23/06/2023
HADITHI IMEANDIKWA NA
TOPISTA ATIENO
DARASA LA NANE.
KUPAMBANA NA MWIZI
Nilipokuwa nimelala niliskia nyayo za mtu akitembea taratibu akikaribia nyumba yetu. Niliingiwa na uoga k**a kunguru na kujifunika blanketi gubigubi. Moyo wangu ulikuwa unadunda mithili ya dramu ya Afrika mashariki. Nilitamani sasa kukuche, lakini wapi? Usiku huo ulikuwa mrefu na mweusi mithili ya makaa.
Mwizi ambaye alikuwa anatembea kando ya nyumba yetu, alikuwa unju hata angeweza kupita kwa mlango akiwa amesimama. Niliamka taratibu kuenda chumba cha wavyele wangu, kumuita baba. Nilikuwa na uhakika k**a mauti kuwa baba na mama hawajui nini kinachoendelea.
Nilipokuwa nikikaribia chumba cha wavyele wangu, nyaya za umeme zilikatwa. Kukawa na giza totoro hadi huwezi kuona kitu chochote. Hapo ndipo niliamua kupiga unyende kuwashtua wavyele wangu. Walitoka inje ya chumba chao wakiwa na hofu telee kunihusu.
Baada ya dakika chache, wavyele wangu kutoka chumbani mwao umeme ulirudi mwaa bila ya kutarajiwa. Niliwaelezea kinaga ubaga nilichosikia wakati nilikuwa nimelala. Baba akaenda chumbani na kuchukua fimbo ya kuenda kupambana na mwizi. Alipiga milundi na kuelekea inje. Pia yeye alikuwa muoga lakini jukumu lake ni kulinda familia yake.
Alikumbuka wasemalo wahenga, usipo ziba ufa utajenga ukuta. Kabla ya jambazi kuingia kwa nyumba yetu, baba alitoka inje kwa ujasiri sana. Ni nani yuko hapa? Na nini unataka nyumbani kwangu? Hakuna aliyejibu. Jambazi tayari ameshaingia kwa nyumba. Alipitia kwa mlango wa nyuma na kupenya ndani.
Wakati sisi tulikuwa inje, tukiduwa na kubung’aa k**a waliyeona mabaki ya adamu na hawa. Mwizi alikuwa ameshachukua chukuwa vitu vya thamani peke yake, akaacha zile ambazo hakuwa anahitaji. Alitungoja kwa hamu na gamu tuingie ndani ya nyumba, iliatoke aende.
Kwa bahati mbaya alikuwa amekanyaga matope na akaingia akiwa amevaa viatu, tulifuata nyayo zake na kutambua alitotoka. Lo! Kumbe ni jirani yetu Hasana, anatutendea kitendo hiki. “hatajua mimi ni nani?” baba alisema kwa mori.
Baba alipotia nanga kwake na kubisha mlango. Hata hakumkaribisha, alianza kutingika miguu. Alijua kuwa chuma chake kimotoni. Alikuwa akiongea akisita sita k**a aliyetoka kushtaki uchafu na maji baridi, mithili ya barafu.
Hassan alithani kesi hii haimuhusu sikio wala dewe, lakini alikuwa mmoja wa washukiwa. Baba alipoingia ndani ya nyumba yake alipata vitu vingi. Alitaka kukimbia mtego wa panya lakini alinaswa. Yamkini mbio za sakafuni huishia ukingoni.
HADITHI IMEANDIKWA NA
TOPISTA ATIENO
DARASA LA NANE.