IQRAA islamic

IQRAA islamic

Comments

Asalam aleykum

" Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba " (96.1 Qur an )

Operating as usual

[07/28/15]   HADITHI YA. 28

NAKUUSIENI KUMCHA ALLAAH NA TABIA NJEMA

Kutoka kwa Abu Najiih Al 'Irbaadh Ibn Saariyah رضي الله عنه ambaye alisema kwamba:

Mtume صلى الله عليه وسلم alituhutubia hutuba ambayo nyoyo zetu zilijaa hofu na macho yetu yalitutoka machozi. Tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu!, inaonyesha k**a kwamba hii ni hutuba ya kuaga, kwa hivyo tuusie. Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم ) nakuusieni kumcha Allaah سبحانه وتعالى na kumtii kiongozi wenu hata akiwa mtumwa. Yule atakayeishi (muda mrefu) ataona ikhtilaaf nyingi (migongano), kwa hivyo fuateni mwendo wangu (Sunnah) na mwendo wa Makhalifa walioongoka (Makhalifa wanne). Shik**aneni nazo kwa magego (kwa nguvu). Na tahadharini na mambo mapya yanayozuliwa kwani kila jambo jipya ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu, na kila upotofu unapeleka motoni.

27/07/2015

QUR AN TUKUFU { 22.1.2} Inasema...

" Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Saa (ya Kiyama) ni jambo kuu."
" Siku mtapo iona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshaye, na kila mwenye mimba ataharibu mimba yake. Na utaona watu wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali. "

25/07/2015

HAKIKA QUR AN HAIKUACHA KITU ANGALIA JINSI ALLAH (S.W)
ANAVYOWEKA USAWA KWA VIUMBE

" Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari. "(Qur an 49.13)

25/07/2015

10. Enyi mlio amini! Nikuonyesheni biashara itakayo kuokoeni na adhabu iliyo chungu?
11. Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua. { Qur an 61.1011}

24/07/2015

Qur an { 2.225}
Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.

[07/23/15]   HADITHI YA 27

UADILIFU NI TABIA NZURIKutoka kwa An-Nawwaas Ibn Sam'aan رضي الله عنه ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:

Uadilifu ni tabia nzuri na udhalimu ni kile kitu ambacho huyumbayumba (chenye mashaka) katika nafsi yako na hupendelei watu kukitambua.

Imesimuliwa na Muslim

Na kutoka kwa Waabisah Ibn Ma'abad رضي الله عنه ambaye alisema:

Nilikuja kwa Mtume صلى الله عليه وسلم naye akasema:

Umekuja kuuliza juu uadilifu? Nikasema: Ndio . Akasema: Ushaurishe moyo wako. Uadilifu ni kile ambacho nafsi yako inakihisi shwari na moyo wako pia unahisi shwari, na udhalimu ni kile kinachoyumbayumba katika nafsi na kwenda na kurudi kifuani ijapokuwa watu wamekupa shauri lao la kisheria (kukipendelea).

23/07/2015

" Na soma uliyo funuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hapana wa kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio isipo kuwa kwake." Qur an tukufu, surah al kahf (18.27)

[07/23/15]   HADITHI YA 26

KILA KIUNGO CHA MTU LAZIMA KITOLEWE SADAKAKutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye alisema : Mtume صلى الله عليه وسلم kasema :

Kila kiungo cha mtu lazima kitolewe sadaka kila siku jua inapochomoza, kufanya haki (uadilifu) baina ya watu wawili ni sadaka, kumsaidia mtu kupanda (mnyama) kwa kumsaidia kumnyanyua au kumnyanyulia mizigo yake ni sadaka, neno jema ni sadaka, kila hatua unayokwenda kuswali ni sadaka, kuondosha dhara katika njia ni sadaka.

Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim

[07/22/15]   HADITHI YA 25

WENYE MALI WAMEONDOKA NA FUNGU (JAZA) KUBWAKutoka kwa Abu Dharr رضي الله عنه ambaye amesema:

Baadhi ya Maswahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم walimuambia Mtume صلى الله عليه وسلم : Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, wenye mali wameondoka na fungu (jaza) kubwa, wanaswali k**a sisi, wanafunga k**a sisi, na wanatoa sadaka ya ziyada ya mali zao. Mtume صلى الله عليه وسلم akasema: Mwenyeezi Mungu hajakufanyieni vitu kwa ajili yenu kutoa sadaka? (Basi jueni) Hakika kila Tasbihi (Subhana Allah) ni sadaka, kila Takbiri (Allahu Akbar) ni sadaka, kila Tahmidi (AlhamduliLlah) ni sadaka, na kila Tahlili (Laa ilaaha illa Allaah) ni sadaka, na kulingania jambo jema ni sadaka, na kukataza mabaya ni sadaka na katika kujamii (wake zenu) kila mmoja katika nyinyi ni sadaka. Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume صلى الله عليه وسل mtu anapojitosheleza shahawa yake atapata malipo kwa ajili yake? Akasema صلى الله عليه وسلم : Mnadhani ingekuwa anajitosheleza kwa njia ya haramu angelipata dhambi? Na hivyo ikiwa kafanya kwa njia ya halali basi atapata thawabu.

[07/21/15]   HADITHI YA 24

ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMAKutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifariy رضي الله عنه naye kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم akisimulia yale aliyopokea kutoka kwa Bwana wake عَزَّ وَجَلَّ ni:

Enyi waja Wangu, Nimeikataza nafsi Yangu dhulma na Nimeiharamisha kwenu (hiyo dhulma), kwa hivyo msidhulumiane.

Enyi waja Wangu, nyote mumepotea isipokuwa wale Niliowaongoza, kwa hivyo tafuteni muongozo kutoka Kwangu Nitakuongozeni.

Enyi waja Wangu nyote mna njaa isipokuwa wale Niliowalisha, kwa hivyo tafuteni chakula kutoka Kwangu na Nitakulisheni.

Enyi waja Wangu, nyote muko uchi isipokuwa wale niliowavika nguo, kwa hivyo tafuteni vazi kutoka Kwangu nitakuvisheni.

Enyi waja Wangu, mnafanya makosa usiku na mchana, na ninasamehe dhambi zote, kwa hivyo tafuteni msamaha kutoka Kwangu nitakusameheni.

Enyi waja Wangu hamuwezi kunidhuru Mimi wala kuninufaisha.

Enyi waja Wangu, ingekuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mcha Mungu k**a moyo wa mcha Mungu yeyote katika nyinyi, haitaongeza chochote katika ufalme Wangu.

Enyi waja Wangu, angelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mbaya k**a moyo mbaya wa mtu miongoni mwenu (mtu mbaya kupita kiasi) haitonipunguzia chochote katika ufalme Wangu.

Enyi waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi mukasimama pahala pamoja na mkaniomba, na nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovya.

Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu ninavyovihesabu, kwa ajili yenu nikakulipeni. Kwa hivyo anayekuta wema amshukuru Allaah na yule anayekuta yasiokuwa mema (basi) ajilaumu mwenyewe.

Imesimuliwa na Muslim

[07/21/15]   " Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema?" ( qur an 63.10)

21/07/2015

JIFUNZE JINSI YA KUJIFUNGA KILEMBA kiOmani' Masarh

19/07/2015

OTHMAN MAALIM_WASIA WA LUQMAAN KWA MWANAWE

18/07/2015

NGUGU MUISLAM, HAKIKA UISLAMU UMESHAWEKA WAZI TARATIBU ZA KUSHEHEREKEA SIKU YA EID, EPUKA KUHARIBU IBADA ZAKO ZA MWEZI MZIMA KWA SIKU MOJA TU YA EID, " MWENYE KUMUASI MUNGU SIKU YA EID NI SAWA AMEMUASI MUNGU SIKU YA QIYAMA" MUNGU ATUWEZESHE INSHAALLAH

[07/18/15]   HADITHI YA 22

JE, NIKISWALI SWALAH ZA FARDHI, NIKAFUNGA RAMADHAAN…Inatoka kwa Abu 'Abdillaah Jaabir bin 'Abdillaah Al-Answaariy رضي الله عنه alisema:

Mtu alimuuliza Mtume ,صلى الله عليه وسلم Unafikiri nikiswali Swalah za fardhi, nikafunga Ramadhaan, nikafanya halali kilicho halali na nikaharimisha kile kilichoharimishwa, na nisifanye jambo lolote lingine, je? Nitaingia peponi? Mtume صلى الله عليه وسلم akamjibu: Ndio.

