Pangani FM 107.5

Pangani FM 107.5

Comments

Pamoja
JE UNAHITAJI DESIGN YA BANGO LA BIASHARA YAKO LEO? AINA GANI YA BANGO UNAHITAJI? JE NI POSTER YA MTANDAONI? JE NI BANGO KUBWA LA KUWAKA TAA USIKU? ( BACK- LIGHT) BANGO LA KAWAIDA? ( BROCK OUT SIGN- BOARD) WASILIANA NASI LEO BEI ZETU NI NAFUU!
Leo 25/12/2020 mpaka 10/12/2020 naungana na watu wengi duniani kote kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia.

Maadhimisho haya ni ya msingi kutukumbusha juu ya masaibu wanayopitia Wanawake na Watoto katika karibu kila pembe ya Ulimwengu.

Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inaanza na uzinduzi, tarehe 25 Novemba ambayo ni siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na kuhitimishwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu Desemba 10.
#InaanzaNaMimi

Mizizi ya ukatili inatajwa kuwa ni mfumo dume , ukimya , machafuko ya amani, tamaduni kandamizi, imani za kishirikina, ombwe la kiuongozi, kupuuzia kuchukua hatua nk.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema Tupinge Ukatili wa Kijinsia Mabadiliko Yanaanza na Mimi.

Ni vyema wote tukasafiria kauli hii kwa kutambua kuwa swala la kutokomeza ukatili wa kijinsia linatuhusu sisi sote, sisi binafsi tukimchukulia mwanamke k**a mama,mwenza , dada, mtoto, shangazi au bibi basi tutaguswa na masaibu wanayopitia kutokana na ukatili dhidi yao.

Katika kuadhimisha #16days2020 nitakuwa nasoma Chapter 2 kila siku toka kwenye kitabu SlutWalk: Feminism, Activism and Media. ungana nami kusikiliza, kutazama , kufuatilia mijadala juu ya ukatili au kusoma majarida, tafiti ama ripoti juu ya #GBV #VAC #IPV.

Naamini katika uelewa na wingi wa taarifa na maarifa wote kwa pamoja tutaweza kuishi kauli mbiu ya Mwaka huu na kushiriki kikamilifu kutengeneza mazingira mazuri kwa ustawi wa Jamii yetu, Taifa na Ulimwengu kwa ujumla.
GOD BLESS U
LEO HII KATIKA KIPINDI CHA MAKUTANO

.
Tutakuwa na Mahojiano na Afisa Uvuvi Wilaya ya Pangani Bwana ๐‡๐ฎ๐ฆ๐ฉ๐ก๐ซ๐ž๐ฒ ๐“๐ข๐ฅ๐ฒ๐š ambapo atakuwa Akitoa Taarifa Rasmi ya Ufunguzi wa Soko la Samaki siku ya tarehe 8 mwezi wa 6 katika Eneo la Pangani Mashariki.

โ–ถ๏ธ๐Œ๐š๐ก๐จ๐ฃ๐ข๐š๐ง๐จ ๐ก๐š๐ฒ๐จ ๐˜๐špo ๐‹๐ข๐ฏ๐ž ๐ฉ๐ข๐š ๐ค๐ฎ๐ฉ๐ข๐ญ๐ข๐š ๐ฎ๐ค๐ฎ๐ซ๐š๐ฌ๐š ๐ฐ๐ž๐ญ๐ฎ ๐ฐ๐š ๐…๐š๐œ๐ž๐›๐จ๐จ๐ค.
Pamoja sana kweny banja bit
Across pangani city,
Let's type our home Legend.

Tunakujaa!!
dah
K**a kawa wadau wa musibaz
Unaweza kufanya kitu ambacho kimtazamo kipo sawa, tena kwa lengo zur la kuelimisha, lkn kumbe hujui k**a unakosea,
Pamba neni wapendwa
Naombeni matokeo ya darasa la saba 2019 shule ya msingi mikocheni pangani tanga.

Pangani FM Radio ni redio ya jamii, na kazi yake kubwa ni kuipa sauti jamii kwenye kuibuia changamoto za kijamii na kimaendeleo na kuyatafutia utatuzi.

