afyayamwanadamu

afyayamwanadamu Tunatoa Ushauri& Suluhisho La Maradhi Kwa Kutumia Viini Lishe ASILI

10/09/2022
Ayubu 22:Job 28 Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.  28 You will also decl...
05/08/2022

Ayubu 22:
Job

28 Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.

28 You will also declare a thing, And it will be established for you; So light will shine on your ways.


29 Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena; Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa.

29 When they cast you down, and you say, 'Exaltation will come!' Then He will save the humble person.

He raises the poor from the dust and lifts the beggar from the ash heap to set them among princes" (I Samuel 2:8)
28/07/2022

He raises the poor from the dust and lifts the beggar from the ash heap to set them among princes" (I Samuel 2:8)

Prayer Is not trying to twist God's arm to make Him do something. Prayer is receiving by Faith What He has already done.
24/05/2022

Prayer Is not trying to twist God's arm to make Him do something. Prayer is receiving by Faith What He has already done.

PART TWO. Nini Chanzo/Visababishi vya Vidonda Vya Tumbo?Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyo...
21/11/2021

PART TWO.

 Nini Chanzo/Visababishi vya Vidonda Vya Tumbo?
Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;

• Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
• Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu k**a asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
• Uvutaji wa sigara
• Kuwa na mawazo mengi
• Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
• Kunywa pombe na vinywaji vikali
• Kuto kula mlo kwa mpangilio

*Tutaelezea Baadhi ya Vyanzo/Visababishi*

*Maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori*
Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yeyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo.Aina hii ya vimelea vya bakteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 ya duodenal ulcers.
Hali hii husababishwa zaidi na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili. Matokeo ya kushindwa huku husababisha kuwepo kwa maambukizi ya kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis), maambukizi ambayo huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni/kichocheo aina ya Gastrin, ambacho ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali.
Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo k**a Parietal cells. Iwapo bakteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wa gastrin pia uharibika, na hivyo kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.

*Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs*
Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo k**a Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani prostaglandins na hivyo...

NIFANYE NINI KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO/ULCERS?Si Kila Maumivu Ya Tumbo Ni Vidonda Vya Tumbo.JE, UNAPITIA CHANGAMOTO HIZI?...
19/11/2021

NIFANYE NINI KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO/ULCERS?

Si Kila Maumivu Ya Tumbo Ni Vidonda Vya Tumbo.

JE, UNAPITIA CHANGAMOTO HIZI?
• Maumivu ya tumbo ya kuchoma au ya kunyonga ambayo huanza dakika 45 hadi saa 1 baada ya kula chakula. Mara nyingi ukinywa maji maumivu ya tumbo huisha au ukitapika au kula kitu cha alkaline mfano kulamba majivu au baking soda hutuliza tumbo.
• Maumivu haya ya tumbo wakati mwingine hukuamsha usiku wa manane hasa saa saba au nane usiku.
• Maumivu chini ya kifua (chembe moyo), ambayo hutembea mpaka kwenye uti wa mgongo. Maumivu haya hufanana na kiungulia, au maumivu ya mtu mwenye njaa kali.
• Maumivu ya kichwa Je, kichefuchefu, maumivu ya uti wa mugongo kucheua nyongo.

K**A JIBU NI NDIO FUATILIA SOMO HILI KWA UMAKINI.

Katika Somo Hili Tunakwenda Kujifunza Kwa Kujibu Maswali Yafuatayo.
1. Vidonda Vya Tumbo/Ulcers Ni Nini?
2. Nini Chanzo/Visababishi vya Vidonda Vya Tumbo?
3. Kuna Aina Ngapi Za Vidonda Vya Tumbo?
4. Ni Dalili Zipi Zinaashiria Kuwa Na Vidonda Vya Tumbo?
5. Vipimo vya kutambua Ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni vipi?
6. Nawezaje Kujikinga/Kuepuka Nisipate Vidonda Vya Tumbo?
7. Nini madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo?
8. Nawezaje Kupata Tiba Ya Vidonda Vya Tumbo?

 Vidonda Vya Tumbo/Ulcers Ni Nini?
• Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda.
• Hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus.
• Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, k**a ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.
• Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine k**a kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.....