Imesimuliwa na Muslim

[07/18/15]   HADITHI YA 21

SEMA NAMUAMINI ALLAH KISHA KUWA MWENYE MSIMAMO

Kutoka kwa Abu 'Amr, vile vile (anajulikana k**a) Abu 'Amra Sufyaan Ibn Abdillah رضي الله عنه ambaye amesema:

Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, niambie kitu kuhusu Uislamu ambacho siwezi kumuuliza mtu yeyote ila wewe. Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم ) : Sema; Namuamini Allaah , kisha kuwa mwenye kunyooka. (kwa kuendelea kufanya ibada na kuwa na msimamo madhubuti katika dini)

Imesimuliwa na Muslim.

17/07/2015

"HAPPY EID FITRY" IQRAA islamic inawatakia happy ya eid na ramadhan yenye kukubaliwa na ALLAH (Subhanah wataallah),tulikuwa na nyinyi katika kipindi cha mfungo wa mwenzi mtukufu wa ramadhan mungu atuwezeshe kuwa na nyinyi miezi iliyobakia inshaallah, Ahsante kuchagua IQRAA islamic and IQRAA islamic international pages

https://facebook.com/iqraaislamic

[07/15/15]   HADITHI YA 20

IKIWA HUNA HAYA BASI FANYA UTAKAVYO

Kutoka kwa Abu Mas'ud ‘Uqbah Ibn 'Amr Al Ansariy Al Badriy رضي الله عنه ambaye amesema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: “Katika maneno ambayo watu waliyapata kutoka kwa Mitume wa mwanzo (waliotangulia) ni haya: “Ikiwa huna haya basi fanya utakalo.”

Imesimuliwa na Al-Bukhari

15/07/2015

ZAKAAH FITR NI ZAKAAH INAYOTELEWA KUANZIA MWEZI 29 HADI KUSALIWA KWA SALA YA EID KATIKA MWENZI MTUKUFU RAMADHAN, ZAKAAH HII NI FARADHI KWA KILA MUISLAMU KWANI FUNGA HAIPANDISHWI KWA ALLAH HADI MUISLAM ATOE ZAKAAH HII NA KUWATOLEA WALE WALIO CHINI YAKE ( FAMILIA YAKE) SHIME WAISLAMU KUCHANGAMKIA FADHLA HIZI IKWA LEO TUMESHAINGIA MWEZI 29 RAMADHAN

15/07/2015

USISAHAU MAUTI HAKIKA MAUTI HAYAKUSAHAU

14/07/2015

" Na soma uliyo funuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hapana wa kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio isipo kuwa kwake." Qur an tukufu, surah al kahf (18.27)

[07/14/15]   HADITHI YA 19

MUHIFADHI ALLAAH سبحانه وتعالى ATAKUHIFADHI

Kutoka kwa Abul ‘Abbaas Abdullah Ibn ‘Abbaas رضي الله عنهما ambaye alisema:

Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume صلى الله عليه وسلم akaniambia: Kijana nitakufundisha maneno (ya kufaa); Mhifadhi Allaah سبحانه وتعالى (fuata maamrisho Yake na chunga Mipaka Yake) Atakuhifadhi. Muhifadhi Allaah سبحانه وتعالى na utamkuta mbele yako. Ukiomba, muombe Allaah سبحانه وتعالى, ukitafuta msaada tafuta kwa Allaah سبحانه وتعالى. (lazima) ujue kuwa ikiwa taifa zima litaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile alichokwishakuandikia Allaah سبحانه وتعالى na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hotodhurika ila tu kwa kile Allaah سبحانه وتعالى alichokwishakuandikia (kuwa kitakudhuru) . Kwani Kalamu zimeshanyanyuliwa (kila kitu kishaandikwa) na sahifa zimeshakauka (Hakuna kupangwa tena wala kupanguliwa).

Imesimuliwa na At-Tirmidhi akasema kuwa ni hadithi Hasan Sahihi.