Radio hii ni sehemu ya shirika la UZIKWASA (LENYE KIREFU CHA UZIMA KWA SANAA ) la wilayani PANGANI

Operating as usual

Photos from Pangani FM 107.5's post 13/09/2021

PANGANI FM YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UMAHIRI WA HABARI TANZANIA 2020.
-
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Radio Pangani FM Rajabu Mustapha Mrope ameibuka mshindi wa kwanza Kitaifa wa tuzo za umahiri wa Habari Tanzania (EJAT) mwaka 2020 katika kipengele cha Habari za Data na Takwimu.
-
Makala iliyopelekea ushindi huo ilionyesha namna ambavyo wapiga kura walipungua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulinganisha na miaka mitano iliyopita.
-
Juma ya kazi 147 ziliwasilishwa kwa Baraza la Habari la Habari Tanzania ili kushindanishwa katika kinyangโ€™anyiro hicho.
-
Tuzo hizo zimetolewa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na waandishi wachache huku sehemu kubwa wakishiriki kupitia njia ya Mtandao k**a tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
-
Akizungumza mara baada ya kutajwa k**a mshindi katika tuzo hizo Bwana Rajabu Mrope amelishukuru Shirika la UZIKWASA kwa uwepo wake kwenye Safari Yake ya uandishiwa Habari pamoja na timu nzima ya waandishi wa kituo hiki katika kufanikisha ushindi wake.
-
Hii ni mara ya Pili mfululizo kwa Rajabu Mrope kuibuka mshindi katika tuzo hizo na mara ya sita mfululizo kwa Pangani FM kutoa mshindi katika Tuzo hizo kubwa Zaidi za Habari nchini Tanzania zinazoandaliwa na Baraza la Habari nchini (MCT).

31/08/2021

Endelea kunasa kupitia 107.5 Mhz

Endelea kunasa kupitia 107.5 Mhz

18/08/2021

AJINYONGA KISA WIVU WA MAPENZI
-
Kijana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Amury Mwin-dadi mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Kijiji cha Mikinguni Wilayani Pangani Mkoani Tanga amejinyonga hadi kufa.
-
Mrakibu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Pangani ASP ELIJAH MATIBU amethibitisha kisa hicho kwa kusema kuwa uchunguzi wa awali umebainisha kuwa kijana huyo ambaye ni Bobadoba amejinyonga kutokana na wivu wa mapenzi.

"Marehemu inaonekana alikuwa amemfuata mke wake nyumbani kwao ambaye alikuwa amerudi nadhani ni kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri yule mama hakukubali kurudi, akachukua maamuzi ya kujidhuru hapohapo bado tuanendelea kufanya utafiti lakini kwa awali tunaona ni wivu wa mapenzi, watu wasiwe na hasira ambazo zinapindukia.. nitoe wito kwa watu kuzuia hasira zao, kiaja mdogo k**a huyu ameacha mke na watoto"- Amesema ASP Matiku.
-
Mwili wa Kijana huyo tayari umezikwa hapo jana kijijini kwao MIKINGUNI.

sikiliza hapa https://radio.tadio.co.tz/pangani-fm/2021/08/18/ajinyonga-kisa-wivu-wa-mapenzi-pangani/

17/08/2021

JOTO KUONGEZEKA MARADUFU DUNIANI
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema zinahitajika nguvu za pamoja kutoka kwa viongozi wote wa serikali duniani na kwa haraka sana ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayoikabili dunia baada ya ripoti mpya ya wanasayansi kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC iliyotolewa leo kubainisha kuwa shughuli za binadamu zinapeleka dunia katika madhara ya tabianchi yasiyorekebishika.
-
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo mjini New York, Marekani kuhusu uchambuzi wa ripoti hiyo, Guterres amesema, ripoti imeonesha shughuli za kibinadamu zinazidi kuiathiri sayari dunia na joto limezidi kuongezeka ilihali kuna makubaliano yaliyofanyika Paris ya nchi zote kupunguza gesi ya ukaa.
-
Akizungumzia mkataba wa kimataifa wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi uliopitishwa mwaka 2015, Guterres amesema, โ€œkwa sasa tupo kwenye nyuzi joto 1.2 katika kipimo cha Selsiyasi na joto lingali likiongezeka kwa haraka huku viwango vya gesi chafu navyo vikiongezeka, hali mbaya ya hewa na majanga mengine pia yakiongezeka. Kizingiti tulichokubaliana kimataifa cha nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi kiko karibu sana kufikiwa na hii ni hatari na lazima tuchukue hatua sasa.โ€
-
Ripoti hii imeandaliwa na wanasayansi 234 kutoka nchi 66, ikimulika jinsi binadamu amesababisha ongezeko la joto duniani katika kiwango kisicho cha kawaida katika miaka 2,000 iliyopita.
Mwaka 2019, viwango vya hewa ya CO2 vilikuwa juu kuliko wakati wowote katika miaka angalau milioni 2 iliyopita na viwango vya hewa aina ya methane na Naitrate Oksaidi navyo vilikuwa vya juu kuliko miaka 800,000 iliyopita.

