi zake k**a vile Kufikiria, kujifunza, kufanya maamuzi na kazi nyingine nyingi, zikaweza ku copiwa katika hizi Ai tena zenyewe zinaweza kufanya hizo kazi kwa spidi ya ajabu sana kutokana na kuwa zimewekewa data za vitu vyote duniani au data za kitu maalumu kilichosababisha hiyo Ai itengenezwe.
Kwa hivi sasa uwezo wa kufikiria na kufanya maamuzi wa hizi Ai ni wa hali ya juu sana mfano kuna wanahisabati wakubwa duniania walikaa wakatunga mtihani mgumu wa topic iitwayo Calculus wakaipa Ai na iliweza kufanya kwa sekunde chache tu na ikapata 100 chini ya 100, kuna Ai ambazo zinatengeneza picha zenye ubunifu wa hali ya juu, Zipo zinazotengeneza Website kwa sekunde chache tu, zipo zinazotengeneza beat za miziki, zipo zinazotunga lyrics za miziki, ,zipo zinazotengeneza vitabu, zipo Ai ambazo ukichati nazo unaweza ukadhani unachati na binadamu kumbe unaongea na roboti tu yani uwezo wa kuelewa lugha na kujibu ni wa hali ya juu sana.
Asilimia kubwa ya Ai sasa hivi ni program za kompyuta na asilimia ndogo ni marobot wenye mwili lakini ubongo wa wa robot hizi unaendelea kuboreshwa zaidi na kwa miaka k**a miwili mitatu kutakua na Ai robot nyingi zenye mwili k**a binadamu kabisa.
Kwa miaka michache baadae kuna watu wengi sana watapoteza kazi mfano:
*Jaji wa mahak**a- ni nani atakua tayari kumuajiri binadamu ambae amejaa upendeleo, ubaguzi, rushwa, stess za maisha badala ya kuajiri Robot atakaefata sheria na haki zote za binadamu
* waalimu
* Engineers
* Producers
* Wanajeshi
* Desigers
* graphic desigers na wengineo
Pia hata watu watapenda kutoka kimapenzi na marobot badala ya binadamu wa kawaida maana robot hatakuwa na wivu wala tamaa, yani mtu mmoja atakua na uwezo wa kutoka na marobot hata 6 kwa wakati mmoja bila kuoneana wivu na kuuana.
Uoga wa watu wengi juu ya hii inshu ya Ai na Robots ni juu ya siku moja hizi robot zikijitambua zenyewe ni nani yani zikipata uelewa juu ya maisha yao na zikaamua kuwa negative na kututawala sisi binadamu. Yani k**a ikitokea hii vita basi sisi binadamu hatutaweza kutoboa hata kidogo maana hizi robots zitakua zinajua kila kitu kuhusu sisi mfano. Uoga wetu, udhaifu wetu, jinsi ya kutuangamiza, kitu gani tunaweza kufanya kuwaangamiza na kadhalika
Tutaendelea kuzungumza zaidi.
Genius and Fun
Like, Share and Comment.
29/03/2023
Kwa uzoefu wangu katika maisha na katika sayansi na teknolojia, nimegundua kuwa asilimia kubwa ya watu ambao hugundua vitu mbalimbali huanza kwanza kwa kujiuliza maswali ya kijinga na kipuuzi sana kwa wakati huo...
Mfano: Isaac Newton aligundua Gravity baada ya siku moja kukaa chini ya mti wa Maapple na apple moja likadondoka chini, akajiuliza 'Hivi ni kwanini Hili apple limedondoka chini badala ya kudondoka kwenda juu"? Hili ni swali la kijinga sana ukikaa na kulifikiria.. pia kuna mifano mingine mingi sana k**a
- Alietengeneza ndege alianza kujiuliza "Hivi na sisi tunaweza kupaa k**a ndege"?
- alietengeneza simu alianza kujiuliza "nifanyeje ili watu waweze kuongea live hata k**a wako nchi au mikoa tofauti"
-Aliegundua camera alianza kujiuliza hivi ninaweza kutengeneza kifaa kitakachokuwa kinarekodi matukio yote ili mtu badaae akitaka kuyaona matukio hayo ayaone kwa uhakika...
☆ Hayo yote ni mojawapo kati ya maswali ya kijinga na kupuuzi ambayo watu walijiuliza kwa kipindi hicho hadi kupelekea ugunduzi mkubwa na ukitaka kuamini we Imagine tu umefanikiwa kurudi miaka 1000 iliyopita alafu uwambie watu kuwa baadae tunaweza kupaa k**a ndege, watu hao watakutukana na watakwambia labda siku tukienda mbinguni Mungu atatupa mabawa ndio tutapaa, au uwambie kuwa baadae tunaweza kuongea moja kwa moja mtu hata k**a upo dar es salaam na mwenzako yupo new York City watakuona wewe umechanganyikiwa kabisa, au uende na Camera uwapige picha na video, bas waanza hata kukuabudu k**a mungu maana ni jambo la ajabu sana.
