Benito Mhelela

Benito Mhelela

Computer Repairing, Computer Networking, Sales Computer, Website Designing, Computer Software Installation, Internet Service, Scanning, Printing, Fax.

Computer Repairing, Computer Networking, Sales Computer, Website Designing, Computer Software Installation, Internet Service, Scanning, Printing, Fax, Face Book, Skype, Twitter, Google And Yahoo.

Operating as usual

25/08/2020

Brooklyn Fashion Soweto Mbeya Pambakali

B.M IT SOLUTION tulishaanza kazi rasmi ya kujaza fomu za Maombi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza, kuhakiki vyeti vya vifo na vya kuzaliwa kupitia RITA (E-Huduma) pamoja na kufanya application za kujiunga na vyuo vikuu vyote nchini kwa ngazi ya astashahada, stashahada na shahada.

Na kwa kumalizia tu mwaka huu tumekusogezea na huduma za kisheria au ofisi za mawakili tupo karibu nao, nina maanisha ya kwamba hauna haja ya kuanza kutafuta ofisi za mawakili ili fomu zako zigongwe mihuri kila kitu utahudumiwa hapo hapo.

Wewe ukitoka ofisini kwetu safari inayofuata ni kwenda Kwenye ofisi za serikali za mitaa kwa ajili ya kumalizia hatua za mwisho na baada ya hapo utarudi tena kwa ajili ya ku scan na kuambatanisha ukurasa namba mbili na ule wa namba tano. Na ukimaliza sasa unachotakiwa ni kwenda mahali zilipo ofisi za posta kwa ajili ya kutuma fomu zako kwa njia ya EMS kwenda Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Dar Es Salaam.

Pia Tunahuduma za ziada kama Vile Internet Café, Photocopy, Scanning, Lamination, Printing Colored , Printing Black & White, Typing ,Passport Size Kwa Dakika3,.

Tuna Uza Flash Za Aina Zote , Chaja Za Simu OG, Memory Card, Batteries , Usb Cable ,Ups, Earphone, Rim Paper, Mouse, Keyboard , Power Cable, Software Za Aina Mbali Mbali , Ant-Virus, Computers Maintenance, Kusafisha Picha Za Kwenye Flash, Memory Card Na Simu, Pata Miziki Ya Aina Mbali Mbali Rhumba, Bolingo, Rnb, Hiphop, Slow Jams Na Pia Tuna Movies Kali N.K

Tuna uzoefu na kazi hii kwa zaidi ya miaka 4 sasa pia kama una swali au maoni piga simu au tuma ujumbe mfupi wa simu tutakujibu kadri ya uwezo wetu wasiliana nasi kwa simu nambari whatsapp no 0777392940 or >>>>>0744599814 txt/call>>>>>>>>>>0674416471.
Tupo Soweto-Mbeya Karibu na Mkulu Hotel au Kick Garage.
Na yale yaliyo nje ya uwezo wetu tafadhali wasiliana na watu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu watakusaidia kwa njia ya simu au barua pepe yao ambayo ni [email protected] nambari zao ni 0736 66 55 33 (WhattsApp); 022 550 7910

ASANTE NA KARIBUNI SANA.

07/07/2019

MAMBO NI MENGI, MUDA NI MCHACHE. HAKIKISHA UNAFANYA KILICHOKULETA DUNIANI.


Kwa wale wote wanaotarajia kuomba mkopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yaani (Higher Education Students' Loans Board- HESLB)
Unaweza kufika katika ofisi zetu za B.M IT Solution, Brighter Stationery pamoja na Lilian Stationery zilizopo maeneo ya Soweto Mbeya ili uweze kufanya maombi kwa njia ya mtandao (Online Loan Application and Management System).

Nama ya kufika ofisini kwetu fuata maelekezo haya hapa .

Kama Unatokea Stendi Kuu Mjini Shukia Kituo Cha Daladala Soweto Stendi kushoto kwako Halafu Pandisha Na Barabara Inayoelekea Paradise Hotel Au Gr Hotel.

Kama unatokea Uyole Shukia Mama John Stendi uwe kama unaelekea Mkulu Hotel Au Kiwira Motel.

Na kama unatokea mbalizi shukia kituo Cha Daladala Soweto Stendi kushoto kwako Halafu Pandisha Na Barabara Inayoelekea Paradise Hotel Au Gr Hotel ukishafika piga simu namba zifuatazo 0744-599-814 au 0777 - 392-940 halafu utapokelewa na wahudumu wetu.

Pia usisite kuuliza chochote kuhusiana na masuala ya bodi ya mikopo utajibiwa kulingana na uwezo wetu. Na maombi yameanza rasmi tangu tarehe 1 July 2019 mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 August 2019.

1. Pia Kwa wale wanaotaka kujiunga na vyuo mbali mbali kwa ngazi ya ngazi ya Astashahada (Certificate) Na Stashahada (Diploma) kwa kada ya afya (Health and Allied Sciences) kupitia NACTE huduma hiyo pia inatolewa na mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 02/09/2019.

