Ruo Kimani-Ruo

Ruo Kimani-Ruo Hamasisho:Kushuka kwa kiwango cha elimu nchini ni suala linalowatatanisha wote wanaohusika. Wewe upo?

15/03/2024

Nini tofauti ya aina hizi mbili za usingizi?
□ Usingizi wa pono
na
□ Usingizi wa mang'amung'amu

25/02/2024

MKEREKETWA -
Hadithi fupi ya Ustadh Ruo Kimani-Ruo
(www.ruobooks.ac.ke)

Abuu Hamadi aliketi pale mnarani saa nyingi. Kitu fulani kilimkereketa rohoni. Kitu hicho hakuweza kufafanua kwa maneno japo Nana Hamadi, mkewe, alikuwa amejitahidi kumzungumzisha ili aseme kilichomsumbua tangu Jumamosi jioni...

Angewezaje kueleza akaeleweka? Kuwa kitu mfano wa hasira za hisia za aibu na uchungu wa kujifikiria juha ndiyo yaliyokuwa yakimsumbua akilini mwake?

Kusema kweli katika siku hizi tatu za karibuni, Abuu Hamadi alijiona k**a mtu aliyeko katika safari ya masafa marefu na mara akafika katika kituo fulani cha mabas asichokifahamu na kuambiwa na utingo "Haya shuka, umefika uendako ..."

Sasa endelea kusoma kisa hiki cha kusisimua kinachojikunjua katika kurasa hizi.

Mlango uligongwa tena. Safari hii mgongaji alikuwa amegonga kwa nguvu zaidi. Kwa mbali, sauti yake ilisikika akining'ona...
25/02/2024

Mlango uligongwa tena. Safari hii mgongaji alikuwa amegonga kwa nguvu zaidi. Kwa mbali, sauti yake ilisikika akining'ona, ikiwa na kila dalili ya hofu na wasiwasi, akisema " Tafadhali nifungulie ... dakika moja tu ya muda wako ..."

~ Kiburi cha Nondo .

20/02/2024

Uhai wa lugha wataka kuchochewa. Tusikubali lugha yetu ya Kiswahili kutengwa kwa milima mirefu, mito mikubwa na misitu ya kutisha. Tuikweze lugha yetu milima, tuivushe mito na tuipe nguvu mpya ili kuifanya ionekane vizuri katika kamera za wataalamu wa ramani za lugha. Baraza la Kiswahili lahitajika sasa. Someni Ruo Books. Mwangaza upo!

20/02/2024

RUO BOOKS:
Tuisome Tuijue Tujivunie Lugha Yetu Kiswahili.

Address

Naivasha
254-20100

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ruo Kimani-Ruo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share