English-Swahili Translation and Information Technology Services

English-Swahili Translation and Information Technology Services

Comments

Incarnation.
John 1:14
VIORATE IN SWAHILI?
The Plural of Swahili Nouns by
George Mwidima Kihanda 04 June 2020.

1. Nouns that do not change its form in Plural.

Singular - Plural

Nyumba (house) - nyumba (houses)
Nyanya (tomato) - nyanya (tomatoes)
Rangi (colour) - Rangi (colour)
Sebule (living room) - sebule (living rooms)
Nguo (cloth) - nguo (clothes)
Barabara (road) - barabara (roads)
Meza (table) - meza (tables)
Kalamu (pen) - kalamu (pens)
Kabati (cupboard) - kabati (cupboards)
Karoti (carrot) - karoti (carronts)
Kabeji (cabbage) - kabeji (cabbages)
Sketi (skirt) - sketi (skirts)
Kaptula (a short) - kaptula (shorts)
Suruali (a trouser) - suruali (trousers)
Zana (tool) - zana (tools)
Nyumbani (at home) - nyumbani (at homes)

Nouns borrowed from another language are normally
placed in this noun class.
---------------------------------------------------------------

2. Nouns that change its form in plural by taking vi, vy

Chumba (room) - vyumba (rooms)
Choo (toilet) - vyoo (toilets)
Chuo (college) - vyuo (colleges
Chuo kikuu (university) - vyuo vikuu (universities)
Chombo (utensil) - vyombo (utensils)
Kiti (chair) - viti (chairs)
Kikombe (cup) - vikombe (cups)
Kisu (knife) - visu (knives)
Kiazi kitamu (sweet potato) viazi vitamu (sweet potatoes)
Kitunguu (onion) - vitunguu (onions)
Kitabu (book) - vitabu (books)
Kipindi (session) - vipindi (sessions)

Kipindi cha redio (radio program)

Kiatu (a shoe) - viatu (shoes)

3. Nouns that change in plural by taking ma, me

Jiko (kitchen) - Meko (kitchens)
Jino (tooth) - meno (teeth)
Jokofu (refrigerator) - majokofu (refrigerators)
Dirisha (window) - madirisha (windows)
Soko (market) - masoko (markets)
Duka (shop) - maduka (shops)
Gimbi (yam) - magimbi (yams)
Daftari (exercise book) - madaftari (exercise books)
Dawati (desk) - madawati (desks)
Shati (shirt) - mashati (shirts)
Gwaride (parade) - magwaride (parades)

4. (i) Nouns that change into plural form by dropping U.

Ukuta (a wall) - kuta (walls)
Ufunguo (a key) - funguo (keys)
Ugunduzi (invention) - gunduzi (inventions)
Uvumbuzi (discovery - vumbuzi (discoveries)
Ufito (rod) - fito (rods)

4. (ii) Nouns that change into plural by taking N or M

Wavu (wire mesh) - nyavu (wire meshes)
Waya (wire) - nyaya (wires)
Wembe (razor) - nyembe (razors)
Wenzo (lever) - nyenzo (levers)
Ua (precinct - nyua (precincts)
Ua (fence) - nyua (fences)
Ungo (winnowing basket) - nyungo (winnowing baskets)
Ubao (plank) - (n)bao normally written ‘mbao’

5. Nouns that change into plural by taking MI

Mlango (door) - milango (doors)
Mto (river) - mito (rivers)
Mlima (mountain) - milima (mountains)
Mtelemko (slope) - mitelemko (slopes)

6. Nouns that changes into plural by taking ‘wa’

Mwalimu (teacher) - walimu (teachers)
Mwanafunzi (student) - wanafunzi (students)
Mkufunzi (trainer) - wakufunzi (tutors)
Mkurufunzi (trainee) - wakurufunzi (trainees)
Mteja (customer) - wateja (customers)
Mnyama (animal) - wanyama (animals)
KITENZI JINA (INFINITIVE) KUTUMIKA K**A KITENZI SHINA (STEM FORM VERB)
Na George Mwidima Kihanda. 23 Mei 2020.

Katika lugha mbalimbali hususani Kiswahili tuna kitenzi shina (stem form verb) na kitenzi jina (infinitive)

AINA YA KWANZA: VITENZI VYA SILABI MBILI VYA KUANZA NA IRABU VIONGEZAVYO (KU)
Aina hii ni ya vitenzi shina ambavyo vina SILABI MBILI TU na tumeona vinavyoanza na irabu, havianzi na herufi bubu.

Baadhi ya vitenzi shina (stem form verb) ni k**a hivi vifuatavyo:

OSHA
OGA
ENDA
EPA
IBA
ISHA
IVA

Vitenzi hivi Osha, Oga, Enda, Epa, Iba, Isha, Iva hutumika katika miundo mbili. Muundo wa kwanza huhusisha infinitive form ‘ku’ na bila kutumia ‘ku’ k**a ifuatavyo:

1. Kesho nita-oga asubuhi.
2. Eliza amemaliza ku-koga.
3. Kuoga ni jambo zuri.

K**a umewahi kuishi katika Afrika Mashariki na maeneo jirani utakuwa umewahi kusikia baadhi ya watu wakisema ku-koga, ku-kosha vyombo, umeni-kosha. n.k.

Tukichunguza matumizi ya KUOGA na KUKOGA hayana tofauti na matumizi ya KUEPA na KUKWEPA.