Na kwa mapokezi mengine yasiyokuwa ya At-Tirmidhi inasema:

Muhifadhi Allaah سبحانه وتعالى utakuta katangulia mbele yako (kwa ulinzi Wake, himaya na msaada Wake). Mjue Mola wako katika neema (muombe, mche, mtii) Atakujua katika shida (unapokuwa katika dhiki Naye Atakusaidia). Jua kuwa yaliyokukosa hayakuwa yakupate na yaliokupata hayakuwa yakukose. Jua kuwa ushindi uko pamoja na subira, na faraja iko pamoja na dhiki, na raha iko pamoja na shida (haviachani).

[07/13/15]   HADITHI YA 18

MCHE MWENYEEZI MUNGU POPOTE ULIPO

Kutoka kwa Abu Dharr Jundub Ibn Junaada na Abu Abdur Rahmaan

Mu'adh Ibn Jabal رضي الله عنهما ambao wamemnukuu Mtume صلى الله عليه وسلم akisema:

“Mche Allaah سبحانه وتعالى popote pale ulipo na fuatisha kitendo kibaya kwa kitendo kizuri kitafuta (kitendo kibaya) na ishi na watu kwa uzuri.”

Imesimuliwa na At-Tirmidhi na kasema kuwa ni hadithi Hasan na katika maandiko mengine imesemwa kuwa ni Hasan Sahihi

[07/12/15]   HADITHI YA 17

MOLA KAANDIKA UZURI (WEMA) KATIKA KILA KITU

Kutoka kwa Abu Ya’ala Shaddad Ibn Aws رضي الله عنه ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:

Mola kaamrisha wema katika kila kitu. Kwa hiyo unapoua (mnyama), ua vizuri na unapochinja chinja vizuri. Basi kila mmoja wenu anoe kisu chake barabara (anapotaka kuchinja) na amuondoshee machungu (asimtese) yule mnyama anayemchinja.

Imesimuliwa na Muslim

[07/11/15]   HADITHI YA16

USIHAMAKI

Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye amesema:

Mtu alimwambia Mtume صلى الله عليه وسلم Niusie: “akamwambia “usihamaki, yule mtu akakariri tena (ombi lake) mara nyingi, na akamwambia (jizuie) usihamaki.”

Imesimuliwa na Al-Bukhari

[07/09/15]   HADITHI YA 15

ALIYEKUWA AMEMUAMINI ALLAAH سبحانه وتعالى NA SIKU YA QIYAAMAH

ASEME YA KHERI

Kutoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye alisema: Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم :

Aliyekuwa amemuamini Allaah سبحانه وتعالى na siku ya Qiyaamah aseme (mambo ya) kheri, au anyamaze, na yule anaemuamini Allaah سبحانه وتعالى na siku ya Qiyaamah awe Mkarimu kwa jirani yake, na yule anaemuamini Allaah سبحانه وتعالى na siku ya Qiyaamah amkirimu mgeni wake.

Imesimuliwa na: Al-Bukhaariy na Muslim

09/07/2015

Photos from IQRAA islamic's post

[07/09/15]   HADITHI YA 14

DAMU YA MUISLAMU ISIMWAGWE ISIPOKUWA KWA SABABU TATU

Kutoka kwa Ibn Mas'udرضي الله عنه ambae alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema :

Damu ya Muislamu haiwezi kwa haki kumwagwa isipokuwa katika hali tatu: Mzinzi Muolewa (Mtu mzima aliyeoa/olewa), uhai kwa uhai (nafsi kwa nafsi) na kwa yule anaewacha dini na akajifarikisha na jamaa (kundi) (amejitenga na watu wa dini yake).

Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim

[07/08/15]   HADITHI YA 13

HATOAMINI MMOJAWENU…

Kutoka kwa Abu Hamza Anas Ibn Malik رضي الله عنه mtumishi wa Mtume صلى الله عليه وسلم alisema kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:

Haamini mmoja wenu (kikwelikweli) mpaka atakapompendelea ndugu yake kile anachojipendelea nafsi yake.

Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim

[07/07/15]   HADITHI YA12

MUISLAMU MZURI

Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye amesema: “Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم: Moja ya sifa nzuri za Muislamu ni kutoshughulika na yale yasiyomuhusu.”

