Talawanda Secondary School

Talawanda Secondary School Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Talawanda Secondary School, School, Msigi Talawanda, Chalinze.

Salaam toka Talawanda!Leo Ijumaa tar 1/9/2023, viongozi wa Talawanda Sekondari, Afisa Elimu Kata, Mkuu wa Shule na Makam...
02/09/2023

Salaam toka Talawanda!

Leo Ijumaa tar 1/9/2023, viongozi wa Talawanda Sekondari, Afisa Elimu Kata, Mkuu wa Shule na Makamu Mkuu wa Shule waliungana na viongozi wenzao katika ukumbi wa Kikwete uliopo kwenye Makao Makuu ya Wilaya katika KIKAO KAZI CHA TATHMINI YA MATOKEO NA KUWEKA MIKAKATI KWA MUDA ULIOBAKI.

Katika kikao hicho waliudhuria viongozi mbalimbali wakiwemo: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Mhe Ramadhani Possi, Mkuu wa Idara ya Utumishi Bw *Kilaja Alkanus, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Mama Salama Ndyetabura, Maafisa toka Idara ya Elimu Sekondari, Maafisa Elimu Kata wote, Wakuu wa Shule zote, Makamu Wakuu wa Shule, Viongozi wa Idara ya Michezo na Utamaduni pamoja na Sekritarieti ya Michezo Wilaya.

Yaliwasilishwa mengi. Kwa uchache ni tathmini ya KPI, majadiliano ya namna ya kuboresha utendaji kazi na ufaulu, masuala ya kiutumishi, kifedha, elimu maalumu na lishe, maandalizi na ratiba ya mitihani mbalimbali pamoja na namna ya kuboresha michezo mashuleni.

Mkurugenzi aliweka msisitizo kwenye maandalizi ya mitihani ya Taifa pamoja na maandalizi yake. Aliwataka watakaoteuliwa kufuata maelekezo ya semina walizopewa ili wasiharibu kazi. Pia, usimamizi mzuri wa fedha za serikali kwa wenye kupata miradi ili iendane na thamani ya fedha iliyotolewa. Mwisho alitoa pongezi na kuwatakia watumishi kila la heri.

Imetolewa na Idara ya Habari - TSS.

Salaam toka Talawanda!Tar 26/8/2023, tulipata heshima ya kutembelewa na nguli na mwalimu wa wengi, Mzee wetu Richard S. ...
30/08/2023

Salaam toka Talawanda!

Tar 26/8/2023, tulipata heshima ya kutembelewa na nguli na mwalimu wa wengi, Mzee wetu Richard S. Mabala hapa shuleni. Ni heshima kubwa kwa Shule,Wilaya na hata Mkoa wetu wa Pwani. Ni heshima kubwa kwa tuliopata nafasi ya kuonana naye. Kwa umashughuri wake hakika Shule na Wilaya yetu itatangazika Kitaifa na Kimataifa.

Huyu ndiye mwandishi wa vitabu vya MABALA, THE FARMER; HAWA THE BUS DRIVER; SUMMONS, MABALA AND THE INTERNET, na kadhalika.

Mkuu wa Shule, Mwl Godfrey Charles, alimpa historia ya shule kitaaluma, nidhamu na mazingira. Pia alimshirikisha changamoto za shule k**a ukosefu wa bweni la kiume. Alimshukuru kwa kuja na kutupa heshima hii adhimu kabisa. Historia aliyoiacha haita sahaulika kamwe. Alimuongoza katika kupanda mti ambao utabaki kuwa alama ya ujio wake.

Kaka Emmanuel Kihaule ambaye aliambatana na Mzee wetu Mabala alisema kuwa shule hii imepata fursa adimu sana kuonana na Nguli huyu na mwandishi mashuhuri. Ratiba yake ni ngumu. Ila shule hii imepata bahati hiyo. Sasa amekuwa ni sehemu ya familia ya shule hii. Anapenda watoto na mambo ya elimu. Aliahidi kutoa vitabu 20 kwa nidhamu waliyoionesha watoto.

Naye Mzee wetu alishukuru kwa kualikwa shuleni hapa na huduma alizopata baada ya kufika. Alitoa historia yake fupi. Alifika Tanzania kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya 1970. Sasa yeye ni raia wa Tanzania. Anajivunia kuwa Mtanzania. Pia, alitoa uchambuzi kidogo wa vitabu vyake. Ladha yake haielezeki. Kwa changamoto alisema amezipokea. Elimu ya changamoto na mafanikio yake itabaki kuwa ni somo kwetu sote.

Jumuiya ya Shule ilikuwa ni yenye furaha kubwa. Wageni wetu nao walikuwa ni wenye furaha kubwa.

Kwa hakika siku hii ya leo itabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu.

KARIBUNI TENA TALAWANDA SEKONDARI.
KARIBUNI TENA HALMASHAURI YA CHALINZE.

