06/01/2021
KUMTUKUZA MUNGU NAYE ATAKUTUKUZA
Na.Askofu Patrick Mmeta
Utangulizi....
Kumtukuza Mungu ni kumwinua/kumpa Mungu utukufu,kumtukuza Mungu ni pamoja na kufanya mambo anayotaka Mungu tufanye(maisha matakatifu,kuwa na hofu na Mungu).
Maisha ya wokovu ni ya mtu mmoja mmoja(kwenda mbinguni ni jambo la mtu binafsi na kila mtu anatakiwa awajibikie kuhakikisha analinda uthamani wa wokovu).Wokovu ni vita.
zaburi 27:10
[10]Baba yangu na mama yangu wameniacha,
Bali BWANA atanikaribisha kwake.
walio na Yesu(waliompokea na kumkiri Yesu) wamepita kutoka mautini wameingia uzimani.
Tulio na Yesu hatupo chini ya mamlaka ya mauti(haimaanishi mauti ya kufa)maisha yetu ni ya uzima hakuna kufeli kwasababu maisha yetu yanasimamiwa na Mungu.
Yohana 5:24
[24]Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
FAIDA ZA KUMTUKUZA MUNGU
1. Mithali 4:6-9
[6]Usimwache, naye atakuhifadhi;
Umpende, naye atakulinda.
[7]Bora hekima, basi jipatie hekima;
Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
[8]Umtukuze, naye atakukuza;
Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
[9]Atakupa neema kuwa kilemba kichwani;
Na kukukirimia taji ya uzuri.
Katika mawazo yako hakikisha umuachi Yesu,ukimtendea mema nayeye anakufanyia mema.
Ili Mungu akuhifadhi inategemea ni kiwangi gani unampenda.
Kutukuzwa na Mungu ni kuinuliwa(jina lako linakuzwa).
2.Atakupatia miaka mingi yenye uzima duniani.
3.Mungu hawezi kukuaibisha ukimtukuza(wanaotaka kukuaibisha wataaibika).
*Kumtukuza Mungu ni pamoja na kutopita njia moja na waovu(wabaya).
mithali 4:14-16
*Kukaa na Mungu ni afya ya mwili na Roho.
Mithali 4:20-22
MAMBO YA KUJIHADHARI NAYO
1.Mithali 4:23
[23]Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Damu ya Yesu na maombi ndiyo yatakayokusaidia kufuta makosa yako,moyoni mwako kusiwe na mawazo mabaya.
2.Kujilinda na moyo wa ukaidi /ulimi(mambo mabaya).
Mithali 4:24
[24]Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe,
Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
3.Jilinde macho yako yatazame mbele(kujiepusha na uovu usiingie kwenye ufahamu wako).
Mithali 4:25,27
Katika maisha ya wokovu tunahitaji kuwa makini sana ili Mungu atuinue kutoka sehemu moja hadi nyingine,kwenye huduma,kazi,masomo,ndoa na familia zetu tunatakiwa maisha yetu yamtukuze siku kwa siku tumuishi yeye kila wakati....
Mungu akubariki sana....
Karibu kujifunza neno la Mungu lisilogoshiwa kanisani kwetu Kipunguni kwa Diwani jijini Dar es salaam Tanzania,Jumatatu,Jumanne,na Ijumaa saa Kumi na nusu (10.30) jioni...
Kwa maombi,ushauri na maelekezo zaidi piga
+255 713 802 120,+255 712 050 723