Sio katika sayansi na teknolojia tu, hata katika maisha ya kawaida au biashara usiogope kujiuliza swali la kipuuzi maana haijalishi ni kuhusu kitu gani lakini ukiweka akili, muda na juhudi za kutosha basi jambo lako litafanikiwa tu.
28/03/2023
K**a vile ambavyo kila kiumbe kitaonja mauti ndio hivyo hivyo pia hata nyota zote angani zitaonja mauti, Jua letu pia ipo siku litaonja mauti na hii ni baada ya kutumia kiwango chake chote cha mafuta kilichopo ndani yake. Zifuatazo ni baadhi ya hatua za kifo cha jua letu
1. Jua litakapo tumia Hydrogen yote iliopo ndani yake litabadilika na litakua 'Red Giant' au 'Jitu Jekundu'😀 Yani katika hatua hii jua litapanuka isivyokawaida hadi kufika hatua ya kuzimeza sayari zote za karibu yake, hapa naongelea sayari ya Mercury, Venus na hata dunia yetu itamezwa na k**a kutakua na wanadamu duniani, bas hapo ndio utakua mwisho wao.
2. Baada ya hapo Jua litaiondoa sehemu yake yote ya nje kuitupa huko angani na kubakiza sehemu yake ya ndani tu hapo jua itakua nyota ndogo nyeupe saiz k**a ya dunia yetu na litakua 'White Dwarf'
3. Baada ya muda jua litaendelea kupoa hadi litabadilika na kuwa jeusi kabisa 'Black Dwarf' hapa jua litakua halina maajabu yoyote yani hapa litakua la baridi kabisa, litakua halitoi mwanga wowote na ndio utakua mwisho wake.
☆ Licha ya kwamba Jua litakufa lakini hakuna haja ya kuogopa maana kati yetu sisi sote hakuna hata mmoja ambae atakua hai katika kipindi hicho maana hadi jua linakua Red Giant hapo itakua ni baada ya miaka billion 5 kutoka sasa, na hadi linakua Black Dwarf hapo ni baada ya zaidi ya miaka Trillion hivyo ni wazi kabisa kwa kipindi hicho hata mifupa yetu itakua imekua majivu kabisa.
Genius and Fun
, , ,
27/03/2023
UNSOLVED👽
Mwaka 1969 mwanamuziki Jim Sullivan alitoa album na akaiita 'U.F.O' (Unidentified flying Object) Yani ndege zisizojulikana, ndani ya Album hiyo kulikua na lyrics za ajabu ajabu baadhi yao akiongea kuhusu jinsi anavyochukuliwa na viumbe kutoka nje ya dunia (Aliens) na kuiacha familia yake kwenda sehemu mbali mbali..... Miaka 6 Baadaye,Jim Sullivan alipotea bila mtu yoyote kujua alipo, ni gari lake tu ndio lilikutwa limetelekezwa jangwani Roswell New Mexico sehemu ambayo mwaka 1946 inaaminika lilitokea tukio kubwa la kuanguka kwa ndege ya Aliens
Hadi hii leo hakuna mtu yoyote aliewahi kuelewa ni kitu gani kilimtokea Jim na alielekea wapi, ..hivyo bas linabaki k**a moja ya matukio ya ajabu ambayo hayajapata ufumbuzi hadi hii leo.
Genius and Fun
Like
Share
Comment
26/03/2023
Nyumba za Uyoga Mwezini🌑
Ni hakika kabisa, kwa miaka michache ijayo wanadamu watakuepo katika sayari ya mars pamoja na mwezini au katika sayari nyingine nyingi, na kwa hali inavyoendelea hivi sasa ni wazi kuwa hiyo ndoto ya mwanadamu kutawala sayari mbali mbali zaidi ya hii sayari yetu ya dunia ipo katika sehemu nzuri na leo nitaelezea kidogo kuhusu mpango wa nasa wa kutengeneza nyumba za uyoga katika sayari ya mars na mwezini.
Naam, unaweza ukahisi k**a ni kichekesho lakini kuna watu wapo serious sana katika kuuweka huu mpango wa nyumba za uyoga uwe katika uhalisia. K**a tunavyojua, Uyoga sio mmea bali ni tunda la kiumbe aitwae FUNGI au FANGAS kwa kwiswahili, Sasa Nasa (Shirika la masuala ya Anga Marekani) wanataka wachukue hiyo faida ya fangas wanaoweza kutengeneza umbo k**a zuri k**a la uyoga kuwapeleka katika sayari ya Mars au mwezini kwa ajiri ya kutengeneza makazi kwa watu watakaoenda kuishi katika sehemu hizo.