Ni swali la kujiuliza kwanini double infinitives zimetumika kuunda neno KUKWEPA na kwanini isiwe KUEPA pekee? Tunajua ni makosa kusema KUKWENDA kwa sababu hiyo itakuwa ni double infinitives kuzidisha maneno mawili ya ‘ku’.

FAIDA ZA KUTUMIA ‘KU’ KATIKA KUONESHA MSISITIZO AMRI.

Tunapotoa amri (Imperative Form) msisitizo huoneshwa zaidi tunapotumia infinitive form
K**a ifuatavyo:-

1. KWENDA ZAKO KULE
2. ENDA ZAKO BWANA/NENDA ZAKO

Unaposema Kwenda inaonesha amri kali kuliko ukisema enda au nenda.

ISHA/KWISHA: KWISHA inatokana na KU+ISHA lakini kuna kuisha na kwisha.

1. Mafuta yamekwisha
2. Mafuta yameisha.

Unaposema mafuta yameKWISHA hapo unatumia neno kwisha k**a kitenzi shina (stem form verb) sawa sawa na kitenzi shina ISHA.

KWISHA ni kitenzi shina kilichozaliwa kutokana na KITENZI JINA KUISHA.

ENDA/KWENDA: KWENDA inatokana na KU+ENDA lakini kuna kuenda na kwenda.

1. Watoto wamekwenda shuleni
2. Watoto wameenda shuleni.

Unaposema watoto wamekwenda shuleni hapo unatumia neno kwenda k**a kitenzi shina (stem form verb) sawa sawa na kitenzi shina ENDA.

KWENDA ni kitenzi shina kilichozaliwa kutokana na KITENZI JINA KUENDA.

N.B: Sentensi sahihi ni kusema KUENDA na KURUDI k**a tunazungumzia VITENZI JINA na si kusema KWENDA na KURUDI kwa vile tayari KWENDA inatumika k**a KITENZI SHINA.

Mifano mingine ni k**a ifuatavyo

OSHA: Umenikosha sana.

1. Eliza ataosha vyombo.
2. Eliza atakosha vyombo

OGA
1. Nitakoga muda ukifika
2. Nitaoga muda ukifika

ENDA
1. Nitaenda asubuhi sana
2. Nitakwenda asubuhi sana

EPA
1. Alitupa jiwe nikaepa.
2. Alitupa jiwe nikakwepa
IBA
1. Mtoto ameiba pesa.
2. Mtoto amekwiba pesa.

ISHA
1. Chakula kimeisha
2. Chakula kimekwisha

IVA
1. Ndizi zimeiva.
2. Gawio la fedha limekwiva.

AINA YA PILI: VITENZI VYA SILABI MBILI VYA KUANZA NA IRABU VIONGEZAVYO (W)
Nitazungumzia pia vitenzi shina vingine ACHA na EKA ambavyo hivi vina miundo miwili tofauti ya matumizi k**a ifuatavyo: -

EKA/WEKA
1. Nita-WEKA mbolea bustanini
2. Nita-EKA mbolea bustanini.

ACHA/WACHA

1. Nita-ACHA kuvuta sigara
2. Nita-WACHA kuvuta sigara

AINA YA TATU NI VITENZI VYA SILABI MOJA VICHUKUAVYO (KU)
Hali kadhalika nitazungumzia vitenzi vya SILABI MOJA ambayo hutumia vitenzi jina k**a vile vitenzi shina.

KULA, KUNYWA, KUNYA, KUFA, KUPA, KUJA

Vitenzi hivi vina tabia ya kuchukua KU katika sentensi za wakati ujao, uliopo na uliopita na hutupa mbali KU katika sentensi za wakati uliopo rahisi (Simple Present Tense) kwa mfano
TWALA, TWANYA, TWANYA, TWAFA, TWAJA.

KULA
1. Twala ugali kila wiki.
2. Tunakula ugali kila wiki.

KUJA
1. Uje hapa haraka (Tanzanian)
2. Ukuje hapa haraka (Kenyan)
3. Sijaja asubuhi (Present Perfect Negative) I have not come in the morning.

Imeandikwa na George Mwidima Kihanda - Afrika Mashariki.

https://englishswahilitranslationtanzania.bitrix24.site/
MAANA ZA RESPONSIBILITY AND ROLES KWA KISWAHILI.

Kwanza kabisa kumekuwa na tabia mbovu ya kuchanganya
maana za WAJIBU NA MAJUKUMU na leo nimeamua kuweka
wazi kwa kuzingatia Consistency k**a ifuatavyo hapa chini.

Je umewahi kusikia tafasiri ya sentensi : You are responsible?

You are responsible for…. hufasiriwa k**a Unawajibika kwa…..

Kwa kuzingatia [Consistency] hapa chini:

RESPONSIBLE = WAJIBIKA basi RESPONSIBILITY = WAJIBU

The plural of Responsibility is Responsibilities.

Note that the Noun Wajibu is in U/N Swahili Noun Class
For example: Ungo – nyungo, ua – nyua, uadhifa – nyadhifa,
wadhifa – nyadhifa, wembe – nyembe,

Therefore: Wajibu – Nyajibu

Maana ya ROLE ni JUKUMU na ROLES – MAJUKUMU

Maana ya POWER = MADARAKA

Si sahihi kusema wajibu ni madaraka, unaweza kuwa na wajibu
bila madaraka.