Viwango vya joto duniani vimeongezeka haraka tangu mwaka 1970 kuliko miaka 50 kwa angalau miaka 2,000 iliyopita. Mathalani kiwango cha joto katika muongo wa hivi karibuni zaidi 2011hadi 2020 kilivuka kile cha karne za hivi karibuni zaidi, takribani miaka 6,500 iliyopita.
-
Navyo vina vya maji baharini vimeongezeka kwa kasi kubwa tangu mwaka 1990, kuliko karne yoyote katika angalau miaka 3,000 iliyopita.Iwapo kiwango cha joto kitaendelea hivyo bila kudhibitiwa, itakuwa na madhara mabaya mno kwa binadamu, kwa ekoloji na kwa uchumi, na kusababisha uhaba wa chakula, majanga ya moto kuongezeka, kuongezaka kwa kina cha bahari na kusababisha hali mbaya mno ya hewa.

Fedha zilizopangwa kutolewa ili kusaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zimetolewa asilimia 21 pekee. Hivyo makampuni ya uwekezaji na mabenki yamehimizwa kuwekeza katika shughuli zinazolenga kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi angalau kwa asilimia 50 huku kipaumbele kikisisitizwa kutolewa kwa makundi yenye uhitaji zaidi ikiwemo wanawake na watoto.
-
Uzalishaji wa gesi ya ukaa usipopunguzwa kwa asilimia 7.6 kila mwaka kati ya 2020 na 2030, dunia haitaweza kufikia nyuzijoto 1.5 za kiwango cha joto zinazolengwa kufikiwa chini ya mkataba wa Paris.
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mapendekezo kadhaa ya kukabiliana na hali hii ambayo ni;- dunia kuhakikisha ina uchumi usioharibu mazingira na juhudi za makusudi kuhakikisha kuna hewa safi na nchi tajiri pamoja na mashirika makubwa ya kimataifa, kujiunga na umoja wa kutozalisha hewa ya kaboni.

Pia amesisitiza kundi la nchi 20 zenye uchumi wa juu, au G20 zinatimiza ahadi zao kwa kutoa michango na kuweka sera zinazokubalika kimataifa kabla ya mkutano wa kimataifa wa masuala ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa unatarajiwa kufanyika huko Glasgow, Scotland baadaye mwaka huu 2021.

04/08/2021

WALIOJITOKEZA KUPOKEA CHANJO YA CORONA PANGANI.
-
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga leo imeanza zoezi la utoaji wa Chanjo ya virusi vya Corona kwa makundi yaliyopewa kipaumbele ikiwemo watoa huduma za afya, watu wenye magonjwa sugu na wazee.
-

Viongozi wa Serikali, taasisi, watumishi wa afya na wananchi mbalimbali wamejitokeza katika zoezi hilo la uzinduzi wa utoaji chanjo za Virusi vya Corona kwa Wilaya ya Pangani.
-
Zoezi hilo limefanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani leo Jumatano Agosti 4 mwaka 2021.

Akizungumza na Pangani FM Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Dokta Maulid Majala amesema wamepokea Dozi 1000 za Chanjo ya Corona na amewasisitza Wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo kwani ni salama.
-

Ndani ya muda usiozidi saa 2, kuanzia saa 7 mpaka saa 9 mchana leo idadi ya watu 59 wamepokea chanjo hiyo kwa Wilaya ya Pangani.
-
Mwanahabari wetu Maajab Madiwa amefika katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani na kuzungumza na Viongozi mbalimbali waliojitokeza katika tukio hilo.

Sikiliza hapa taarifa hii.
https://radio.tadio.co.tz/pangani-fm/2021/08/04/pangani-yaanza-rasmi-kugawa-chanjo-ya-corona/

Waliojitokeza kupokea chanjo ya Corona Pangani. โ€“ Pangani FM 04/08/2021

Waliojitokeza kupokea chanjo ya Corona Pangani. โ€“ Pangani FM

Waliojitokeza kupokea chanjo ya Corona Pangani. โ€“ Pangani FM Pangani FMHABARI ZA PANGANIWaliojitokeza kupokea chanjo ya Corona Pangani. Waliojitokeza kupokea chanjo ya Corona Pangani. 4 August 2021, 5:37 PM Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga leo imeanza zoezi la utoaji wa Chanjo ya virusi vya Corona kwa makundi yaliyopewa kipaumbele ikiwemo watoa h...