Salaamu toka Talawanda!Leo tar 24/8/2023, tulipokea ugeni wa shirika la CAMFED.Waliofika ni Afisa Elimu Kata ya Talawand...
24/08/2023

Salaamu toka Talawanda!

Leo tar 24/8/2023, tulipokea ugeni wa shirika la CAMFED.

Waliofika ni Afisa Elimu Kata ya Talawanda, Mwl Omari Kitururu, Mwl Magret Ngonyani (Mjumbe wa CDC, TM & Mwl wa Mdaula SS), LGs na CAMA. Wengine ni Mwl Salum Che-Mponda (MMS) na wanafunzi wanufaika wa CAMFED.

Walifika katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa masuala ya shirika.

Tunawashukuru sana CAMFED Kwa ufadhili huu. Kwa hakika umekuwa wenye manufaa makubwa kwa wanufaika. Tunaomba muendelee na moyo huo huo. Pia, kuona namna ya kuwashika mikono na baadhi ya wavulana wenye changamoto k**a hizo.

Asanteni sana.

© Imetolewa na Idara ya Habari -TSS.

Salaam toka Talawanda!Leo tar 23/8/2023, shuleni kulikuwa na kikao cha Bodi ya Shule.Leo ni siku maalum kwa kuwa kulikuw...
23/08/2023

Salaam toka Talawanda!

Leo tar 23/8/2023, shuleni kulikuwa na kikao cha Bodi ya Shule.

Leo ni siku maalum kwa kuwa kulikuwa na zoezi la kukaribisha wajumbe wa bodi mpya na kuaga wajumbe wa Bodi iliyoisha.

Wajumbe wapya ni (1) Mama Sara H. Mlaki, Afisa Elimu Mkoa (2) Godfrey Charles , Mkuu was Shule (3) Shabani Mbena (4) Verynice J. Shoo (5) Beatha Mchopa (6) Said Omary Zikatimu (7) Zawadi George Njema & (8) Hamadi Shaweji.

Wajumbe waliomaliza muda wao (1) Issa R. Ndugwa (Mwenyekiti) (2) Acheni J. Sudi (3) Kashma M. Kotemo (4) Zakia Bushiri (5) Brighton Christopher (6) Ally Mashuve (7) Emmanuel Mcharo na (8) Aziza Dimoso.

Yalizungumzwa mengi. Msisitizo uliwekwa katika Kupandisha Taaluma, Nidhamu na Uwajibikaji; Umoja na Ushirikiano, Kulinda mali za Shule, Kutatua changamoto zilizopo na zitakazojitokeza, nk.

© Imetolewa na Idara ya Habari - TSS.

Salaam.WANAFUNZI WA ROOM-TO-READWanafunzi wa kidato Cha tatu waliopatiwa elimu ya fedha  mada ya 5 "siku ya gulio", waki...
20/08/2023

Salaam.

WANAFUNZI WA ROOM-TO-READ

Wanafunzi wa kidato Cha tatu waliopatiwa elimu ya fedha mada ya 5 "siku ya gulio", wakiwa kwenye mauzo ya bidhaa zao walizozitengeneza wenyewe chini ya mwalimu wao mahiri Mwl Asia Ally, tar 8/8/2023.

Ujuzi na faida ya mauzo ni ya kwao wanafunzi

Video mbalimbali kukuijia.

Imetolewa na Idara ya Habari, TSS.

Salam toka Talawanda!Jana tar 19/8/2023, ilikuwa ni ziara ya Mhe Ridhiwani Kikwete (Mbunge na Naibu waziri Ofisi ya Rais...
20/08/2023

Salam toka Talawanda!

Jana tar 19/8/2023, ilikuwa ni ziara ya Mhe Ridhiwani Kikwete (Mbunge na Naibu waziri Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora) kata ya Talawanda.

Karibu tena Mh. Mbunge Ridhiwan Kikwete, ziara yako ndani ya Kata ya Talawanda imekuwa na tija kubwa kwa Wananchi wa Talawanda hasa kwa ahadi ulizozitoa kwa ajili ya Kata hii, nguvu yako katika Ujenzi wa Kituo Cha Afya Cha Talawanda ambacho Kimsingi kitakuwa ni Mkombozi Mkubwa kwa wanatalawanda.

Imetolewa na Idara ya Habari- TSS.

Salaam toka Talawanda!Tar 19/07/2023, tulipokea wanafunzi 31 wanaosomea kozi ya famasia toka Chuo Kikuu cha Kampala (KIU...
24/07/2023

Salaam toka Talawanda!

Tar 19/07/2023, tulipokea wanafunzi 31 wanaosomea kozi ya famasia toka Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) tawi la DSM Tanzania.

Walifika shuleni ikiwa ni sehemu ya eneo lao muhimu katika kufanya utafiti.

Karibuni sana Talawanda, Talawanda ni njema!

Imetolewa na idara ya Habari na Mawasiliano kwa Umma.

Tunawatakia sikukuu ya Iddi iliyo njema kwenu na familia zenu.Tufurahi kwa kula na kunywa kwa mujibu wa mafundisho ya Di...
29/06/2023

Tunawatakia sikukuu ya Iddi iliyo njema kwenu na familia zenu.