It is not correct to translate responsibility as power, because you
may have responsibility without power.

Play your role = timiza jukumu lako.

DUTY = RESPONSIBILITY = WAJIBU.

DUTIES = NYAJIBU.

Imeandikwa na mwenyewe mbobezi wa Kiswahili George Mwidima Kihanda.
NINI MAANA YA NENO HASA?

Neno hasa lina maana tatu tofauti kabisa.

MAANA YA KWANZA.

Maana ya kwanza ya neno HASA ni perform rituals, TAMBIKA, katika sehemu zenye mizimu

Mfano: Kesho tutaenda kuhasa chini ya mti mrefu wenye mizimu.
Kesho tutaenda ku-tambika chini ya mti.

Katika mfano huo hapo juu umethibitisha neno HASA ni KITENZI SIELEKEZI, kt [sie].

MAANA YA PILI
Maana ya pili ya neno HASA ni KIELEZI, kl

Hiki ndicho kitabu changu hasa. This is exactly my book.

I know her exactly. Ninamjua yeye hasa.

KIELEZI huelezea kitenzi kuhusu kiasi au namna kilivyofanyika.

MAANA YA TATU

Maana ya tatu ya neno HASA ni especially, most of all.

Mfano: Ninapenda wasichana HASA warwanda.
I like girls ESPECIALLY Rwandans or Rwandese.
---------------------------------------------------------------
Katika Kiswahili sanifu hakuna neno HASWA, neno haswa ni la mitaani kwa watu waliogopa kusoma karatasi nyeupe ambao humaanisha HASA.
MONOSYLLABLE VERBS – VITENZI VYA SILABI MOJA.
Vitenzi vya silabi moja ni vitenzi vyenye tamko moja tu la muunganiko wa herufi bubu na irabu (vokali). Kwa mfano ukichukua herufi bubu ‘f’ na irabu moja ‘a’ utapata kitenzi ‘fa’ hiki ni kitenzi cha silabi moja ‘fa’ iliyoundwa na herufi bubu moja na irabu moja.
YAANI: SILABI MOJA = HERUFI BUBU MOJA + IRABU MOJA.
Id est: i.e. yaani MONOSYLABLE = CONSONANT + VOCAL.
Yafuatayo hapa chini ni maneno ya silabi moja ya Kiswahili.
‘fa’ = die
‘la’ = eat
‘wa’ = be
‘nywa’ = drink
‘nya’ = poing, defecate

Kwa kutumia monosyllable ‘wa’ tunaweza kuunda maneno na sentensi k**a ifuatavyo:
1. Ku’wa’ mwalimu.
2. Napenda ni’we’ mwalimu
3. Inapendeza a’we’ mwalimu
4. Ili kuikuza lugha yetu sisi sote tu’we’ walimu wa kujitolea.

Na kwa kutumia monosyllable ‘la’ tunaweza kuunda sentensi hizi:
1. Ku’la’ chakula.
2. Napenda ni’le’ chakula
3. Inapendeza a’le’ chakula kizuri.
4. Ili kuikuza afya yetu sisi sote tu’le’ chakula bora.
Katika lugha ya Kiswahili kuna maneno mawili tofauti kabisa, maneno hayo ni ‘kua’ na ‘kuwa’. Neno ‘kua’ ni kitenzi kamili chenye silabi mbili ambapo ni tofauti na kitenzi-jina ‘kuwa’.
KITENZI JINA NI NINI?
Kitenzi jina ni nomino/jina liliundwa kutokana na kitenzi shina pamoja na kineno ‘ku’, kwa mfano kufa (dying) kula (eating), kunywa (drinking), kukua (growing)
KITENZI SHINA NI NINI?
Kitenzi shina ni kitenzi kabla hakijawekewa ‘ku, kwa mfano kimbia, imba, fa, la, nywa, nya, kua, zembea, n.k. Ukisema ‘kuzembea’ tayari kinakuwa ni kitenzi-jina.
Kitenzi-jina (infinitive) huundwa kwa kuongeza ‘ku’ mwanzoni mwa kitenzi chochote kile cha silabi moja au zaidi.
Kitenzi-jina cha kitenzi cha silabi mbili ‘kua’ ni ‘kukua’.
Kitenzi-jina cha kitenzi cha silabi moja ‘wa’ ni ‘kuwa’
Kumekuwa na wazungumzaji wa Kiswahili wanaochanganya matumizi kati ya ‘kuwa’ na ‘kua’ na leo hii ninawauliza je wakitaka kusema hivi “Nataka ni’we’ mwalimu” watatumia silabi gani ikiwa wanakataa kuwapo kwa kitenzi cha silabi ‘wa’ ambapo wao wanasema ‘kua mwalimu’ badala ya ‘kuwa mwalimu’?
Watasema ‘nataka nie mwalimu’?

Imeandikwa na mbobezi, mfuatiliaji wa lugha za Kibantu na Kiswahili.
George Mwidima Kihanda
Studied Internet Super User – University of Cape Town.
Studied Translation Quality Management – Tomsk State University – Russia.

We offer English and Swahili translation and secretarial services with credentials from Secondary School, Kiswahili A grade, and English B grade, we also offer Information Technology services, studied at University of Cape Town.

My page is about open and professional English-Swahili translation and computer services.

Operating as usual

Photos from English-Swahili Translation and Information Technology Services's post 14/06/2021

Kwema Wana!

