Uislamu NDIO DIRA Yangu

Uislamu NDIO DIRA Yangu

Share

Dr Saeed kide alzahary
Mawasiliano : +20110 447 2103

12/08/2025
27/07/2025

📚 Jifunze Kiarabu Ndani ya Miezi 6 Tu! 🌙
Unataka kuzungumza na kuelewa Kiarabu kwa urahisi? Hii ni nafasi yako ya kipekee!

🕰️ Kozi ya Miezi 6 Tu – Mtandaoni
💸 Ada: Dola 10 tu kwa mwezi
🎁 Siku 3 za kwanza ni BURE – Jaribu kabla ya kulipa!
💻 Masomo hufanyika mara 4 kwa wiki kupitia mtandaoni

✅ Inafaa kwa anayeanza au mwenye uelewa wa msingi
✅ Njia rahisi, ya kisasa na inayolenga matokeo
✅ Unasoma popote ulipo – kupitia simu au kompyuta

📲 Wasiliana nami kwa WhatsApp:
📞 +20 110 447 2103

👉 Anza leo – jifunze lugha ya Kiarabu kwa njia nyepesi, nafuu na yenye tija!

---

23/07/2025

Ya ALLAH, give me eyes that see the best in people, a heart that forgives the worst, and a soul that never loses faith....

~ A'ameen!!

17/07/2025

TAFAKARI UMRI WAKO
************************
Umri wo wote atakaopewa mtu kuishi ulimwenguni hapa, urefuke utakavyorefuka hata ukapindukia miaka alfu, bado utakuwa ni mfupi. Ufupi huu unatokana na ukweli kuwa mauti/kifo ndio mwisho wa kila kilicho hai, katika ulimwengu huu. Allah amrehemu mshairi aliyenena: (Ikiwa kufa ndio mwisho wa umri basi ni sawasawa ufupi na urefu wa umri).
Siku mauti yatakapo muhudhuria mtu, miaka aliyoishi itajikunja na kuonekana k**a ni vipindi vifupi vilivyopita k**a umeta wa radi. Imepokelewa hekaya kwamba malaika wa mauti- Allah amshushie Amani – alipomjia Nabii Nuhu – Amani imshukie – ili amfishe baada ya kuishi zaidi ya miaka alfu moja. Alimuuliza akisema: Ewe mrefu wa umri kuliko Mitume wote, umeionaje dunia? Akajibu (Nuhu): Mithili ya nyumba yenye milango miwili, nimeingia (nyumbani humo) kupitia mmojawapo wa milango na kutoka kupitia mlango mwingine..

