16/04/2026
*KUMEKUCHA TAASISI YA ITRAVEL HAJJ AND UMRA KUANZA RASMI SEMINA ZA HIJJA JUMAMOSI HII, NYOTE MNAKARIBISWA*
Na Saimu Gwao
April 17/ 2026.
Mumbai nchini India
Kumekucha Sasa, kuelekea katika ibada ya Hijja 2026, Taasisi ya ITravel Hajj & Umrah, inatarajiwa kuanza rasmi semina za mahujaji kwa muda wa wiki nne kuanzia 18/04/2026, chini ya usimamizi wa Mwanachuoni Shekh Twaha Suleiman Bane..
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na mratibu Mkuu wa maswala ya Hijja wa Taasisi ya ITravel Hajj & Umrah, Sheikh Juma Kijepa, ni kwamba masomo yatakua kila siku jumamosi na jumapili kwa kila wiki.
Na masomo yatakayo somehswa ni:-
Maana ya ibada ya Hijja, na umuhimu wake, nguzo zake na wajibu wake, mbali na hayo pia kutakuwa na adabu za safari, maana ya Umrah.
Mbali na Shekh Twaha Bane, pia atakuwepo Sheikh.Muaharram Mwaita Mkurugenzi wa Africa Tv Swahili, na Shekh Yusuf Machalenga, Shekh Juma Kijepa, pamoja na Mkurugenzi Mkuu Ahmed Sharif.
Semina zitafanyika katika Msikiti wa Mwinyimkuu Magomeni Mapipa Jijini Dar es Salaam, na Mahujaji wa taasisi zote wanaruhusiwa kuhudhuria semina hiyo kwaajili ya kuijua mapema ibada ya hijja ili wasipate tabu wakiwa Makka.
Ni kawaida kwa taasisi ya ITravel na taasisi zingine kuanza mapema semina za hijja, tayaari taasisi ya Jamaraty , Tawheed, Al Safaa , Al istaqama na zingine zimekwisha anza semina za hijja.
Semina hiyo huwa inaanza saacTatu asubuhi mapema kabisa na kwa wale waliokuwa Mikoani , mtapata matukio yote kupitia Saimu Gwao tv.
Darul Arcam tv
Arcas tv.
Tutakuwa live bila chenga.