Leo hapa nimepata wazo kuunda sakiti ambayo itagawa Volti 13V za Solar Battery ili nipate Volti 4V, 8V na 12V ili nije ni-feed moja kwa moja katika Smart Chip ya Battery ya Laptop ili nitumie battery la Solar la 100AH k**a backup ya chaji kuwasha laptop bila kutumia Inverter. Sitaki Inverter kwa sasa. Mwendo ni DC kwa DC.

Naomba mawazo yenu ili niweke Capacitor and Diode ili kuwa mtiririko usioyumba wa mkondo (current) na msukumo (voltage) katika mafungu matatu ya 4V, 8V na 12V kwa 2.16A

Mawazo yenu tafadhali hasa kuhusu capacitor and Diode na nifanyeje kusiwe na Voltage Drop kubwa ghafla?

Nimedownload app ya Resistor Color katika Android Play Store.

NB: Sakiti hii nimechora kwa program ya TinyCAD inapatikana bure hapa chini
https://sourceforge.net/projects/tinycad/

Repair Dead Li-ion Battery With Syringe | Lithium Ion Battery Repair 04/06/2021

Repair Dead Li-ion Battery With Syringe | Lithium Ion Battery Repair

Repair Dead Li-ion Battery With Syringe | Lithium Ion Battery Repair #LithiumBatteryRepair #18650BatteryRepair #LithiumionBatteryRepair Repair Dead Li-ion Battery With Syringe | Lithium Ion Battery Repair Hello Friends Assalam...

[05/03/21]   UMEME WA SOLAR NA MAHESABU KATIKA MFUMO WA 12 DC
Imeandikwa na George Mwidima Kihanda.

MATUMIZI YA TAA 4 @ WATT 3 NA TV 1 NDOGO @ WATT 30.
Taa 4 za solar za Watt 3 kila moja hutumia wastani wa Amps (A) 1.6 kwa saa moja kwa hesabu ya kila taa moja kutumia wastani wa Amps 0.4.

TAA 4
Taa hizo hapo juu zikiwaka kwa masaa 10 yaani kuanzia saa 1:00 jioni hadi saa 11 alfajiri zitakuwa zimetumia 0.4 Amp x taa 4 x saa 10 = 16 Amps.

Ili uweze kuwasha taa hizo kwa masaa 10 unahitaji kuwa na betri itayokupa Amps 16 kila siku ya Mungu na betri hiyo kubakiwa na Amps nyingine za kuhifadhi betri kwa vile haitakiwi kunyonywa Amps zote hadi sifuri 0 kwani itaua betri haraka.

Betri ndogo ya kuanzia ni ile ya 26Ah yaani 26Amps*h kwa vile itakupa Amps 16Amps*h na kubakiwa na 10Amps*h

K**a bajeti yako ni ndogo unaweza kununua betri ya 12Ah kwa kuanzia lakini taa zako zitawaka kwa masaa matano tu yaani 0.4 x taa 4 x saa 5 = 8Amps na kubakiwa na 4Amps kwa ajili ya uhai mrefu wa betri. Ili kuongeza masaa mengine matano itabidi ununue tena betri nyingine ya 12Ah kwa uzifunge in Parallel ili kupata 24Ah ili kuwasha taa 4 kwa masaa 10.

CHARGE CONTROLLER (KIDHIBITI CHAJI)
Unatakiwa ufunge kidhibiti chaji ambacho kitakuwa kinazuia betri isiliwe chaji hadi 0 ili kuzuia kuharibika. Kidhibiti chaji hiki au charge controller kitalinda betri yako isiharibike mapema kutokana na kunyonywa moto wote hadi 0 na kitazuia jua lisiendelee kuchaji betri pale inapojaa. Bila kidhibiti chaji jua litaendelea kuchaji betri yako na itapata moto kwa vile itakuwa imeshajaa na umeme unaozidi kuja utageuka kuwa joto na kuunguza betri yako. Charge controller ni muhimu sana.

KUWASHA TV YA WATT 30.
TV moja ya WATT 30 yaani 30W mara nyingi inakuwa na adaptor inayotumia wastani wa Amps 2 kwa saa kwa mfumo wa 12V. Ukizidisha 12V x 2A = 24W. Kuna wakati betri inakuwa na 13V x 2 = 26W. Kwa hesabu za makadirio 24W au 26W ni wastani wa 30W.

TV hii ya 30W inatumia Amps 2 kwa saa kwa hiyo kwa betri 24Ah inaweza kuwasha TV hii kwa saa 8 yaani 2A x saa 8 sawa na 16Ah na kubakiza 8Ah kwa ajili ya uhai wa betri libakiwe na chaji ya kuendelea siyo kubaki tupu yaani sifuri.

Ili kupata umeme vizuri hakikisha unatumia waya nzuri zenye upitishaji wa kutosha na katika waya zako kusiwe na Diode au fuse inayozuia kupitisha umeme vizuri ikibidi badilisha fuse weka inayopitisha umeme wa kutosha.

JUMLA YETU SASA.
Tumeona kwamba TAA 4 kwa masaa 10 = 16Amps
Na TV 1 ya 30W kwa masaa 8 = 16 Amps JUMLA 36Amps

Kwa hiyo tunahitaji betri 4 za 12Ah kupata 48Ah ambapo tutatumia 36 Amps na kubakiwa na 12Amps kwa ajili ya uhai wa betri zetu ili zisikaukiwe hadi 0 na kushindwa kuamka tena.

