Jifunze Kiswahili Na Bi Mercy

Jifunze Kiswahili Na Bi Mercy Karibu kwenye "Jifunze Kiswahili na Bi Mercy”: Safari ya Kujifunza Kiswahili"!

Jiunge nasi kwenye safari ya kusisimua tunapochunguza miujiza ya lugha ya Kiswahili. πŸ˜„

22/05/2026

Je, unajua kutumia wakati ujao kwenye Kiswahili? πŸ‘€πŸ“š

Leo tunajifunza mifano rahisi:
βœ… Mimi nitaogelea 🏊🏽
βœ… Mimi nitacheka πŸ˜„
βœ… Mimi nitasoma πŸ“

Karibu darasani tujifunze Kiswahili kwa njia rahisi na ya kufurahisha pamoja na Bi Mercy πŸ‡°πŸ‡ͺ✨

20/05/2026

Unajua jinsi ya kutumia na kukanusha β€œmimi nitaoga” kwenye Kiswahili?

Leo tunajifunza:
✨ Ni β†’ Nafsi ya kwanza
✨ Ta β†’ Wakati ujao
✨ Oga β†’ Kitenzi

βœ… Mimi nitaoga
❌ Mimi sitaoga

Karibu ujifunze Kiswahili kwa njia rahisi na ya kufurahisha pamoja na Bi Mercy

15/05/2026

Unachanganya matumizi ya β€œnita…” kwenye Kiswahili?

Karibu darasani na Bi Mercy tujifunze wakati ujao nafsi ya kwanza umoja kwa njia rahisi na ya kueleweka.

Leo utajifunza jinsi ya kutumia maneno k**a:

βœ… Nitasoma
βœ… Nitakula
βœ… Nitaenda
βœ… Nitafanya

Somo hili litakusaidia kuzungumza Kiswahili kwa ufasaha zaidi kila siku

03/04/2026

Yeye aliandika ✍🏽 lakini hakuandika, yeye alilala 😴 lakini hakulala β€” jifunze kwa urahisi jinsi ya kukanusha nafsi ya tatu umoja katika wakati uliopita kwa kutumia haku- 😊

πŸ“š Kazi ya ziada:
Kanusha sentensi hii πŸ‘‰ Yeye alicheza

Tuandikie jibu lako kwenye comments πŸ‘‡

31/03/2026

Yeye alisoma πŸ“š lakini jana hakusoma β€” jifunze kwa urahisi jinsi ya kukanusha nafsi ya tatu umoja katika wakati uliopita kwa kutumia haku- 😊
Wewe unaweza kutunga sentensi gani? Tuandikie kwenye comments πŸ‘‡

27/03/2026

Yeye alipika 🍲 lakini jana hakupika β€” hapa tunajifunza jinsi ya kukanusha nafsi ya tatu umoja katika wakati uliopita kwa kutumia haku- kwa urahisi 😊

Wewe unaweza kutunga sentensi gani? Tuandikie kwenye comments πŸ‘‡

19/03/2026

Karibu tena kwenye Jifunze Kiswahili na Bi Mercy 😊
Leo tunarudi darasani kujifunza pamoja.
Jiandae kuongeza ujuzi wako wa Kiswahili hatua kwa hatua!

10/11/2025

πŸ“š Somo jipya la Kiswahili: Kukanusha Wakati Uliopo – Nafsi ya Tatu Umoja (yeye) ✍🏽

10/11/2025

Mfano wa kwanza πŸ‘‡πŸ½

Wao wanacheka πŸ‘‰πŸ½ Wao hawacheki

Kumbuka: wana- hubadilika kuwa hawa- unapokanusha.

πŸ‘‰πŸ½ Tunga sentensi zako kwa nafsi ya tatu wingi na kanusha. Andika majibu yako kwa maoni!

10/11/2025

Karibu tena kwenye Somo la Kiswahili na Bi Mercy.

Leo tutajifunza jinsi ya kukanusha wakati uliopo nafsi ya pili wingi .

Hii inakusaidia kujua namna ya kutengeneza sentensi sahihi unapoongea na watu zaidi ya mmoja

Address

Nairobi
Nairobi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jifunze Kiswahili Na Bi Mercy posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share