Ibuga secondary group

Ibuga secondary group Ukurasa huu unawahusu waliosomea shule ya secondary Ibuga

09/12/2019

MTUNZI JUMA 0713493692 WIMBO WA AJABU SEHEMU YA TANO. "Ni ahidi hautamuonyesha mtu huu mtihani". Kwasababu nilikuwa na shauku ya kuuona huo mtihani nilijibu harakaharaka. "Sitamuonyesha mtu". "Je ukimuonyesha?". "Nichinje". "Unasema mwenyewe nikuchinje nitakuchinja kweli mimi sina masihara". Nikajikuta nacheka tu kimoyomoyo. "Aahaa ,hata nikimuonyesha mtu atajuaje kwani huyu". "We cheka tu Ila ukimuonyesha mtu utanitambua" Aliongea kwa hasira sana kiasi cha kunitisha maana muda ule nilijichekea moyoni na maswali nilijiuliza moyoni sasa amejuaje huyu k**a mimi niliwaza hivyo? "Acha kujiuliza maswali ya ajabu nimejua tu maana wewe unaonekana kutaka kumuonyesha mtu". Bado nikawa natetemeka namuhofia sana na kujiuliza moyoni "Ni jini nini huyu mbona anayajua ya moyoni mwangu?". "Sio jini bwana ,ebu acha kujiuliza ujinga ujinga" Alisema hayo kisha akanikumbatia. "Unajua Musa mi nakupenda sana, Sipendi kukupoteza naomba niahidi hutoniacha utanipenda mimi tu maishani". Alinikumbatia Kwa nguvu huku akinibusu shingoni na kunifanya nipagawe kidogo na kujikuta nasahau maswali niliyokuwa najiuliza juu yake. "Hata mimi nakupenda pia". Nilijibu kauli yake kisha akanitoa kwenye kumbatio laki akiwa kashika mtihani na booklet la majibu nilishtuka. "Eehee hizi karatasi zimefikajefikaje". "Mmmh ,kwani hukuniona nikiwa nimezishika mkononi muda mrefu" Alijibu fasta ambapo jibu lake mi sikuliridhia haraka. "Mbona sikukuona nazo". "Ulivyonikumbatia Kwa nyuma nikazificha Kwa mbele ulivyonikumbatia kwa mbele nikazificha Kwa nyuma". "Aahaa"Nikajikuta naitikia hivyohivyo tu maana huyu binti nilivyomkuta sikumkuta na karatasi hata moja sasa hii ni miujiza nilijikuta napata hofu kidogo. "Mbona unahofu na mimi mpenzi?" Aliniuliza swali ambalo nalo lilizidi kunichanganya ni kwanini amejua nina hofu. "Sina hofu na wewe" ikabidi nimjibu tu hivyohivyo. "Mtihani wenyewe wa Physics ndo huu" Alinionyesha ule mtihani nami nikaanza kuusoma harakaharaka na kujisemea "Mama yangu kwa pepa hii hatoki mtu Si Saleh wala Gerald" Mtihani ulikuwa ni mgumu sana. "Vipi umeuonaje mwepesi eehee?" Alisema huku anacheka. "Huu mtihani Janet ni mgumu sana aise k**a utatoka huu watu wengi watafeli". "Ndo huo huo utakaotoka usiseme k**a utatoka,Huo ndo unaotoka". Janet alitoa booklet ya majibu. "Haya majibu yake haya,Kuna lingine la ziada unahitaji?"Janet aliuliza. "Umesema nisimuonyeshe mtu huu mtihani, Sasa hapa kuna calculation zingine ni ngumu zinahitaji mtu uelekezwe kidogo". "Usijali nitakusaidia" Basi ikabidi tukae na Janet akaanza kufanya Yale maswali yote magumu ili kunisaidia kuelewa hata kwenye kukalili iwe rahisi. Nakumbuka siku hiyo wakati Janet ananisaidia yale maswali alipita John mbio mbio na kidaftari chake akaniona nimekaa kwenye mbuyu. "Hoya Musa vipi wewe mbona umekaa hapo peke yako wakati mambo yashavuja huko". Nikajikuta nimepigwa na butwaa maana sijui cha kujibu maana sikutegemea k**a John ataona nimekaa peke yangu ,Lakini John aliondoka harakaharaka maana ni k**a alikuwa amenishtua tu kuhusu kuvuja kwa mtihani alafu akaondoka hakujali kitu tena. Akaniacha nikiwa na maswali moyoni Inamaana John hakumuona Janet au. Nikamuangalia Janet nikamuona naye ananiangalia kwa kunikazia macho mpaka nikajikuta nahogopa nikarudisha macho kwenye mtihani haraka. Basi tuliendelea kusolve ule mtihani huku Janet akipiga story mbalimbali ili kujaribu kuniondoa hofu na kuna wakati nilikuwa nawaza vitu na akawa hayasomi mawazo yangu. Basi ile hofu ya kuwa Janet sio binadamu wa kawaida ilianza kunipotea na kuanza kuhisi ni mawazo yangu tu. Tulimaliza kusolve ule mtihani na Janet akanipa ile pepa. "Vip we uhitaji kujikumbushia?" Nilimuuliza Janet ambaye alikuwa anaondoka bila kuchukua hata mtihani ili akajisomee. "Mi nipo fiti" Janet alijifanya kukaza mikono k**a baunsa ili kuonyesha ufiti wake hali ambayo nikajikuta nacheka tu. "Basi Musa mpenzi , Tafadhari usimuonyeshe mtu,Alafu kumbuka kesho tukutane hapa kwaajili ya Mathematics" Alisema huyo huku anaondoka. Mi nikajikuta natabasamu tu yahaani hata siamini nimepata mtoto mkali namna hii tena ni kichwa kwelikweli anafanya maswali ya physics bila kubabaika. Furaha niliyonayo siku hiyo ilikuwa kubwa mno kiasi cha kusahau kabisa kumuuliza Janet kuhusu ule wimbo "Kwanini ukiimbwa ndio yeye anatokea?" Pia nilijikuta navisahau vituko vyote vya Janet na kuanza kuhisi huwenda Janet ana karoho fulani kabaya kwani hataki watu wote tufaulu nami roho mbaya siwezi, Moyoni moja kwa moja nilipanga kumshirikisha mshikaji wangu Nashon kwasababu yeye ndiye alinishtua k**a kuna fake hivyo amenipa mzuka wa kusoma nami nilitamani kulipa fadhila mshikaji wangu asije akadhalilika kwenye pepa

***Share Kwa wingi ili tusonge mbele***

07/12/2019

Hata waliofanikiwa kwanza walifeli Ila hawakukata tamaa

Address

Kamachumu
Bukoba
DEGEA

Telephone

+255742291651

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ibuga secondary group posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category