Solar Panel inayoweza kutupatia 4Ah kwa saa ni nzuri inaweza kuwa ya Watt 80 au Watt 100 inatosha kwa kuanzia huku polepole ukijipanga kuongeza solar na betri zingine pale uchumi ukiruhusu. Unaweza kuongeza na kufunga betri hizo in Parallel.

Asanteni kwa kusoma.

18/04/2021
MKALIMANI AZUA BALAA DODOMA/ATAFSIRI TOFAUTI KWA RAISI WA S.AFRICA/MSIBA WA JPM LEO...AZUA GUMZO 23/03/2021

MKALIMANI AZUA BALAA DODOMA/ATAFSIRI TOFAUTI KWA RAISI WA S.AFRICA/MSIBA WA JPM LEO...AZUA GUMZO

I felt honoured because President Magufuli was not a great traveler. He did not like traveling very much. He preferred to stay here at home. Ninajivunia kwa sababu Rais Magufuli hakuwa mtu wa kusafiri sana. Hakupenda kusafiri sana. Alipendelea kukaa hapa nyumbani. What does it mean to say I am honored? I feel honoured?
To feel very proud about something, often something that someone has bestowed upon one.

MKALIMANI AZUA BALAA DODOMA/ATAFSIRI TOFAUTI KWA RAISI WA S.AFRICA/MSIBA WA JPM LEO...AZUA GUMZO #MKALIMANI#MTAFSIRI#DODOMA#JPM

Buy, Sell and Exchange Crypto Ultra-Fast 12/01/2021

Buy, Sell and Exchange Crypto Ultra-Fast

https://switchere.com/?r=9i8tkwrkaskk

Buy, Sell and Exchange Crypto Ultra-Fast Safe, licensed and trusted crypto exchange services are at your convenience. Buy, sell or swap all leading coins the way you want and receive amazing cashback up to 1%. Multiple payment methods, user-friendly interface, instant delivery, secure transaction processing and best-paying affiliate progra...

[12/25/20]   Mkahawa – coffee tree

Mgahawa – café, canteen, restaurant

Laundry – nguo zifuliwazo

Disinfect – nyunyizia dawa

Sanitize – eua; takasa

You should notify – unapaswa kumjulisha – umjulishe

You should eat – unapaswa kula – ule

a weak immune system – mfumo dhaifu wa kinga NOT mfumo wa kinga dhaifu.

You may also add more structure by saying – mfumo mdhaifu wa kinga instead of mfumo dhaifu wa kinga although both are correct.

Mfumo (m)dhaifu

Remember Nouns in M/MI Noun Class prefer additional prefix m before an adjective, more example as follows:

Mto (m)refu – a long river

Mto (m)gumu – a hard pillow

Adverbs of Frequency

- Always (100%) – siku zote; mara zote
- Usually (90%) – Kwa kawaida (kwa kawaida lakini si mara zote)
- Often (70%) – mara nyingi; mara kwa mara

[11/23/20]   MATUMIZI YA COULD na SHOULD.
Imeandikwa na George Mwidima Kihanda tarehe 23 Novemba 2020.

Tunaweza kutumia maneno yote mawili COULD na SHOULD k**a namna ya kutoa ushauri kwa watu wanaohitaji ushauri wetu. Lakini namna hizo mbili ni tofauti kabisa.

Tunatumia SHOULD tunapotoa ushauri palipo na kitu kimoja tu cha uhakika kilicho dhahiri.

Tunatumia COULD tunapotoa ushauri palipo na uwezekano wa vitu vingine vingi vya kufanya.

MIFANO:

Kwa mfano unasikia mtu anasema “NINASIKIA KIZUNGUZUNGU”

Basi tumia SHOULD kwa vile wewe unataka kumshauri kitu kimoja tu cha kufanya ambacho ni kuenda kumwona daktari.

Mwambie hivi: YOU SHOULD SEE A DOCTOR.

Lakini k**a uwezekano wa kumshauri vitu vingi kwa mfano:
- Anywe maji.
- Ale chakula,
- Apumzike,
- Apime malaria

basi unaweza kumwambia hivi:

YOU COULD DRINK WATER

YOU COULD EAT

YOU COULD RELAX

YOU COULD TEST FOR MALARIA

[10/05/20]   Power of attorney: the legal right to act for someone else in their financial or business matters, or the document which gives someone this right.

Haki ya kisheria kutimiza kwa ajili ya mtu fulani mwingine katika masuala yake ya kifedha, shauri au biashara, au hati inayompa mtu fulani haki hii.

22/06/2020

Attending Brain Buster Quiz at International School of Tanganyika on 09th March 1996 at Masaki Dar es Salaam, Tanzania.

[05/31/20]   UUNDAJI SENTENSI ZA KISWAHILI HUHITAJI UJUZI WA NGELI.
Imeandikwa na George Mwidima Kihanda, tarehe 31 Mei, 2020.

Kwanza kabila kabla sijazungumzia NGELI maneno ya Kiswahili
Hutamkwa kwa ngazi ya SILABI yaani kwa kuunga HERUFI BUBU
na IRABU k**a ifuatavyo:

KA-NI-SA not KAN-ISA

And

- a is pronounced as a in bad.
- e is pronounced as e in bed.
- i is pronounced as i in pit.
- o is pronounced as o in pot.
- u is pronounced as u in put.

