Fursa Kuna ombwe kubwa kati ya maarifa anayopata mtu na jinsi ya kuyatumia katika kutatua changamoto mbalimbali katika maisha ya kila siku.

Kwa kutumia uzoefu wa miaka 10 katika ujasiriamali tunaamini kwamba tunaweza kuchangia katika kuwapa vijana wa Tanzania fursa ya kujitathimini, kuchukua hatua, na kujenga Tanzania imara kiuchumi. Kijana anayemaliza elimu msingi, elimu ya sekondari, au elimu ya juu anakuwa hana elimu mbadala kumsaidia kutumia kile alichojifunza kutatua changamoto zinazomkabili. Changamoto ya ukosefu wa ajira rasmi

ni tatizo linalokua kila mwaka. Vijana wengi wanaingia mtaani wakiwa hawafahamu wafanye nini kujipatia kipato. FURSA tunaamini kwamba elimu ya ujasiriamali ni moja ya suluhisho nyingi ambazo zinaweza kusaidia kumpa mtu yeyote maarifa na ujuzi wa kutengeneza ajira yake mwenyewe na hata kuajiri watu wengine. Ili kijana atatue changamoto yeyote ni lazima apate maarifa. Maarifa yanapatikana kwa kusoma na kujifunza. FURSA tuna miongozo 8 ambayo inamsaidia kijana kujiandaa kikamilifu kuingia mtaani na kujenga maisha yake mwenyewe – kwa kujiajiri.
1. Jinsi ya kuandaa wazo la biashara
2. Kutengeneza mpango wa Biashara
3. Kugharimu biashara katika ujasiriamali
4. Kutunza kumbukumbu katika biashara
5. Manunuzi na udhibiti wa mali za biashara
6. Mpango mkakati wa kusimamia biashara yako
7. Masoko na Mauzo katika biashara
8. Kusimamia wafanyakazi katika biashara yako

Kwa kutumia uzoefu wa miaka 10 katika ujasiriamali tunaamini kwamba tunaweza kuchangia katika kuwapa vijana wa Tanzania fursa ya kujitathimini, kuchukua hatua, na kujenga Tanzania imara kiuchumi.

Address

P. O. Box 62220 Ubungo
Dar Es Salaam
16103

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fursa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Fursa:

Shortcuts

Share