Tufurahi kwa kula na kunywa kwa mujibu wa mafundisho ya Dini.

TAARIFA:Salam Mzazi/ Mlezi! Tafadhali pokea maelekezo yafuatayo, k**a tulivyotuma kwenye ujumbe wa kawaida kupitia namba...
23/06/2023

TAARIFA:

Salam Mzazi/ Mlezi!
Tafadhali pokea maelekezo yafuatayo, k**a tulivyotuma kwenye ujumbe wa kawaida kupitia namba za Makamu M/Shule:

1. Shule itafunguliwa: -
- Tar 30/6/2023 kwa wanafunzi wote wa kidato cha Nne.
- Tar 2/7/2023 kwa wanafunzi wa hosteli.
-Tar 3/7/2023, kwa wanafunzi wa kutwa.

2.HAKIKISHA
a. Mfz anaripoti kwa wakati bila kuchelewa.
b. Mfz amefanya home package.
c. Umejaza maoni yako kwenye ripoti ya mwanao.
d. Umelipa madeni yote ya chakula kwa wa hosteli hadi kufikia tar 26/6/2023.

3. Bili ya maji ni sh 10,000/- kwa mwaka.

4.. Malipo yote yafanyike kupitia
Benki:NMB
Akanti: 21101100024
Jina: Talawanda secondary school revenue account.

5. Mahitaji mengine ya shule yaletwe kwa mujibu wa maelekezo.

6. Usafiri upo kwa 'route' mbili:
i. Dar (Mbezi) - Chalinze - Talawanda
ii. Moro (Msamvu) - Chalinze - Talawanda.

Salamu kutoka Talawanda!Ilikuwa ni tar 26/5/2023, ambapo shule ilikuwa na tukio la kuwakaribisha kidato cha kwanza 2023....
08/06/2023

Salamu kutoka Talawanda!

Ilikuwa ni tar 26/5/2023, ambapo shule ilikuwa na tukio la kuwakaribisha kidato cha kwanza 2023. Siku iliyoambatana na maonesho mbalmbali ya Taaluma, sanaa, burudani, ugawaji wa zawadi mbalimbali kwa walimu na wanafunzi waliofanya vema kitaaluma & utolewaji wa nasaha mbalimbali kuhusu kufika ufaulu ulio bora zaidi.

Waliohudhuria ni wengi: Afisa Mtendaji Kata-Talawanda, Ndg Godwin Tumaini, Mwenyekiti wa bodi, Ndg Issa Ndugwa, AEK-Talawanda, Mwl Omari Kitururu, Mkuu wa Shule, Mwl Godfrey Charles, Viongozi wa UWAWA-Umoja wa Wazazi na Walimu, Watumishi wa Talawanda Sekondari, Majirani wa Shule, pamoja na wanafunzi.

Imetolewa: Idara ya Habari na Maelezo- TSS.

Salam toka Talawanda, SS!Jana, tar 18/5/2023 baada ya kikao cha jamii. Afisa Elimu Kata ya Talawanda Mwl Omari Kitururu ...
18/05/2023

Salam toka Talawanda, SS!

Jana, tar 18/5/2023 baada ya kikao cha jamii. Afisa Elimu Kata ya Talawanda Mwl Omari Kitururu alipata fursa ya kukabidhi mtungi wa gesi uliotolewa na Mhe Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa Wakuu wa Shule. Ikiwa ni miongoni ya zawadi zilizotolewa katika kilele cha kuookea, kukimbiza na kukabidhi Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Chalinze.

Tunamshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo. Tunamuombea Mwenyezi Mungu amzidishie pale alipo punguza.

Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo- TSS.

Salamu kwa kila mmoja!Hii ndio orodha ya umoja wa wanafunzi wa Talawanda Sekondari waliojiandikisha hadi leo tar 10/05/2...
10/05/2023

Salamu kwa kila mmoja!

Hii ndio orodha ya umoja wa wanafunzi wa Talawanda Sekondari waliojiandikisha hadi leo tar 10/05/2023 toka tulipoanza zoezi hili tar 1/4/2023.

Wale ambao tumejiandikisha tujitahidi kuwaambia wengine ambao pengine hawapo kwenye mitandao ya kijamii. Ili tuweze jisajili kwa wingi. Na ambao moo humu na hamjajisajili, mjisajili sasa. Tuma: Majina yako matatu, mwaka uliomaliza/ama mdau wa maendeleo, mwaka uliomaliza, namba ya simu & mahali ulipo sasa.

Pia, Ili kukuepusha usumbufu, tafadhali, naomba utume taarifa zako kwenye 'inbox' ama namba 0683404023.

Asanteni. Karibuni nyumbani, kumenoga.

© Idara ya Habari Maelezo-TSS.

Address

Msigi Talawanda
Chalinze

Telephone

+255766316910

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Talawanda Secondary School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Talawanda Secondary School:

Shortcuts

Share

Category