Uundaji wa sentensi za Kiswahili tokea mwanzo kabisa kwa mwanafunzi
Huhitaji ujuzi au ufahamu wa ngeli.

Iwe kwa mwanafunzi wa hatua ya mwanzo au hatua ya juu zaidi.
Ujuzi au ufahamu wa ngeli (Noun Class) humsaidia sana mwanafunzi
huyo kuwa mahiri katika uzungumzaji na uandikaji wa lugha ya Kiswahili.

Pamoja na mbinu zingine za masomo mepesi kwa mwanafunzi wa awali
lakini msititizo katika ngeli humjenga na kumfanya aweze kujiamini
katika kuzungumza Kiswahili.

Kutokana na hoja hiyo hapo juu ndiyo maana nasisitiza ufundishaji wa
ngeli wa wanafunzi wa kigeni kwa kutumia lugha yao ya Kiingereza.

Kwa kuwa lugha ya Kiswahili ina ngeli tofauti ambazo hutumia
KIONESHI tofauti kulingana na NGELI yenyewe kwa hiyo nimeamua
kufafanua VIONESHI VYA SARUFI k**a ifuatavyo:

Demonstrative describes words such as 'this', 'that', 'these' and 'those'
that show which person or thing is being referred to

In the sentence 'This is my brother', 'this' is a demonstrative pronoun.

KIONESHI NI NINI KATIKA SARUFI?
Kioneshi (demonstrative) ni neno ambalo huonesha mtu au kitu
kinachozungumziwa katika sentensi. Kioneshi ni k**a vile:

KIONESHI CHA KARIBU
- hili, haya.
- haka, hutu,
- hii, hizi
- hiki, hivi,
- huu, hizi
- huyu, hawa.

KIONESHI CHA MBALI
- hilo, hayo
- hako, huto
- hiyo, hizo (hiyo ni Glide formation ya hio)
- hiko, hivyo ( hivyo ni mazoea badala ya hivo)
- huo, hizo
- huyo, hao (hao ni mazoea badala ya hawo)

Katika uundaji wa sentensi na uzungumzaji kuelezea vitu na viwakilishi
vya vitu upande wa KITENDA (SUBJECT) na KITENDWA (OBJECT)
hutegemea sana KIONESHI CHA KARIBU kuliko KIONESHI CHA MBALI
k**a ifuatavyo:

KIONESHI KATIKA NGELI YA (JI)/MA

Hi(li) jiwe (li)meporomoka, (li)ta-umiza watoto. hapa (li) imetumika k**a
KIWAKILISHI CHA KIONESHI CHA KITENDA (SUBJECT)

Tuta(li)ondoa jiwe hili. (Hapa (li) imetumika k**a KIWAKILISHI CHA KIONESHI
CHA KITENDWA (OBJECT)

Ukichunguza (li) zilizowekwa kwenye mabano linatokana na
KIONESHI CHA KARIBU HI(LI). Kwa hiyo basi LI ni kiwakilishi cha
KIONESHI HILI ambacho HUWAKILISHA NOMINO iliyo katika ngeli ya (JI)/MA

Ngeli ya (JI)/MA huwa na maneno mengi yanayoanza na JA, JE, JI, JO, JU
na ndiyo maana tumeweka (JI) katika mabano kuonesha kubadilika kuwa
JA, JE, JI, JO, JU maneno haya ni k**a JAGI, JENGO, JIWE, JOHO, JUMBA.
Maneno haya hutumia KIONESHI HILI.
Maneno haya pia huchukua MA katika kuunda wingi kwa mfano
JAGI > MAJAGI,
JENGO>MAJENGO,
JIWE>MAWE, JOHO>MAJOHO,
JUMBA>MAJUMBA.
Kwa vile maneno haya huchukua MA katika wingi ndiyo maana huwekwa
katika daraja (JI)/MA ambapo daraja la nomino huitwa ngeli kwa Kiswahili.
Na katika wingi wa maneno haya hutumia KIONESHI ‘HAYA’ k**a ifuatavyo:

Ha(ya) mawe (ya)meporomoka, (ya)ta-umiza watoto.
Hapa (ya) imetumika k**a KIWAKILISHI CHA KIONESHI CHA KITENDA (SUBJECT)

Tuta(ya)ondoa mawe haya.
(Hapa (ya) imetumika k**a KIWAKILISHI CHA KIONESHI CHA KITENDWA (OBJECT)

NGELI (JI)/MA huchukua pia na maneno yote ambayo huanza na silabi zingine zozote
si lazima JA, JE, JI, JO, JU lakini maneno hayo lazima yaanze na MA katika wingi.

Kwa mfano: -

- GARI > MAGARI
- BATI > MABATI
- BOMBA > MABOMBA.

Imeandikwa na George Mwidima Kihanda. 31 Mei 2020

englishswahilitranslationtanzania.bitrix24.site 24/05/2020

Home

KITENZI JINA (INFINITIVE) KUTUMIKA K**A KITENZI SHINA (STEM FORM VERB)
Na George Mwidima Kihanda. 23 Mei 2020.

Katika lugha mbalimbali hususani Kiswahili tuna kitenzi shina (stem form verb) na kitenzi jina (infinitive)

AINA YA KWANZA: VITENZI VYA SILABI MBILI VYA KUANZA NA IRABU VIONGEZAVYO (KU)
Aina hii ni ya vitenzi shina ambavyo vina SILABI MBILI TU na tumeona vinavyoanza na irabu, havianzi na herufi bubu.

