22/05/2026
Kuna kipya huku!!
Wanafunzi watapata kuhamasishwa kuhusu thamani ya Kiswahili kwao kwa mtindo thabiti na bora wa kuleta ufanisi.
Haloooooo!
Siku zinazidi kuyoyoma!
Tunahesabu tu dakika!
Je, ushasajili wanafunzi wako?
Makani: Jabali Christian School, Barabara ya Cosmas Ndeti, nyuma ya Imaara Mall,
Imara Daima Estate - Nairobi.
Siku: Jumamosi 30 May 2026,
Saa: 8:00 AM - 4:00 PM
Mambo yatanogaaaaaa!
Fika mapemaaaaaa!!!
22/05/2026
Haloooooo!
Siku zinazidi kuyoyoma!
Tunahesabu tu dakika!
Je, ushasajili wanafunzi wako?
Makani: Jabali Christian School, Barabara ya Cosmas Ndeti, nyuma ya Imaara Mall,
Imara Daima Estate - Nairobi.
Siku: Jumamosi 30 May 2026,
Saa: 8:00 AM - 4:00 PM
Mambo yatanogaaaaaa!
Fika mapemaaaaaa!!!
07/05/2026
Hallooooooooo!
Wanafunzi wetu katika magatuzi ya Nairobi, Kajiado, Kiambu, Muranga, Makueni, Machakos mpoooo?
Hayawi hayawi hatimaye imekuwa!
Jumamosi ya 30 Mei, sote tupo mbioni kujaza ukumbi wa kisasa pale Moi Educational Centre Senior School ili kujifunza, kusikilizwa, kujiburudisha na kuelimishana!
Fika asubuhi na mapemaaaa!
06/05/2026
Ndungu zetu kutoka Jiji kuu la Nairobi na viunga vyake, Tamasha iliyoahirishwa mwezi Machi inarudi kwa kishindo!
Makani yatatangwazwa hivi punde!
Panga wanafunzi ili wajipange kuhakikisha kuwa mbwembwe za Tamasha zimeshamiri kotekote!!
Tamasha hoyeee!!!
06/05/2026
Siku k**a ya leo, mwezi kesho, tutakuwa Makini School - Cambridge and CBC Curriculum , Kisumu City kwa awamu ya pili ya kukata na shokaaaaa!!!
Umejisajili?
19/02/2026
MBIU YA MGAMBO IMELIA! 🔔
Habari zimefika!
Tarehe ni Jumamosi, 14 Machi 2026
Makani ni The Standard Group Grounds
Njooni tushuhudie burudani, vipaji na ushindani wa hali ya juu — kwa ubora na upekee wake!
Zaidi ya mashindano, wanafunzi watanufaika na:
1. Uelekezaji kuhusu taaluma mbalimbali
2. Kuangaziwa kupitia Radio Maisha (Nuru ya Lugha) na KTN Home
3. Ukaguzi wa kiafya: macho, shinikizo la damu na BMI
4. Uigizaji wa moja kwa moja wa Wema Hauozi jukwaani
Wanafunzi wasajiliwe kulingana na vitengo na viwango vyao.
Usikose — hii ni fursa ya kipekee!
25/12/2025
Ujumbe wa Heri na Shukrani kwako🫵
Tunazishukuru kwa dhati shule zetu washirika, walimu, na wanafunzi kwa kuamini Tamasha ya Ulimbwende wa Kiswahili k**a jukwaa la kufufua fahari na nafasi ya Kiswahili. Kupitia ushirikiano wenu, tumetangamana kwa karibu na zaidi ya wanafunzi 8,000, walimu na wataalamu zaidi ya 500 na shule yapata 100 tukikuza maisha, kuamsha hamu na vipaji, na kukuza mapenzi ya dhati kwa Kiswahili.
Asanteni walimu kwa kuilinda na kuifundisha lugha, shule kwa ushirikiano thabiti, na wanafunzi—nguvu ya Tamasha—kwa ubunifu, ujasiri na ubora wenu.
Tunapoelekea mbele, tunaahidi kuimarisha ushirikiano, kupanua wigo, na kuendelea kuinua ubora na fahari ya Kiswahili.
Asanteni sana—mema zaidi bado yapo mbele.
27/08/2025
Waungwana mpo?
Asanteni sana wanatamasha!!!!
Mlitupa mirejesho na sasa ni wakati wa kutimiza yote!
Tamasha ya Ulimbwende wa Kiswahili-Sauti ya Mtoto wa Kiafrika, imefika na kutua.