2. Kutuma na kupokea vyeti vya kuzaliwa au vya vifo vilivyohakikiwa na RITA kupitia uhakiki portal huduma hiyo pia inatolewa.

3. Mwisho kabisa kwa wale wanaotaka kusoma ngazi ya Shahada kwa maana ya (Bachelor Degree) vyuo mbalimbali hapa nyumbani maombi yao pia tunafanya kwa njia ya mtandao.

Free Soft Drinks kwa wateja wetu wote ambao wataweza kufika na kufanya huduma yeyote ile kwenye ofisi zetu zilizopo Soweto Mbeya.
Vinywaji ni bure kwa wateja wetu wote kuna Juice, Soda Na Maji isipokuwa pombe tu.

4. Ili kupata huduma zetu iwe ni za Stationery , Online Application , kujaza fomu za bodi ya mkopo , Scanning , Photocopy , Typing , Printing , Lamination , Binding , Internet Cafe , Software , OS na nyingine nyingi.

Call us 0744-599-814 / 0777-392-940

E - Mail address: [email protected] or [email protected]

07/07/2019

Benito Mhelela's cover photo

06/05/2019

Benito Mhelela

06/05/2019

Benito Mhelela's cover photo

06/05/2019

Ratiba ya kuupokea mwili wa Marehemu Dr. Reginald Mengi, Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere imeelezwa kuwa itafanyika Leo Jumatatu, saa 8:00 mchana.

Mwili wake utaletwa na ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kutokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).

Baada ya mwili kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa JNIA, utapitishwa katika maeneo ya Tazara, Buguruni, Ilala, Kigogo, Magomeni hadi Kinondoni.

Imeelezwa baada ya Kutoka Kinondoni, mwili wake pia utapitishwa hadi katika maeneo ya Morocco, barabara ya Bagamoyo, Sayansi, Mwenge hadi katika hospitali ya Lugalo ambako mwili wa Dr. Reginald Mengi utahifadhiwa.

Ratiba hiyo itaendelea kesho siku ya Jumanne ya Mei 7, 2019, ambapo mwili utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya watu wote kuuaga na kisha utarejeshwa nyumbani kwake eneo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Aidha Siku ya Jumatano mwili wa Marehemu utasafirishwa kupelekwa Machame Moshi mkoani Kilimanjaro ambako Ibada na mazishi yatafanyika siku ya Alhamis katika kanisa la K.K.K.T Kisereni.

[04/13/19]   Waziri wa ulinzi wa Sudan aliyetwaa madaraka ya uongozi baada ya mapinduzi ya kijeshi ya kumuondoa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Omar al Bashir amejiuzulu.

Awad Ibn Auf ametoa tangazo hilo la kujiuzulu kupitia Televisheni ya taifa hilo na kumtaja mrithi wake kuwa Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan.

Wananchi wa Sudan wamekuwa wakiendelea na maandamano hata baada ya kuondolewa madarakani kwa al Bashir wakishinikiza mabadiliko ya utawala mzima uliokuwa chini ya rais huyo aliyeongoza tangu mwaka 1989.

Jeshi la nchi hiyo lilitangaza kushika hatamu za nchi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili.

[04/11/19]   SERIKALI ya nchini Sudan, leo imeondolewa madarakani na jeshi la ulinzi la nchi hiyo, na kutangaza kumkamata Rais Omar Al-Bashir.

Kiongozi huyo ambaye amekaa madarakani kwa miaka 30, ameondolewa kufuatia maandamano ya wananchi ambayo yamedumu kwa takribani miezi kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa ya kijeshi iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa nchini humo leo Alhamisi Aprili 11, 2019, imesema Al Bashir amevuliwa kwa nguvu cheo cha kuwa kiongozi mkuu na kupelekwa "sehemu salama."

Akitoa taarifa kwa umma ya kuondolewa kiongozi huyo, Makamu wa Bashir ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Jenerali Awad Ibn Auf, amesema kuanzia sasa nchi hiyo itaongozwa na serikali ya mpito ya kijeshi itakayotawala kwa miaka 2.

"Jeshi la ulinzi limechukua madaraka ya kuongoza wananchi ili kurejesha utengamano kwa Wasudan wote kuishi kwa amani na utulivu," imesema taarifa hiyo na kukaririwa na shirika la habari la Ufaransa (AFP).

Jenerali Auf ametangaza hali ya hatari ya miezi 3 sanjari na kusimamisha Katiba ya nchi hiyo, ambayo ilitungwa mwaka 2005.

Jenerali huyo amesema kuwa anga ya nchi hiyo imefungwa kwa saa 24 zijazo kuanzia tangazo hilo, na pia kufungwa mipaka yote ya Sudan.

Akitangaza vipaumbele vya serikali hiyo mpya, jenerali huyo amesema taasisi zote za kiutawala nchini humo, likiwemo bunge na baraza la mawaziri zimevunjwa ili kutoa nafasi ya kile alichokiita ni "kutoa nafasi ya kuandaliwa uchaguzi mkuu huru na wa haki.