Uelewa mdogo wa matumizi ya Barakoa Pangani. โ€“ Pangani FM 03/08/2021

Uelewa mdogo wa matumizi ya Barakoa Pangani. โ€“ Pangani FM

Uelewa mdogo wa matumizi ya Barakoa Pangani. โ€“ Pangani FM Pangani FMHABARI ZA PANGANIUelewa mdogo wa matumizi ya Barakoa Pangani. Uelewa mdogo wa matumizi ya Barakoa Pangani. 3 August 2021, 8:59 PM Wauzaji wa barakoa Wilayani Pangani Mkoani Tanga wameeleza namna wanavyowaelimisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya barakoa. Wakizungumza na Pangani FM kwa ny...

01/08/2021

Mahak**a ya wilaya ya Pangani Mkoani Tanga imemuhukumu mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina Seleman Salim Rajab mwenye umri wa miaka 26 kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la ubakaji.
-
Katika hati ya mashata iliyowasilishwa mahak**ani hapo ilidaiwa kuwa mnamo terehe 1 mwezi 10 mwaka 2020 majira ya mchana ndani ya wilaya hii ya Pangani mshatakiwa huyo alimbaka binti wa miaka 7.
-
Baada ya ushahidi wa pande zote mbili uliotolewa mahak**ani hapo,mahak**a ilijiridhisha na ndipo ilipomkuta na hatia mshtakiwa huyo hivyo kuhukumiwa kifungo hiko cha maisha gerezani.
-
Hukumu hiyo imetolewa wiki hii tarehe 27 na hakimu wa mahak**a ya wilaya Fransesca Magweza.

15/07/2021

SIKU YA UJUZI KWA VIJANA

Leo ni siku ya ujuzi kwa vijana duniani , Jamii Wilayani Pangani Mkoani Tanga imeshauriwa kuwekeza zaidi katika elimu ya ufundi stadi kwa vijana wao ili kuwawezesha kuwa na ujuzi utakao wapa fursa ya kuingia katika soko la ajira.
-
Hayo yamelezwa na Mhandisi wa maji RUWASA hapa Wilayani PANGANI ndugu RAJABU YAHYA.
Amesema kuwa RUWASA imekuwa ikitangaza nafasi za ajira kwa watendaji wa vijiji lakini hakuna muamko mkubwa miongoni mwa vijana wa Wilaya ya Pangani.

-
Mhandisi Rajabu amesema RUWASA-Pangani imekuwa na miradi ya maji inayohitaji mafundi na wataalamu wa fedha na matarajio yao ni kutoa ajira hizo kwa vijana wazawa, hivyo ametoa rai kwa viongozi kuwa mabalozi katika kuhakikisha vijana wanajiunga na elimu ya ufundi stadi.
-
Itakumbukwa kuwa tarehe 15 Aprili, 2021, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu ilitangaza fursa za mafunzo ambayo yatatolewa katika taasisi za mafunzo zilizotangazwa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara.
Na hadi sasa Ofisi ya Waziri Mkuu imearifu umma kuwa, vijana 14,440 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo katika vyuo 72 nchini.

Videos (show all)

Swala ya Eid al Fitr Pangani
Kontena la Ofisi ya Bandari KIpumbwi
Pangani FM STUDIO
Getrude Clement
Machi 17,2020 Shule za Awali, Msingi na Sekondari Nchini Tanzania zilifungwa k**a hatua ya Kupunguza mikusanyiko na maam...
PANGANI FM HABARI
Bongo Kitambo Mpaka saa 10 Jioni.
๐™ˆ๐™ฌ๐™–๐™ฃ๐™–๐™›๐™ช๐™ฃ๐™ฏ๐™ž ๐™จ๐™๐™ž๐™ ๐™– ๐™†๐™–๐™ก๐™–๐™ข๐™ช ๐™ฌ๐™–๐™จ๐™๐™– ๐™๐™–๐™™๐™ž๐™ค ๐˜ฟ๐™–๐™ง๐™–๐™จ๐™– ๐™‡๐™ž๐™š๐™ฃ๐™™๐™š๐™ก๐™š๐™š.Leo hii katika Kipindi Radio Darasa  kwenye somo la Kiswahili kwa K...
Wananchi wa kata ya Pangani Magharibi Wilayani Pangani Mkoani Tanga wamejikututa katika hali ya taharuki na kustaajabu b...

Location

Telephone

Address

Jamhuri Street
Pangani
B.O.X 1
Other Pangani schools & colleges (show all)
Bushiri Secondary School Bushiri Secondary School
P.O. Box 28
Pangani, +255

Fountain of knowledge