Mara hii tunafanya tofauti!
Tunaangazia _mabadiliko ya tabianchi_ kwa kushirikisha wanafunzi katika mashindano yafuatayo:
1. ulumbi,
2. ngano na hadithi mbalimbali,
3. imla,
4. ushairi,
5. mijadala,
6. hotuba,
7. maigizo na mashindano ya mitihani kwa watahiniwa wa KPSEA na KJSEA.
Kaulimbiu: Kiswahili, Daraja la mabadiliko ya tabianchi.
Kila mwanafunzi atahusishwa katika kila hatua!
Kilele cha yote ni upanzi wa miche ili kufanya Kiswahili kuwa daraja bora la mabadiliko ya tabianchi.
Panga wanafunzi wako kwa kurejelea viwango vilivyowekwa zaidi ya burudani na wasilisho kuegemea kaulimbiu ya siku.
Ulizia barua upate maelekezo kamili.
Mshindi katika kila kundi na kiwango, atatuzwa live katika hafla itakayopeperushwa live na KTN, Radio Maisha na washirika!
Tuzo za vyeti vitakuwa vya moja kwa moja jukwaani!
Burudani itazidi kiwango chetu unachokijua!
Wanafunzi kuanzia gredi ya tatu wanashiriki. Siku ni Jumamosi, tarehe ikiwa Oktoba 4!
Mlete mwanafunzi aelimike, aburudike na afaharikie lugha katika mabadiliko haya ya tabianchi.
Tufanye uamuzi wa kufaa! Tufae vizazi vijavyo!
07/07/2025
Leo ni Siku ya Kiswahili Duniani!
Tunapoadhimisha siku hii, ni vyema kufahamu kuwa kwa sasa Kiswahili kina wazungumzaji wapatao milioni mia tano duniani!
Je, Artificial Intelligence katika Kiswahili ni nini?
Sema nasi!
29/06/2025
USIKU WA MSWAHILI UMEFIKA!!
Stella alirudi tarehe 17 mwezi wa 5 mwaka huu. Sasa ni awamu yake Freshley kumweka kwa umma. Je, atamtambua Stella ama Wakesho?
Ukishangaa basi ujue vijiweni hamruhusiwi kuwa na jino la pembeni ama Zuhura atawapanga.
Lipia tiketi kupitia *826*125 # ama kupitia kiunzi: https://little.africa/events/125 au kwa kufuata maelezo kwenye bango ili tumwone kwa pamoja ama Stella au Wakesho huku tukuburudika kwa vyakula vyenye asili ya kipwani!
Chondechonde!
25/06/2025
🌙✨ USIKU WA MSWAHILI 2025 ✨🌙
🔥 Usiku wa Utamaduni, Ladha na Ubunifu wa Kiswahili! 🔥
📅 Tarehe: Jumamosi, 5 Julai 2025
🕕 Muda: Saa 12 jioni (6 pm) – Saa 9 asubuhi (3 am)
📍 Makani: Carnivore Grounds – Simba Salon, Barabara ya Lang’ata, Nairobi
🎭 Kaulimbiu: Lugha Yetu, Akili Yetu, Dunia Yetu
Karibu kwenye usiku wa kipekee ambapo utamaduni wa Kiswahili unang'ara, ladha za pwani zinapendeza, na ubunifu wa Kiafrika unapata jukwaa lake! Hii ni fursa ya kusherehekea Kiswahili k**a chombo cha umoja na maendeleo.
🎟️ KIINGILIO:
🔹 Kawaida: Ksh. 1,000
🔸 VIP: Ksh. 2,500
Ada inajumuisha vocha ya chajio!!
💳 JINSI YA KULIPIA:
🌐 Bonyeza hapa: https://little.africa/events/125
📱 Au piga: *826*125 # kwenye simu yako
🌟 MATUKIO MAKUU:
✅ Mlo wa Kiafrika wenye ladha za pwani
✅ Vyakula vya Kiswahili (street swahili buffet)
✅ Maonyesho ya mavazi ya kitamaduni
✅ Ushairi, muziki, ngoma na sarakasi
✅ Uzinduzi wa Tamko la Kiswahili
✅ Mavazi: Vaa kitamaduni, kiasili au kwa mtindo wa pwani
🎉 Hii si hafla ya kawaida — ni sherehe ya utambulisho wetu, lugha yetu, na matumaini yetu ya kesho.
📢 Alika marafiki zako, valia kwa fahari ya Kiafrika, na tukutane Carnivore kwa USIKU WA MSWAHILI wa kukumbukwa!