Kiswahili Made Simple na Mwalimu Keya

Kiswahili Made Simple na Mwalimu Keya

Share

Nafundisha Kiswahili kwa njia rahisi, ya kuvutia na inayoeleweka. Karibu kwenye JUKWAA LA KISWAHILI -jifunze na uzungumze kwa ustadi.

12/01/2026

MKUKI KWA NGURUWE MTAMU KWA BINADAMU MCHUNGU

KATIKA MAISHA NINI UNACHOPENDA KUWATENDEA WENZAKO ILA HUPENDI KUTENDEWA?
HUU NI MWAKA WA KUJITATHMINI. UNAISHI VIPI NA WATU?

12/01/2026

NATAFUTA SCHOLARSHIP YA MASTERS

12/01/2026

PEMA USIPOPEMA SI PEMA TENA

MWAKA HUU WA 2026 UWE MWAKA WA UTULIVU NA BARAKA ILI PALIPO PEMA PAZIDI KUWA PEMA NA MAFANIKIO.

11/01/2026

METHALI YA SIKU

UDONGO UWAHI UNGALI MAJI

KOSA TULIKOSOE NA KUREKEBISHA MAPEMA KABLA YA KUKOMAA. HERI TUZIBE UFA KULIKO TUJENGE UKUTA

07/01/2026

METHALI YA SIKU

MAVI YA KALE HAYANUKI.


06/01/2026

HONGERA WALIMU WETU. SHULENI MMEFIKA BILA KUCHELEWA. MOLA AWAJALIE AFYA NJEMA. NANYI TWAWATAKIENI HERI NJEMA MUHULA HUU WA KWANZA. NEEMA NA REHEMA ZAKE ZIWE JUU YENU.


'oananga

05/01/2026

HERI NJEMA

Shuleni mrudipo,
Shikeni sana elimu,
Msiiwache iende,
Twawatakieni heri njema.

Sisi wazazi wenu,
Tumejinyima mpate nyie,
Japo kidogo na hafifu,
Twawatakieni heri njema.

Tulichokosa mpate nyie,
Kikubwa hatuna kwenu,
Elimu twawapatia,
Twawatakieni heri njema.

Dua zetu twawaombea,
Jalali tulindie hawa,
Mabaya waepushie,
Twawatakieni heri njema.

Nyie watoto wetu,
Tunu Mola katupa,
Katukirimia bila gharama,
Twawatakieni heri njema.

Ja mchwa mjitume,
Matokeo tuyaone,
Msingi mwema mjiwekee,
Twawatakieni heri njema.

Ya kesho huanza leo,
Msifanye ajizi,
Juani chumieni,
Twawatakieni heri njema.

Tamati nimefika,
Kuasa sitoacha,
Utiifu ni thawabu,
Twawatakieni heri njema.

03/01/2026



Karibu tena kwenye JUKWAA LA KISWAHILI na Mwalimu Keya
Kuna mengi ya kupakuliwa.

Keti ange kila siku kupata uhondo.

Kisswahili hoyeeee! Kiswahili Kitukuzwe!

01/01/2026

OMBI LANGU
TUREJESHEE UFAHAMU, TUNAOMBA OMBI LA MFALME NEBUCHADNEZZAR. TUKETISHE TENA KWENYE ENZI. UFALME WETU ZIDISHA MARADUFU

01/01/2026

I MADE THROUGH AND I DON'T HOW I MADE IT.

31/12/2025

NAWATAKIENI MWAKA MPYA WENYE FANAKA NA BARAKA TELE.
TUMEPENDELEWA NA TUMEWEKWA TENA KWENYE KALENDA YA 2026.

30/12/2025

KATIKA MAISHA, TUJIFUNZE NENO SHUKURANI. ULICHONACHO WEWE LEO NDICHO ANACHOTAFUTA MWENZAKO.

Want your school to be the top-listed School/college in Nairobi?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address

P. O. BOX 64538-00619
Nairobi