15/01/2024
Jungu kuu yaomboleza kifo cha mwanzilishi wa chuo tajika cha Nairobi Institute of Business Studies (NIBS) , Lizzie Wanyoike Preparatory School na hoteli ya Emory.
Atakumbukwa kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha masomo yanazingatiwa k**a pembejeo ya maendeleo na nasaha zake anuwai kwa wengi hasa wazazi na vijana π
Makiwa kwa familia, marafiki, wafanyakazi wake na wengi wa wanafunzi waliopitia mikononi mwake π
Mungu ailaze roho yake Liz Muthoni Wanyoike mahali pema π
13/01/2024
Naamini hakika, ipo siku itafika
Tope mnazonipaka, nitatakasika
Wala donge sitoweka
Mwamini nina nia njema, kwenu nyie
Sijui niwaweke fungu gani, viumbe mhesabike?
La faraja kwenu dhiki, lema kwenu huwa mbaya!
07/12/2023
Mwaka umekuwa wa ajabu βΊ
Uhaba wa fedha, wingi wa ukak**avu!
Wingi wa uhifadhi wa mazingira tumeufanya kukabiliana na athari za tabianchi π±
U hali gani π?
20/04/2023
Mwambaje?
Kwetu kwema.
Muda mwingi tu umepita, tukajishughulisha na upanzi wa miche ya miti na kuitunza.
Je, wajua umuhimu wa miti katika udhibiti wa makali ya tabia nchi (climate change)?
06/12/2020
Inanitia moyo kuona kaka zangu tayari wamepata makali tosha kujibwaga katika uwanja wa utangazaji na pia uandishi wa habari.
Hongera Maina Dominic Dommy na gwiji mwezako wa lughaπ― β
05/09/2020
Vipi ndugu zetu?
Niwaulize hivi, nyinyi hushabikia aina gani ya muziki?
Kwangu Taarab yanituliza na kunipa raha isiyo kifani π₯
Kati ya wasanii bingwa ninaowaenzi ni :
1.Malkia wa Mipasho Khadijah Kopa
2.Rukia Ramadhan
3. Mzee Yusuf
4. Omar Kopa
5. Patricia Hillary
Taarab ni muziki π₯π₯π―
30/06/2020
Mwambaje wapenzi wa Kiswahili?
Somo la leo ni fupi tuβΊοΈ
Aina za Nambari:
1.Nambari Witiri :Odd numbers
2.Nambari Shufwa:Even numbers
3.Nambari Tasa :Prime numbers
Umejifunza jipya?
Nijuze kwenye "Comments "
13/10/2019
Asalam aleikum wenzangu,
Jungu Kuu lingali tisti hata k**a posti ni adimu.
Tungali kwenye lengo.
Mola awajalie Siku njema.
01/01/2019
Salamu za kwangu za Mwaka mpya pokeeni.
Ni Mwaka ambao Mola ametujalia kufanikisha malengo yetu.
Nawaombeeni Maulana awape upendo, furaha na amani tele.
Uwe mwaka wa ufanisi katika nyanja mbalimbali.
Mwaka mpya wenye Fanaka.
Happy, Great, Prime 2019.
24/12/2018
Wakaa wa Krisimasi umewadia,
π β₯ π β₯ π β₯ π β₯
Saa chache tu tusherehekee kuzaliwa kwa Yesu Mwana wa Mungu,
Anayetuopoa kutoka maovuni,
Nawaombea furaha na amani tele wadau.
βββββββββββββββββββββββ
Tule, Tunywe, Tucheze, Tujipe raha kwa kipimo.... Huu ndio muda murua wa kujituliza roho.
π
π
π
π
π
π
π
π
π
π
π
π
π
Nawatakia Krisimasi ya furaha na mwaka Mpya wenye fanaka ziso idadi
ππππππππ
25/11/2018
Jumapili ya kufana wenzangu,
Tumshukuru Maulanaπ
Uzuri wake wastajabisha.
πππππππ