K**a tunavyojua ya kwamba ni gharama sana kuwatoa mafundi huku duniani na kuwapeleka mwezini au mars pamoja na vifaa vyote kwa ajiri ya kutengeneza makazi ya kudumu huko, hivyo basi Nasa wameamua kutumia njia rahisi na ya asilia ya kuchukua sehemu ambayo kwa asilimia kubwa hujawahi kuisikia ya viumbe fungi iitwayo Mycelia na hivi sasa wanaendelea kuwaprogram viumbe hawa ili waweze kutengeneza nyumba imara za uyoga ambazo zitakuwa imara na watatengeneza kwa shape ambayo inahitajika pamoja na furniture zote za ndani watangeneza hawa fungi bila kutuma fundi yoyote, yani hawa fungi wanatumwa tu mwezini au mars, wanawekewa tu mazingira yao vizuri wanamaliza kazi yote sisi tunaenda tu kuishi.
K**a tunavyojua kua fungi nao ni viumbe na wanahitaji chakula, maji na hewa ya oxygen,, sasa hapa ndio 'Cyanobacteria' wanaingia kazini, naam, hawa Cyanobacteria ni bacteria ambao wanauwezo wa kubadilisha mwanga wa jua kuwa maji, Carbondioxide pamoja na Oxygen, hivyo bas hawa Cyanobacteria wataandaliwa mazingira mazuri ili waweze kufanya kazi na kukamilisha kazi wakiwa pamoja na fangus Mycelia kule mwezini au Katika sayari ya Mars.
Kitu kingine kinachowafanya Nasa waendelee kutilia mkazo hii project ya nyumba za uyoga ni kutokana na kwamba nyumba hizi zinazuia mionzi hatari ya jua kuweza kuingia ndani, na k**a tunavyojua ya kua moja kati ya changamoto ya mars na Mwezi ni kwamba hazina magnetic field za kutosha kuweza kuzuia mionzi mikali ya jua, mionzi ambao inaweza kuua mtu kwa dakika chache tu hivyo hizi nyumba zinazojengwa na Fangas Mycelia zinamaana sana kwa sababu zitakua salama dhidi ya mionzi mikali ya jua.
Usisahau ku LIKE, SHARE na COMMENT
25/03/2023
Je ulishawahi kujiuliza ni kwanini tunaona vitu vikiwa na rangi tofauti tofauti hapa duniani?
Tambua kwamba, ukiona kitu flani kina rangi flani jua kwamba hiyo rangi uionayo ndio rangi pekee isiyokuwepo katika kitu hicho,....
..Ipo hivi, Jua ndio chanzo kikuu cha mwanga hapa duniani, jua hutoa mwanga mweupe na k**a tunavyotambua kwamba mwanga mweupe ni jumla ya rangi zote zinazoonekana katika upinde wa mvua,... hatua za kukiona kitu flani kina rangi flani hutokea baada ya mwanga mweupe kutoka katika jua au taa yako ya umeme kufika katika kitu hicho, k**a tulivyosema hapo mwanzo kwamba mwanga mweupe ni jumla ya rangi saba zinazoonekana katika upinde wa Mvua hivyo basi ili kitu ukione kina rangi flani inaanisha kwamba kitu hicho kimemeza au kufyonza rangi zote zilizopo katika mwanga mwaupe na kuiacha iyo rangi ambayo unaiona katika kitu hicho,. Mfano, ukiona kitu kina rangi nyekundu inamaanisha kwamba kitu hicho kimemeza rangi zote zilizopo katika mwanga mweupe na kuiachia rangi nyekundu pekee, iyo rangi nyekundu inapoachiwa na kitu hicho inaakisiwa na macho yako yatona kitu hicho kina rangi nyekundu, hivyo hivyo inatokea kwa vitu vyenye rangi zingine k**a blue na kadhalika
Kitu kikiwa kina rangi nyingi inamaanisha kitu hicho kiameachia rangi nyingi, ila kitu kikiwa na rangi nyeupe inamaanisha kitu hicho kimeziachia rangi zote zilizopo katika mwanga mweupe, na kikiwa cheusi inamaanisha kimezimeza au kuzifyonza rangi zote zilizopo katita mwanga mweupe.
Pia rangi ya kitu hutegemea material na mwanga unaomulika kitu hicho, mfano kitu kikiwa kinamulikwa na mwanga mwekundu kitu hicho utakiona kikiwa na rangi nyekundu au kitu kikimulikwa na mwanga wa blue kitaonekana cha blue, hata mtu mweusi kiasi gani akikaa kwenye mwanga mwekundu utamuona anarangi nyekundu k**a mzungu hadi uje uwashe taa yenye rangi nyeupe ndio utamuona alivyo mweusi.