12/09/2025
Biashara ina hatua 5 katika kukua. Hatua ya kwanza ni hatua ya "kabla ya kuzaliwa"
(Au kujitungisha Mimba kichwani). Hatua hii ndiyo inazaa Wazo la Biashara (Business Idea).
Wazo (la biashara) ndiyo kiini au uhai wa kiuchumi. Ukipoteza huu uhai, unakuwa umekufa kiakili.(Akili jangwa au ugumba)
Wazo la biashara ni nini? Ni taarifa kuhusu Jambo au kitu cha thamani ambacho watu wanakihitaji, na wako tayari kukigharamia au kukinunua kutoka kwako katika muundo fulani. Hata ukiamua kuwapa bure kitu hicho, watakutamkia maneno ya baraka kwasababu kitu hicho ni kitu cha thamani.
Zingatia neno "kitu cha thamani" na Zingatia neno kukiweka katika "Muundo" fulani
Je unajua jinsi ya kujitungisha mimba kichwani ili uzae wazo la kibiashara, hasa wazo kinara la kukupa upenyo wa kiuchumi au la kufanya watu wakutamkie maneno ya baraka?
Na je unaweza kutengeneza muundo unaofaa kwa wazo hilo?
Kiwanda chako cha kichwani cha kuzalisha mawazo ya kibiashara kina hali gani, na unakula taarifa gani hasa ili kiwanda kiwe na tija?
Kwanini Mungu kabla ya kuumba Dunia, alisema, "Iwe Nuru?"
Yesu alikuja duniani bila Yohana Mbatizaji kumtangulia kwanza? Uchumi mkuu unaweza kuja kwako kabla ya hekima, maarifa na ufahamu kutangulia kwanza akilini mwako? (Mithali 3:13-16)
Mungu akubariki!🙏🏿
Joseph Mayagila
Idara ya Miradi na Maendeleo TAG - Jimbo la Arusha Mashariki
1. Tunaendelea kuuza hisa za kiwanda cha maji ya kunywa cha TAG, Jimbo la Arusha Mashariki. 0715769615
2. Kuna kongamano kubwa la Wanaume wote wa TAG (CMF) tarehe 23 hadi 25 hapa TAG Betheli Christian Centre Kijenge nyuma ya Polisi (0754298 850)
3. Hakuna mtu anayeenda juu kimaisha(kiuchumi) bila kupigia magoti kitu fulani.