12/06/2025
0001. FUZU E MWANANGU
Mwanangu Zawadi,wewe ni zawadi,
Mpaji zawadi,ni Mungu mwenyezi,
Furaha ajabu, ’meshatuletea,
Nalo tumaini, kwako ‘mejengeka,
Fuzu e mwanangu, Mungu mkumbuke.
Mamangu ni Ruthu, ndiye kanizaa,
Malezi ni yeye, mengi kanifunza,
Kwako pendo langu, ladumu daima,
Wewe u mwanangu, unayependeza,
Fuzu e mwanangu, Mungu mkumbuke.
Wakati ‘mepita, ’meshaandaliwa,
Kazi ‘shafanywa, na yeye mwalimu,
Kiwango wapaa, ngazi uikwee,
Mbele endelea, safari ‘shaanza,
Fuzu e mwanangu, Mungu mkumbuke.
Kwenye fuzu lako, uwe na furaha,
Wewe wapendwa, na baba na mama,
Dadako na ndugu, wote wakupenda,
Kupita lolote, Mungu akujali,
Fuzu e mwanangu, Mungu mkumbuke.
Maneno ni mengi, kwako kusifia,
Ila ushairi, unazo sheria,
Mi’ huzifuata, makosa sitaki,
Heko binti wangu, kwayo matokeo,
Fuzu e mwanangu, Mungu mkumbuke.
Asante!