Hadithi iliyo katika daraja ya Hasan (nzuri inayokubalika) Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na wengineo

05/07/2015

ANGALIA HII VIDEO KISHA MUOMBE ALLAH (SUBHANA WATAALAA) AWAEPUSHE NA TABU HIZI WAISLAMU WOTE DUNIANI

[07/05/15]   HADITHI YA 11

WACHA KILE KINACHOKUTIA SHAKA UFUATE KILE

KISICHOKUTIA SHAKAKutoka kwa Abu Muhammad Al-Hasan Ibn ‘Ali Ibn Abi Twaalib mjukuu wa Mtume صلى الله عليه وسلم na kipenzi chake رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا alisema :

Nilihifadhi kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم maneno haya: “Wacha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka”.

Imesimuliwa na At-Tirmidhi na An-Nasai, At-Tirmidhi akisema kuwa ni hadithi Hasan na Sahihi.

04/07/2015

NDUNGU MUISLAM TUUNGANE NA WAISLAMU WENZETU KULANI VITENDO WAVYOFANYIWA WAISLAMU DUNIANI. MUNGU AWAPE ADHABU HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA WANAOWAFANYIA VITENDO HIVI WAISLAMU

04/07/2015

Timeline Photos

[07/04/15]   HADITHI YA 9

NILICHOKUKATAZENI KIEPUKENI

Kutoka kwa Abu Hurayra Abdur Rahman Ibn Sakhr رضي الله عنه ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:

Kile nilichokukatazeni kiepukeni, Na kile nilichokuamrisheni fanyeni kwa wingi kadiri muwezavyo. Hakika kilichowaangamiza watu wa Umma zilizopita, ni masuala (mahojiano) mengi na kupingana na Mitume yao.

Videos (show all)

JIFUNZE JINSI YA KUJIFUNGA KILEMBA  kiOmani' Masarh
OTHMAN MAALIM_WASIA WA LUQMAAN KWA MWANAWE
USISAHAU MAUTI HAKIKA MAUTI HAYAKUSAHAU
ANGALIA HII VIDEO KISHA  MUOMBE ALLAH (SUBHANA WATAALAA)  AWAEPUSHE NA TABU HIZI WAISLAMU WOTE DUNIANI
BAADA YA KUFA
MIUJIZA YA NABII M***A NI ISHARA INAYOTHIBITISHA UWEPO NA UKUMBWA WA ALLAH S.W

Location

Category

Telephone

Address


Amani
Zanzibar
Other Education in Zanzibar (show all)
IQRAA Islamic International IQRAA Islamic International
Darajani
Zanzibar, 09777

" Read in the name of Lord who created " {Qur an 96.1}

Zanzibar Climate Change Alliance Zanzibar Climate Change Alliance
Mwanakwerekwe
Zanzibar

We are a non-profit organization fighting against the impacts of climate change.

American Corner Zanzibar American Corner Zanzibar
PO BOX/ SLP 4270
Zanzibar

American Corners is a service to provide the citizens of Zanzibar with information about the United States through book collections and Internet access.

Mr.fundi Mr.fundi
Mwera Mtofaani
Zanzibar

Hii ni page kwa ajili yako kwa kupata elimu, michezo na burudani bila kusahau kutangaza biashara yako.

Golden tree academic Golden tree academic
MTOFAANI KIGOROFANI-ZANZIBAR
Zanzibar

Welcome golden tree academic

Karume Institute Of Science And Technology Karume Institute Of Science And Technology
Karakana
Zanzibar, P.O. BOX 476

Karume Institute of Science and Technology (KIST), is a parastatal organisation under the Ministry of Education and Vocational Training.

Zanzibar adventure Zanzibar adventure
Nungwi Zanzibar, P.o Box 2591
Zanzibar

Zanzibar adventure is an organization deals with arrangement for accommodations, tours and transfers

Treasure Education Institute Treasure Education Institute
MASINGINI - ZANZIBAR
Zanzibar

we help orphans, homeless children and miserable children for free. We welcome any body who wants to volunteer in teaching them, helping material, supporting financial or else to save the children.

Flora primary school Flora primary school
Zanzibar, +255

Dhow Countries Music Academy (DCMA) Dhow Countries Music Academy (DCMA)
Old Customs House, Mizingani Rd
Zanzibar, 255

The school provides a unique opportunity for the inhabitants of Zanzibar and the Dhow Regions.

Acme nursery and primary school Acme nursery and primary school
Fuoni, Mtundani
Zanzibar

Acme Nursery and Primary school - ANPS Was established in 2015, a good progress and with increase in number of students between 10% 25% each year