Itaendelea.WhatsApp 0768504232

*PART THREE**IFAHAMU SIRI YA MBEGU NA GANDA LA TIKITI MAJI KWA AFYA YAKO MWANADAMU**Lakini je wajua siri ya mbegu ya tik...
10/11/2021

*PART THREE*
*IFAHAMU SIRI YA MBEGU NA GANDA LA TIKITI MAJI KWA AFYA YAKO MWANADAMU*

*Lakini je wajua siri ya mbegu ya tikiti maji*

Huenda wewe ni mmoja wa wale wanaotupa mbegu za tikiti maji - au kuyatoa kabla ya kutumia.

Hivi hapa ni vidokezo ambavyo huenda vikakusaidia kubadili mtazamo wako kuhusu mbegu za tikiti maji kwa mujibu wa mtaalamu wa lishe bora.

Hizi ni baadhi ya manufaa ya mbegu za tikiti maji kwa mwili wa binadamu

1. Zinaongeza nguvu mwilini

2. Zinaimarisha tendo la ndoa

3. Husaidia kutatua tatizo la Hedhi kwa wanawake

4. Huimarisha afya ya akili

5. hujenga Uboho

6. Ni ngao ya mwili

7. Inatibu aina mbili ya Kisukari

8. Hukuza nywele iliyokatika kwa wanawake

9. Hurekebisha ngozi

10. Afya ya moyo

Mwisho.

Kwa Ushauri Zaidi, Karibu WhatsApp
0768504232

*Part TWO**IFAHAMU SIRI YA MBEGU NA GANDA LA TIKITI MAJI KWA AFYA YAKO MWANADAMU**Kinga dhidi ya saratani*Miongoni mwa v...
10/11/2021

*Part TWO*
*IFAHAMU SIRI YA MBEGU NA GANDA LA TIKITI MAJI KWA AFYA YAKO MWANADAMU*

*Kinga dhidi ya saratani*
Miongoni mwa virutubisho vinavyopatikana kwenye tikiti maji ni kinga dhidi ya aina fulani za saratani

Utafiti hata hivyo unaonesha kuwa watu wanaokula tikiti maji wana uweze mkubwa wa kupata tiba ya saratani ya tumbo.

Kinga dhidi ya maradhi ya moyo
Wataalam wanasema kwamba ugonjwa wa moyo ndio chanzo kikuu cha vifo ulimwenguni.

Hatahivyo, imegundulika kuwa aina fulani za virutubisho hupunguza hatari ya mshtuko wa moyo na kiharusi kwa kupunguza shinikizo la damu na kupunguza mafuta mwilini.

Lishe nyingi kwenye tikiti maji zinaweza kutoa uponyaji na kusaidia katika vita dhidi ya magonjwa haya.

*Ni ngao na nguvu*

Tikiti maji huupa mwili kinga, husaidia virutubisho vinavyosaidia mwili kupambana na magonjwa na kupata kinga kutokana na magonjwa au kuumia, na hutibu uchovu na kudorora.

*Husaidia macho*
Kunywa sharubati ya tikiti maji huimarisha afya ya macho na kuyalinda dhidi magonjwa mengine mabaya ambayo huenda yakasababisha upofu.

Watu wanaokunywa juisi ya tikiti maji mara kwa mara au kuweka tone lake kwenye macho wanapokuwa wazee hupata kinga kamili ya mwili kwa mujibu wa wataalamu.

*Kuvimba kwa viungo*

Citrulline, inayopatikana kwenye tikiti maji inasaidia kupunguza kuvimba kwa viungo vya mwili. Pia inatumiwa kutengeza dawa za kuzuia kuvimba.

*Kunywa juisi ya tikiti maji kunamsaidia mtu dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Basir*

*Hurekebisha ngozi na mwili*
Vitamini A na C inayopatikana kwenye tikiti maji ni muhimu sana kwa kutoa collageni ambayo inafanya mwili kuwa laini na wa kupendeza. Pia inarekebisha nywele zilizoharibika.