11/07/2025

Dua ni silaha ya Mu’min #1

Kulikuwa na mfanya biashara mmoja alidai ardhi ambayo haikuwa ya kwake. Japokuwa mwenye ardhi hakiki alikuwa na vibali kamili lakini hakuweza kumshinda tajiri yule. Hila aliyokuwa nayo myonge huyo ni kupeleka mashtaka mahak**ani. Mfanya biashara huyo alitumia ujanja na kutengeneza vibali ambavyo hata mahak**ani vilionekana k**a ni vya kweli. Huko mahak**ani hakimu alidai kila upande ulete mashahidi. Yule tajiri kwa uwezo wa mali yake aliweza kuwapanga mashahidi wawili na kuwaleta mbele ya hakimu. Upande wa myonge yule hakukuwa na ushahidi ila Allah SWT. Hakimu aliamua kuwa ardhi ile apewe tajiri kufuatia vibali na ushahidi aliotoa. Baada ya kutoka mahak**ani, kilamtu alishika njia yake. Tajiri alionekana ni mwenye furaha na kwa mbali, aliwapungia mkono na kuonyesha ishara ya kidole gumba juu kwa wale mashahidi wake, na kuasharia kuwa atawalipa zawadi. Kwa furaha ile, Yule mnyone akiona harakati zile aliinua mikono juu na kuomba dua ya kuwa watu hao waisifanikiwe tena hapa duniani. Huku akivuka barabara kwa furaha ya ushindi wa kesi ile, tajiri huyo alikumbwa na dharba ya gari lililo mgonga na kumrusha juu. Kisha alianguka na kupigiza kichwa na kufa papo hapo. Wale mashahidi kuona tukio lile bila kuchelewa, wakijua hiyo dharba ni kwa sababu ya tazwiir na uongo wa tajiri yule. Walikimbia na kurejea mahak**ani. Huku wakitweta kwa khofu, walimwambia hakimu kwamba” Samahani, sisi tumerejea kusema ukweli, kwani sis ni mashahidi wa kupangwa kwa ajili ya maslaha. Hakika aridhi ile na yule bwana. Na yule tajiri amemdhulumu bwana yule”. Hakimu akasema, “ hivi sasa ndio mnasema ukweli na ilikuwaje hata mkageuza nia yenu?” Mashahidi wale wakajibu, “Tajiri yule kagongwa na gari na amekufa pale pale. Na hakuna sababu ila ni kwa ajili ya dhulma”. Hakimu akwaambia basi nendeni na nitatuma upelelezi na nitakuiteni. Walipotoka mahak**ani, nao katika kuvuka bara bara, waligongwa na gari vile vile k**a yule tajiri na kufa papo hapo.
Ndugu zangu!!
Hutokezea hakimu akawa na subra ya kutafuta uchunguzi zaidi au kufuata uzito wa ushahidi au kufuata umaarufu wa mtu anaeshtakiwa au anaeshaki. Kwa vyo vyote itavyo kuwa dhulma haimfikishi mtu mbali. Na mara nyingi malipo huanzia hapa hapa duniani. Kamwe na tena kamwe usichukue kitu ambacho si cha kwako na usitowe ushahidi wa uongo kwa ajili ya maslaha au kwa ajili ya kumuogopa au kumheshimu mtu.
Kumbukeni kwamba uwongo mara mbili au tatu haufanyi ukweli mmoja. Kunapokuwa na uongo Ukweli Hujitenga.

Sunan Abi Dawud : Hadith 3592
Ilinukuriwa na Khuraym Ibn Fatik RAA:
Mtume SAW alisali sala ya alfajiri. Alipomaliza, alisimama na kusema kwa kurudishia mara tatu, “ushahidi wa uongo (kutunga) umelinganishwa sawa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu” Kisha akasoma: Epukaneni kuabudu masanamu, na epukaneni na ushahidi wa uongo (kutunga) muwe k**a watu wale wenye imani na Mwenyezi Mungu, na msimshirikishe na kitu chechote.

Sahih Bukhari Hadith 839
Ilinukuriwa na Ibn Mas'ud RAA:
Mtume SAW aliseam, Yeyote atae kula kiapo kwa sababu kunyang’anya mali za wenzake, basi atakutana na Mwenyezi Mungu hali ya kuwa Amem’ghadhabia.

...

