Salamu wafuasi wangu wapya! Nina furaha kuwa nanyi! Mercure Dieu Merci, Zai Mukanusoni
Nasry Zain Stories
@nasryzain
18/07/2025
😂😂😂😂
18/07/2025
Mtu mmoja alichinja ng’ombe mkubwa aliyenona, akawasha jiko la kuchomea nyama, akamwambia binti yake:
“Enenda ukawataarifu ndugu, jamaa, marafiki na majirani zetu waje tufanye sherehe!”
Lakini badala ya kutoa mialiko ya sherehe, binti yake alikimbilia barabarani akapiga kelele:
“Tusaidieni! Nyumba ya baba yangu inateketea kwa moto!”
Baada ya muda mfupi, ni watu wachache tu waliojitokeza. Wengine walijifanya hawajasikia chochote.
Wale wachache waliofika walikula na kunywa mpaka usiku wa manane.
Baba akiwa na mshangao, akamuuliza binti yake:
“Wako wapi ndugu na jamaa zetu, marafiki na majirani?”
Binti akamwangalia baba yake na kumwambia:
“Waliokuja walikuja kutuokoa(kwasababu nilipiga kelele kwamba nyumba yetu inaungua), si kwa sababu ya sherehe. Hawa ndio watu wanaostahili kukaa mezani nasi.”
Funzo:
K**a hawajitokezi wakati wa shida zako, hawastahili kuwa nawe wakati wa shangwe yako.
03/01/2025
Nikiungo gani katika mwili wako kimetumika sana mwaka 2024?
Mimi ni akili maana nilitafakari saana
😀😀😀
31/12/2024
Sijui nisemeje ila mama zetu na ma wetu
10/10/2024
Amitabh Bachchan (mwigizaji gwiji nchini India) aliwahi kusema:
"Katika kilele cha kazi yangu, wakati fulani nilikuwa nikisafiri kwa ndege. Abiria mmoja karibu yangu alikuwa bwana mzee aliyevaa shati ya kawaida sana na suruali. Alionekana kuwa mtu wa kawaida na mwenye kipato cha kawaida sana na msomi flani hivi.
Abiria wengine labda walinitambua mimi ni nani, lakini bwana huyu alionekana kutojali uwepo wangu....Alikuwa akisoma karatasi yake, akichungulia dirishani, na chai ilipotolewa, aliinywa kimya kimya.
"Nilipojaribu kuanzisha mazungumzo naye nilitabasamu. Mzee huyo naye alitabasamu kwa heshima na kusema 'Habari?'
"Tulizungumza na nikaleta mada ya sinema na kuuliza, 'Je, unatazama filamu?'
"Mzee huyo alijibu, 'Oh, mara chache sana. Niliona moja miaka mingi iliyopita.'
"Nikamwaambia kwamba ninafanya kazi katika tasnia ya sinema.
"Mzee yule akajibu .." oh, hiyo ni nzuri. Unafanya nini?'
"Nilijibu, 'Mimi ni mwigizaji'
"Mzee huyo akaongeza, 'Ah, hiyo ni nzuri!'
"Tulipotua, nilinyoosha mkono wangu na kusema," nimefurahi kusafiri pamoja nawe. Jina langu ni Amitabh Bachchan!'
"Mzee huyo alinishika mkono na kutabasamu, "Asante... nimefurahi kukutana nawe..Mimi ni J R D Tata (Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni iitwayo TATA)!"
"Nilijifunza siku hiyo kwamba hata ujifikirie kuwa mkubwa kiasi gani, siku zote kuna mtu mkubwa zaidi.
Kuwa mnyenyekevu, haigharimu chochote"
~ Kutoka peruzi mitandaoni.
Imetafsiriwa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili na Karume J. Asangama.
Nasry Zain Stories
05/10/2024
Rest in peace dada yetu shaibu
04/10/2024
DUBAI NIMEENDA MARA NYINGI
KULIKO MOROGORO - BILLNASS
Kutoka kwa msanii Billnass amefunguka ujumbe huu wa hamasa kwa vijana wenzake akiwa na Mama yake huko Ulaya.
"Nikikumbuka niliwahi Kuwa na Ndoto ya Kwenda Africa Kusini...Hata kwa kuiba na Nikawasimulia rafiki zangu kua nitaenda South Africa...wakanicheka sana na kuniambia unadhani South Africa ni Majani Mapana au Kisosora!! Lakini Sikukata tamaa nilibahatika kwenda South nikiwa Bado Nasoma na nikaenda tena na tena na Nikaenda Dubai Mara ya Kwanza nikiwa Chuoni... Imefika Hatua South na Dubai nimeenda Mara Nyingi kuliko Mara nilizoenda Morogoro...Na Nimeweza Kwenda Mataifa Mengine Makubwa Mengi sio kufanya Show wala Kutafuta Maisha Bali Kutembea tu... pia nimeweza Kusafiri na Watu ni wapendao Karibu Kila Mwaka Mke Wangu na Mtoto Wangu...Na Nilitamani Sana kusafiri na Wazazi Wangu lakini maokoto yalikuwa Hayajakaa... Mungu ni Mwema Birthday ya Mama Mwaka Huu atasherekea Europe na Mungu ampe Maisha Marefu Next time Aje na Baba na Wajukuu zake...!! Lengo la Maneno Yote Haya ni Kukutia Moyo kijana Mwenzangu wa Mtaani...Usikate tamaa.... Yote yanawezekana ipo Siku utawapa Furaha unaowapenda na Utafurahia Maisha k**a Unavyotamani...Kwa Mungu Hakuna Kinachoshindikana."
Nasry Zain Stories
03/10/2024
Mnamo mwaka 2009 Kijana wa Urusi mwenye umri wa miaka 28 Sergey Tuganov alishinda shindano la kufanya mapenzi na Wanawake wawili kwa muda wa saa 12 mfululizo.
Muda mfupi baada ya kushinda alifariki, uchunguzi ulifanyika ikagundulika kabla ya shindano hilo alimeza chupa nzima ya Vidonge vya kuongeza nguvu za kiume (Vi**ra) na ndicho kilipelekea kifo chake
Nasry Zain Stories
03/10/2024
Rapa Nicki Minaj amefunguka kuwa mali zake zote zimesajiliwa kwa jina la Kenneth Petty ambaye ni Mume wake tangu mwaka 2019.
Nicki Minaj anasema amefanya hivyo kwa sababu anamuamini sana, yeye siyo Mwanamke anayependa kushindana na Mwanaume ndani ya ndoa bali anamuheshimu sana Mume wake ingawa anajua amemzidi pesa lakini heshima yake ipo pale pale na amemuachia aongoze kila kitu.
Kenneth Petty anakadiriwa kuwa na utajiri wa $500K, huku Nicki Minaj akiwa na utajiri wa $150M.
Vipi kwa upande wako unaweza kubali mali zako zote zisajiliwe kwa jina la Mume/Mke wako?
Nasry Zain Stories
03/10/2024
03/10/2024
Du7uuuh 🤣🤣🤣🤣
Click here to claim your Sponsored Listing.