Baadhi ya vitenzi shina (stem form verb) ni k**a hivi vifuatavyo:

OSHA
OGA
ENDA
EPA
IBA
ISHA
IVA

Vitenzi hivi Osha, Oga, Enda, Epa, Iba, Isha, Iva hutumika katika miundo mbili. Muundo wa kwanza huhusisha infinitive form ‘ku’ na bila kutumia ‘ku’ k**a ifuatavyo:

1. Kesho nita-oga asubuhi.
2. Eliza amemaliza ku-koga.
3. Kuoga ni jambo zuri.

K**a umewahi kuishi katika Afrika Mashariki na maeneo jirani utakuwa umewahi kusikia baadhi ya watu wakisema ku-koga, ku-kosha vyombo, umeni-kosha. n.k.

Tukichunguza matumizi ya KUOGA na KUKOGA hayana tofauti na matumizi ya KUEPA na KUKWEPA.

Ni swali la kujiuliza kwanini double infinitives zimetumika kuunda neno KUKWEPA na kwanini isiwe KUEPA pekee? Tunajua ni makosa kusema KUKWENDA kwa sababu hiyo itakuwa ni double infinitives kuzidisha maneno mawili ya ‘ku’.

FAIDA ZA KUTUMIA ‘KU’ KATIKA KUONESHA MSISITIZO AMRI.

Tunapotoa amri (Imperative Form) msisitizo huoneshwa zaidi tunapotumia infinitive form
K**a ifuatavyo:-

1. KWENDA ZAKO KULE
2. ENDA ZAKO BWANA/NENDA ZAKO

Unaposema Kwenda inaonesha amri kali kuliko ukisema enda au nenda.

ISHA/KWISHA: KWISHA inatokana na KU+ISHA lakini kuna kuisha na kwisha.

1. Mafuta yamekwisha
2. Mafuta yameisha.

Unaposema mafuta yameKWISHA hapo unatumia neno kwisha k**a kitenzi shina (stem form verb) sawa sawa na kitenzi shina ISHA.

KWISHA ni kitenzi shina kilichozaliwa kutokana na KITENZI JINA KUISHA.

ENDA/KWENDA: KWENDA inatokana na KU+ENDA lakini kuna kuenda na kwenda.

1. Watoto wamekwenda shuleni
2. Watoto wameenda shuleni.

Unaposema watoto wamekwenda shuleni hapo unatumia neno kwenda k**a kitenzi shina (stem form verb) sawa sawa na kitenzi shina ENDA.

KWENDA ni kitenzi shina kilichozaliwa kutokana na KITENZI JINA KUENDA.

N.B: Sentensi sahihi ni kusema KUENDA na KURUDI k**a tunazungumzia VITENZI JINA na si kusema KWENDA na KURUDI kwa vile tayari KWENDA inatumika k**a KITENZI SHINA.

Mifano mingine ni k**a ifuatavyo

OSHA: Umenikosha sana.

1. Eliza ataosha vyombo.
2. Eliza atakosha vyombo

OGA
1. Nitakoga muda ukifika
2. Nitaoga muda ukifika

ENDA
1. Nitaenda asubuhi sana
2. Nitakwenda asubuhi sana

EPA
1. Alitupa jiwe nikaepa.
2. Alitupa jiwe nikakwepa
IBA
1. Mtoto ameiba pesa.
2. Mtoto amekwiba pesa.

ISHA
1. Chakula kimeisha
2. Chakula kimekwisha

IVA
1. Ndizi zimeiva.
2. Gawio la fedha limekwiva.

AINA YA PILI: VITENZI VYA SILABI MBILI VYA KUANZA NA IRABU VIONGEZAVYO (W)
Nitazungumzia pia vitenzi shina vingine ACHA na EKA ambavyo hivi vina miundo miwili tofauti ya matumizi k**a ifuatavyo: -

EKA/WEKA
1. Nita-WEKA mbolea bustanini
2. Nita-EKA mbolea bustanini.

ACHA/WACHA

1. Nita-ACHA kuvuta sigara
2. Nita-WACHA kuvuta sigara

AINA YA TATU NI VITENZI VYA SILABI MOJA VICHUKUAVYO (KU)
Hali kadhalika nitazungumzia vitenzi vya SILABI MOJA ambayo hutumia vitenzi jina k**a vile vitenzi shina.

KULA, KUNYWA, KUNYA, KUFA, KUPA, KUJA

Vitenzi hivi vina tabia ya kuchukua KU katika sentensi za wakati ujao, uliopo na uliopita na hutupa mbali KU katika sentensi za wakati uliopo rahisi (Simple Present Tense) kwa mfano
TWALA, TWANYA, TWANYA, TWAFA, TWAJA.

KULA
1. Twala ugali kila wiki.
2. Tunakula ugali kila wiki.

KUJA
1. Uje hapa haraka (Tanzanian)
2. Ukuje hapa haraka (Kenyan)
3. Sijaja asubuhi (Present Perfect Negative) I have not come in the morning.