22/06/2025

KHASARA YA MILELE
Maiti ya mama mmoja ilikuwa ikitayarishwa kwa ajili ya mazishi. Na watu walikusanyika katika matanga yale wakiwepo wanae wa kiume mfa yule isipokuwa mmoja tu. Lakini kwa bahati yake aliwahi kufika pale. Kijana huyo alimuomba Sheikh amfunue ili amuone mama yake jicho la mwisho. Sheikh alimruhusu na yule kijana aliomba watu wasogee kando ili aweze kumuona peke yake. Alimfunua usoni lakini kwa haraka alimfunika na kuirudisha sanda k**a ilivyo kuwa. Kijana yule alihuzunika sana na kutokwa na machozi kwa wingi. Alimwita Sheikh yule pembeni na kumwambia, mbona huyu si mama yangu, si sura ile ninayo ijua mimi. Kwani imegeuka weusi wa ajabu. Nimepata khofu kumuona mama yangu hala hiyo. Sheikh akasema kwani mama yenu alikuwa namambo gani katika uhai wake? Yule kijana alibaki kimya na machozi kutiririka. Ndugu zake walimshika na kumnasih. Huko makaburini, maiti ilishushwa ili itiwe ndani ya mwanandani. Kwa ajabu kubwa kila maiti ikigeuzwa qibla iligeuka upande wa pili. Sheikh alijaribu mara kadha, lakini mambo yalikuwa ni vile vile. Hata mwishoni maiti iligeuka ikawa haiwezekani kuenea ktk mwanandani kwani viugo viliinuka. Sheikh yule aliamua kuomba dua kwa kipindi hadi akamuaa kumzika hali ya kuwa si Qibla. Sheikha aliwauliza ndugu wote amal gani alikuwa nayo mama yao, lakini kila mtu alibaki kimya bila kutamka kitu.
Baada ya muda kupita yule kijana aliekuwa akilia, aliamua kumfanyia mama yake Sadaqat Al-jariya ili iweze kumuokoa. Aina kwa aina ya sadaqa alimtolea mama yake, lakini hakupata dalili k**a sadaqa zinamfikia.
Muda mrefu ulipita baada ya kijana huyo kukosa mafanikio aliyo yatraji, na kuamua kumtafuta yule Sheikh alie simamima mazishi. Kwa bahati alionana nae. Akamkumbusha, “Ya Sheikh unakumbuka mazishi kasha wa kadha na tukio kadha wa kadha?” Yuel sheikh akajibu,”Naam nakumbuka vizuri kabisa, ehe nini hoja yako?” Yule kijana akasema, “mimi nimejaribu kumfanyia mama yangu sadaqa mbali mbali lakini sijaona dalili k**a zinamsaidi kitu!” Sheikh akamuuliza, “mimi nilikuulizeni siku ile ya mazishi nini ilikuwa amal ya mama yenu lakini hamkujibu?” Kijana yule akasema tulikuwa tunajaribu kumsitiri mama yetu” “Kumsitiri nini ?” Sheikh aliuliza. Kijana akasema, huku machozi yakimlenga kwamba, “mama yetu kamwe hakuwahi kuelekea qibla na kusali katika maisha yake yote!!!” Jibu hilo lilimshutusha Sheikh. Nae akasema,” Kwa nini basi msingalisema tangu mwanzo mkaacha tumesumbuka bure? Sisi wala tusingalimsalia wala kuMzika katika makaburi yetu bali tungalimzika katika makaburi ya makafiri!!

AlahmduliLlah bi Ni’mat Al-Islam
Allahuma Ij’alna mina Salihiin, Qaimin, Rakiin, Sajidiin, Saimin. Amiin
Mtume SAAW anasema Tofauti ya Muislamu Na Kafir ni Salaa.
Ndugu zangu Ni wajibu wetu kukumbushana Salaa. Ikiwa unamjua mtu hana salaa, basi mpe Da’wa na muulize swali lifuatalo:
“Utamshawishi vipi mtu asie Sali aanze kusali?” Na asIe Sali msikitini aanze kusali msikitini?

20/06/2025

📚 Learn Arabic Online! 🌍
✅ 6-Month Program
✅ From Beginner to Confident Speaker
✅ Flexible Online Classes
✅ Native Arabic Teachers

💬 Contact us on WhatsApp
📞 +20 110 447 2103

01/05/2025

Leo ulimwengu mzima unateseka na kupitia katika majanga makubwa, umekumbwa na maradhi mabaya yanayo ambukiza kwa kasi kubwa na kuua kwa halaiki. Familia nyingi leo, watoto wameachwa yatima, wanawake wameachwa wajane, wazazi wanateseka kwa kukosa wa kuwalea.

Yote hayo yanaukumba ulimwengu kutokana na wanaadamu kuutupa muongozo wa Mola Muumba wao na badala yake wakaishi k**a watakavyo wao na si k**a walivyo pangiwa na Allah. Kumkaidi Allah ni kujitafutia maangamivu, kwani Yeye hakatazi ila hicho alicho kikataza huwa na madhara na wala haamrishi ila kile kilicho na manufaa kwa waja wake.

Kwani ni Yeye ndiye aliye waumba na anawajua fika; lipi linawadhuru na lipi lina faida kwao. Tuacheni zinaa, kwani ndio sababu kubwa ya mengi miongoni mwa maradhi makubwa na mabaya yanayo utesa ulimwengu hivi leo na badala yake tukidhi haja zetu za kimaumbile kwa kupitia mlango wa ndoa tulio funguliwa na Mola wetu.

Haya na tusome kwa nia ya utekelezaji: “WALA MSIKARIBIE UZINZI. HAKIKA HUO NI UCHAFU NA NJIA MBAYA”. Al-Israa [17:32]

27/03/2025

Mwalimu bora kutoka azhary university, Karibu tujifunze Quran and Arabic kwa Mda wa miezi sita tu au wasiliana nami Kupitia WhatsApp +20110 447 2103

Want your school to be the top-listed School/college in Cairo?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Cairo