19/03/2022
Hellow!
Kwa wanazuini Kuna maswali ambayo tunatakiwa kujiuliza
1: Kwa Nini u nasoma?
2: Kwa Nini kutumia muda ambao takriba ni nusu ya muda wa maisha katika kusoma?
3: Kwa Nini kuwekeza kiasi kikubwa Cha pesa kwenye Elimu?
4: Kwa nini jamii inawaamini zaidi watu walioenda shule?
Kila mtu Ana sababu au majibu yake, lakini Mimi najaribu kukupa mtazamo wangu juu ya maswali haya
1: Kusoma ni kuondoa ujinga, ni kujikomboa na umaskini wa fikra, ni kustaarabika na kuwa mtu ambaye anaweza kuishi katika mazingira yote hasa Yale ambayo mtu ambaye hajasoma hawezi kuyamudu(Mazingira magumu)
2: Tunatumia muda mwingi Kusoma ili kujiandaa na maisha yaliyo mbele yetu katika kutatua changamoto zitakazotukabili na kufanya mazingira rafiki ya maisha ya binadam, wanyama na viumbe wengine wasio na utashi
3: Mtu yeyote anayewekeza ni kwa ajili ya kusaidia yeye kupata faida ya kiuchumi au ya kijamii, hivyo Basi tunategemea uwekezaji katika Elimu ulete mapinduzi makubwa kwenye uchumi wa mhusika na jamii kwa ujumla, lakini kubwa zaidi unasoma ili kusaidia maisha ya kijamii kwenda sawa, mfano kuusimamia ukweli, kulinda maadili n.k. ukiangalia maisha ya viongozi wengi yamejaa uoga na ukosefu wa maadili huku wakigubikwa na ulafi wa maslahi binafsi na uoga wa kusimamia ukweli kwa sababu ya kujipendekeza. Elimu inapingana na hili.
4: Sifa ya Elimu ni kulainisha Mambo magumu kuwa laini, Sasa K**a una Elimu tunatarajia huo uwezo unao, na ndio maana waliosoma wanaaminika. Sasa K**a umesoma na huaminiki katika kusaidia watu maana yake huna Elimu inayostahili au K**a kweli unayo Basi ni ya magumashi.
NB; KARIBU KISONGO TEACHERS' COLLEGE UPATE ELIMU INAYOENDANA NA UHALISIA WA MAISHA