Najivunia Kiswahili

Najivunia Kiswahili

Share

This page is wide and covers matters from education to politics by presenting them poetically- Kiswahili.

23/04/2023

After a sermon on Ecclesiastes 1.
Everything happens at its own time and season.
Nakuru North environs.

07/03/2023

Hivi karibuni,
kuna habari za kipekee zinazopeperushwa kwenye televisheni - Mwenge wa kaunti. Kipindi hiki kinaendelezwa na Mashirima Kapombe. Kwangu hii ni hatua nzuri na pevu na ya kipekee Kwani ni motisha Kwa wananchi-WASAKATONGE, wanaoambulia na wakati mwingine kupata TONGE , wakatia mdomoni na kushtaki njaa. Ni suala la kuleta motisha hasa kwa vijana ambao asilimia yao haimithilishwi hata na siafu....Hongera Kwa magavana Mashujaa,ambao wamedhihirisha ukuaji mkuu wa uchumi. Nitakumbusha kuwa Ukipanda pantosha utavuna pankwisha na ole wako unayekisa kutumikia raia. Siku ya Kiama itakuja ya kutambua mbichi na mbivu . Utaondoka pasipo kutaka, utabeba msalaba wako Kwa ulochombeza mfukoni....
Fanyeni Kazi Kwa UMMA,ewe kiongozi mteule
Akija raia kuamua, hakika utaona cha mtemi
Kidogo kidogo hatima, hujaza kibaba kauntini
Ushuru unapotoza , mikakati uyaweke.
Inshallah.
Malenga Chipukizi.

07/04/2022

Asalaam Aleikum Varamatulahi, Ni Salamu za ndugu zetu waislamu. Katika sherehe hii yao ya kufunga ,utawaona namna walivyo wakarimu ndugu hao. Watatoa Bila masharti kwote kuanzia mavazi Hadi vyakula kufikia wasiojiweza. Wakenya wenzangu tujifunze kitu kutoka ndugu hao. Amina.

13/03/2022

Najuvunia Kiswahili yakuletea

04/01/2022

Hujambo Kwa niaba ya kina baba wanaopigania Likizo ya Baba Mtoto, hili langu rai. Karibu.
Amini usiamini, haki zetu tunataka
Mlo sema msomeni,tazameni twafumbuka
K**a kweli mwauzeni , usawa je yauzika?
Kina baba wa kortini, Likizo ya baba toto

Leo peupe someni, habari kuaminika
Mepeperushwa jioni, televisheni tajika
Mswada upo mezani,kuamuliwa na haji
Kina baba wa kortini, Likizo ya baba toto

Hata kabla kubalini, mnatupinga haraka
Eti likizo ya nini, na malezi hushirika
Hakuna sikilizeni,haki haki zetu kaka
Kina baba wa kortini, Likizo ya baba toto

Kina baba tu kortini,Likizo yetu ishaka
Pia Sisi walezini,kupika kuosha kaka
Enyi hao wavivuni, pigia debe mkataka
Kina baba wa kortini, Likizo ya baba toto

Kina mama tuungeni,twafahamu ongezeka
Mmekwea viungani,uongozi mamlaka
Kortini hata vyuoni, umoja wenu twataka
Kina baba wa kortini, Likizo ya baba toto

10/12/2021

Kiswahili Kitukuzwe.
mwanafunzi.

08/12/2021

learning.

24/03/2021

Makiwa Watanzania.

Hujambo hili ni shairi langu Kwa watanzania
"Wema hulipwa kwema, kote hata Kizarani

Kilio maombolezo, hewani ilitanda wa
Jeshi bila bembelezo, walishika doria pa
Toka Chato hadi mwanzo, umma ulijitokeza
Wema hulipwa kwema, kote hata Kizarani

Watanzania na ujamaa, kweli hao Ni taifa
Undugu nao umoja, tuhimize kila kukicha
Iwapo hivi unajibeza, huwajali wale wanyonga
Wema hulipwa kwema, kote hata Kizarani

John pombe magufuli, historia atabakia shujaa
Mlolongo hadi Busisi, kupewa mwisho heshima
Wadogo wakubwa pi, waliomboleza Kwa simanza
Wema hulipwa kwema, kote hata Kizarani

Shukrani. Roho yake Mola ailaze mahali pema peponi

24/03/2021

Hili ni ombi langu tunapoomboleza na ndugu zetu watanzania

Want your school to be the top-listed School/college in Kericho?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Bomet
Kericho