*Husaidia kumen'genya chakula*
Tikiti maji ina maji mengi hivyo kuitumia kwa wingi kunasaidia kusaga chakula.

*Kunywa sharubati ya tikiti maji mara kwa mara kunasidia mwili kumeng'enya chakula kwa haraka*

*0768504232*

*PART ONE* *IFAHAMU SIRI YA MBEGU NA GANDA LA TIKITI MAJI KWA AFYA YAKO MWANADAMU*Tikiti maji ni moja ya mazao ya kifaha...
10/11/2021

*PART ONE*
*IFAHAMU SIRI YA MBEGU NA GANDA LA TIKITI MAJI KWA AFYA YAKO MWANADAMU*

Tikiti maji ni moja ya mazao ya kifahari duniani.

Tunda hili ni chanzo kikuu maji na ni muhimu kwa mwili wa binadamu.

Wataalamu wanaelezea tikiti maji k**a tunda ambalo ni muhimu sana kwa afya ya binadamu, kwasababu ina madini ya hali ya juu ya ikiwa ni pamoja ya Vitamini, Midini, Vizuia oksidi na Mafuta.

Kuna aina tano tofauti ya tikiti maji.

Lakini katika mataifa kadhaa ya Afrika, tikiti maji ni tunda maarufu sana.

Tikiti maji lina asilimia 92 ya maji, ikimaanisha kuwa wale wanaotumia tunda hilo hawana hofu ya kukabiliwa na ukosefu wa maji mwilini, anasema mtaalamu wa masuala ya lishe bora Maijidda Badamasi Burji.

Zifuatazo ni faida tisa za tunda la tikiti maji kwa mwili wa binadamu kwa mujibu wa wataalamu:

Inaongeza maji mwilini
Maji ya na umuhimu mkubwa kwa mwili wa binadamu, ndio maana watu wanakunywa maji kwa wingi ili kuboresha afya zao.

Wataalamu wanashauri matumizi ya tunda la tikiti maji ambalo lina asilimia 92 ya maji, utafidia haja ya kunywa maji zaidi.

Tunda hili pia lina madini ya hali ya juu inayosaidia mwili wa binadamu.

Vitamininamadinini mengine

Tikiti maji ni moja ya matunda na mboga ambazo zina kiwango cha chini cha mafuta.

Kiwango cha mafuta katika tunda la tikiti maji kiko chini ikilinganishwa na matunda mengine.

Kikombe kimoja cha maji ya tikiti maji kina madini aina ya Vitamini C, A, Potassium, Magnesium, Vitamini B1, B5 na B6.

0768504232

10/11/2021

Karibu Tz.

FAIDA ZA ASALI MBICHI KWA AFYA NJEMA YA MWANADAMUAsali ni chakula muhimu sana kinachousaidia mwili katika kupambana na m...
07/11/2021

FAIDA ZA ASALI MBICHI KWA AFYA NJEMA YA MWANADAMU

Asali ni chakula muhimu sana kinachousaidia mwili katika kupambana na magonjwa mbalimbali pamoja na matatizo mengine yatokanayo na uzee.

Tafiti za wataalamu mbalimbali wa madawa lishe na vifaa tiba duniani zimedhihirisha kwamba uwezo wa asali katika kutibu huongezeka maradufu k**a itachanganywa na mdalasini.

1. Asali ikichanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

2. Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.

3. Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.

4. Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha unaweza kupungua na kupotea kabisa ikiwa watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo.

5. Asali na mdalasini huaminika pia kuamsha hamu ya tendo la ndoa endapo itatumiwa kwa kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Hii inaokoa ndoa nyingi sana

6. Asali na mdalasini husaidia katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji.

7. Asali na mdalasini husaidia kupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

8. Ulaji wa asali pamoja na mdalasini husaidia kuondoa mchafuko wa tumbo uletwao na gesi.

9. Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini wakati wa kifungua kinywa husaidia kuzuia uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo pamoja na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu.

10. Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku ni muhimu pia kiafya kwani hupunguza uwe

Address

Babati

Telephone

0768504232

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when afyayamwanadamu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to afyayamwanadamu:

Shortcuts

Share