Imeandikwa na George Mwidima Kihanda - Afrika Mashariki.

https://englishswahilitranslationtanzania.bitrix24.site/

englishswahilitranslationtanzania.bitrix24.site Sharing Common Parts of English

[05/17/20]   Maana ya Central:

Neno central linatokana na maneno mawili ‘centre’
na kikomo yaani suffix –al. Kwa lugha hiyo hiyo na si
nyingine ni kwamba ‘centre + al = central. Nini maana
ya suffix –al. Suffix –al maana yake ni ‘ya’ kwa Kiswahili.
Kwa mfano neno ‘national’ maana yake ni ‘ya taifa’.
Mfano National Bank maana yake ni Benki ya Taifa.
Si vibaya kuita pia Banki ya Taifa. Tofauti za Benki na Banki
haziharibu maana kwa vile yote ni sawa.

Maana za Neno Central.

Central = ya katikati; (principal) -kuu; ya maana, ya muhimu.

Central maana yake ni ya kati, k**a ofisi ni ya kati basi moja
kwa moja kwa ofisi hiyo kuwa kati inakuwa ‘muhimu’ kwa
vile ni ‘ya kati’. Na kwa vile ni ‘ya kati’ na ni ‘muhimu’ basi ofisi
hiyo inaweza kuwa ni ‘kuu’ kutokana na umuhimu wake wa
kuwa ya kati.

Tukiangalia katika kamusi neno Central kwa upande wa
Kiinglanzi tunapata:
- Central = of centre
- Important
- central registry n masijala kuu.
- central heating n upashaji joto mabomba toka kituo kikuu
- central committee k**ati kuu.
- the central government n serikali kuu
- centralism n mfumo wa mamlaka toka sehemu moja, mfumo kati, ukati

KIKOMO AU SUFFIX - IZE

Ukichukua neno CENTRAL + IZE = CENTRALIZE
Unapata kitenzi centralize ambacho kinabadili adjective central
kuwa kitenzi maana ikiwa kufanya ofisi au kitu kuwa muhimu,
katikati au kuwa kikuu.

centralize vt,vi leta/weka katikati; weka chini ya makao makuu.

centralization n. uwekaji kitu kuwa kikuu au muhimu.

Imeandikwa na mwenyewe mzingatifu:
George Mwidima Kihanda wa Afrika Mashariki.

[05/17/20]   MAANA YA NENO KIMBARI

Neno ‘kimbari’ limetokana na vitu viwili
Cha kwanza ni KITANGULIZI yaani PREFIX ‘ki’
Cha pili ni neno shina lenyewe ‘mbari’

MBARI ni neno linaloelezea ASILI ya watu.
MBARI si UKOO bali asili ya watu kwa vinasaba
au GENES.

TOFAUTI YA MBARI NA UKOO
MBARI maana yake ni RACE wakati UKOO = CLAN

UKOO unaweza kuwa na watu wa MBARI tofauti
Yaani RACE tofauti. Kwa mfano UKOO unaweza
kuwa na watu kutoka UCHINA, AFRIKA, UARABUNI
ambao wameoana na kuzaliana.

MBARI ni aina moja ya watu mfano WACHINA tu
WAAFRIKA tu na WAARABU tu. MBARI = RACE

GENOCIDE NI NINI?
Neno GENOCIDE linatokana na maneno mawili

GENES + CIDE = GENOCIDE

KIKOMO au SUFFIX –‘CIDE’ maana yake ni KUUA

Mfano INSECT + CIDE = INSECTICIDE yaani ya
KUUA WADUDU

INFANT + CIDE = Kuua vitoto Vichanga

FRATRICIDE = Kuua kaka zako

Kwa hiyo GENOCIDE = Ya kuua watu wa asili moja
Yaani mauaji ya kuua watu wa RACE moja.

ASILI MOJA = RACE MOJA = MBARI MOJA

RACE si UKOO, mnaweza kuwa kabila moja
lakini si ukoo mmoja bali ninyi ni race moja au asili moja
au mbari moja.

Ukiua wananchi wote hiyo inakuwa ni HOLOCAUST
Si genocide, genocide inalenga asili moja ya watu.

Imeandikiwa na mwenyewe mwandishi
George Mwidima Kihanda wa Afrika Mashariki.

Location

Products

English - Swahili Translation at USD 0.05 per word.
Proofreading at USD. 0.02 per word

Telephone

Address


Bomani, Sengerema
Mwamza
TZ

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 22:00
Wednesday 07:00 - 22:00
Thursday 07:00 - 17:00
Friday 09:00 - 22:00
Saturday 07:00 - 22:00
Sunday 07:00 - 17:00
Other Mwamza schools & colleges (show all)
Mwanza rainbow academy of art Mwanza rainbow academy of art
Kirumba
Mwamza, +255 757 345 921/+255 715 345 921

Its forefront in art management,talent discovery,booking & posting of models,stage and TV plays,Adverts,events management,music and dancing.!

Wandera Institute of Tourisim & Hotel Management Wandera Institute of Tourisim & Hotel Management
[email protected]
Mwamza

CHUO CHETU KINA PATIKANA MWANZA WILAYA YA ILEMELA KINA WALIMU KABAMBE WALIO BOBEA KUFUNDISHA CORS MBALI MBALI

Tumain english medium Tumain english medium
Makonge
Mwamza, 0000

advertising tumaini

LEDA Computronics & It Solutions Company LEDA Computronics & It Solutions Company
Mwamza, 255

LEDA Computronics & IT Solutions is a technological company dealing with designing, developing, maintenance and recycling of electronic devices