29/07/2026
Mafunzo kwa Vitendo Yanayojenga Wataalamu wa Kesho
Katika chuo cha Sila Arusha, tunaamini kuwa mafanikio ya mwanafunzi yanatokana na mchanganyiko wa elimu ya darasani na uzoefu wa vitendo. Wanafunzi wetu wa kozi ya Hotel Management wakiwa katika Practical Session katika Main Campus – Baraa kwa Mrefu, wakipata fursa ya kujifunza kwa kufanya kazi halisi katika mazingira yanayofanana na sekta ya hoteli na ukarimu.
Kupitia mafunzo haya, wanafunzi wanajifunza mbinu za kisasa za utoaji wa huduma kwa wateja, maandalizi na uwasilishaji wa vyakula na vinywaji, usafi na mpangilio wa maeneo ya huduma, pamoja na kanuni za kitaalamu zinazohitajika katika tasnia ya hospitality. Kila somo la vitendo linawajengea ujuzi, kujiamini, nidhamu ya kazi na uwezo wa kukabiliana na changamoto za soko la ajira.
Lengo letu ni kuzalisha wahitimu wenye uwezo wa kuajirika mara moja au kujiajiri kwa kutumia ujuzi walioupata chuoni. Hii ndiyo sababu Sila College inaendelea kutoa elimu inayozingatia vitendo, ubunifu na ubora ili kuwafanya wanafunzi wetu kuwa wataalamu wanaohitajika ndani na nje ya nchi.
📍 Sila College Arusha – Education for Self Employment.
Karibu Sila College Arusha, mahali ndoto zako za taaluma zinapogeuzwa kuwa mafanikio kupitia elimu yenye ubora na mafunzo ya vitendo.