Omar Bashir (75) ambaye pia ni Jenerali wa jeshi alishika madaraka ya kuongoza Sudan akiwa Rais wa 7 mwaka 1989, kufuatia mapinduzi yaliyoondoa serikali ya kiraia ya Waziri Mkuu Sadiq Al-Mahdi (sasa umri miaka 83).

Al Bashir ambaye licha ya kuwa na wake 2 hana mtoto, mwaka 2008 alikabiliwa na shinikizo la kimataifa kutaka akamatwe na kupelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC), yenye makao makuu mjini The Hague nchini Uholanzi.

Serikali yake ilikuwa ikishutumiwa kwa tuhuma za mauaji ya wananchi wa jimbo la Darful nchini humo, katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.

[01/29/19]   Mwaka 1969 Jijini Washington, Majenerali watatu kutoka Pentagon walikuwa wakipata Mlo wa jioni pamoja na Maofisa watano wa Jeshi la Chile ...Mwenyeji wa Chakula hiki kilichosindikizwa na Maongezi ya Siri alikuwa ni Luteni kanali Gerardo Lopez Angulo, Huyu alikuwa ni Afisa wa jeshi la Anga la Chile aliyekuwa hapo Marekani kikazi...Wageni toka Chile katika kikao hiki waliongozwa na Mkurugenzi wa Chuo cha kijeshi cha Mambo ya Anga nchini Chile Jenerali Carlos Toro Mazote,..huyu alifika Washington mapema siku moja kabla ya Kikao.

Naam!, Jumla ya Maofisa 8 wa Jeshi wakiwa ktk Dinner hii Jijini Washington walikula Matunda ya kila aina,Nyama Choma na Mvinyo Mtamu huku wakishangaa Barafu inayoanguka kila Mahari huku Ndege wengi wakiimba na kurukaruka... na ikumbukwe kabla ya Kikao Majenerali hawa walitokea Beach Kuogelea.

Mazungumzo ya jioni hiyo yalihusu zaidi Uchaguzi Mkuu wa Chile ambao ungefanyika Mwaka unaofuatia, Mmoja wa Majenerali toka Pentagon aliwauliza wale Maofisa wageni toka Jeshi la Chile swali moja tu la Msingi " Huyu mtu anayeitwa Salvador Allende tunajua kabisa Siasa na Misimamo yake ni ya Mlengo wa kushoto, sasa je iwapo atachaguliwa na wananchi katika Uchaguzi ujao nyinyi Mtafanya nini kuhusu hili?"

Jenerali Carlos Toro Mazote alijibu.“ Hilo tu?, Tutaichukua Ikulu ya La Moneda ndani ya Nusu saa tu, hata kama itatulazimu kuichoma Moto" .

Sasa ni Miaka 46 imepita Tangu Rais Salvador Allende wa Chile auawe ndani ya Jumba la Kifahari la La Moneda mjini Santiago baada ya kuwindwa kwa miaka miwili tangu achaguliwe kuwa Rais Wa Chile,...Aliuawa akiwa anajaribu kujilinda na Bunduki yake aina ya AK-47 ambayo alipewa na Rais Fidel Castro wa Cuba aliyekuwa Rafiki yake...hii ilikuwa 1973.

Rais Salvador Allende aliuawa akiwa ndio kwanza ana miaka mitatu tu Madarakani pale Chile Tangu Achaguliwe mwaka 1970, Aliuawa katika Mapinduzi ya kijeshi Yaliyoasisiwa huko Marekani na Nafasi yake kuchukuliwa na Dikteta Augusto Pinochet .

Mjamaa Salvador Allende aliuawa mara Baada ya kuthubutu kuleta Sera bora kwa Watu Wa Chile, Sera ambayo ilinuia kutokomeza kabisa Umasikini wa watu wa chile na kuifanya Chile kuwa moja ya Mataifa makubwa kiuchumi kwa kutegemea Rasilimali zake yenyewe.

Leo tunaambiwa kwamba Kijana Mmoja Kiongozi Wa Upinzani huko Nchini Venezuela naye amejitangaza Rais bila Uchaguzi huku akishangiliwa na Marekani na Washirika Wake, je kuna Haja ya Kushangaa? Je nani hajui kuwa Venezuela ndiyo Nchi inayoongoza kwa Akiba kubwa ya Mafuta kwa Sasa Duniani ikifuatiwa na Saudi Arabia?, ...Shida ni "Mafuta".

Unaposikia Kiongozi Wa Upinzani Venezuela anatangaza Maandamano ikiwa pamoja na kushawishi Jeshi la Nchi kupindua Serikali basi Rejea Mapinduzi ya kijeshi huko Chile ya 1973 yaliyoasisiwa na Watu 8 huko Washington mwaka 1979....tulisikia pia Gabon ikinusurika Kupinduliwa hapa Majuzi, Je nani hajui kuhusu Utajiri Wa Mafuta Wa Gabon?..na ni nani Mwingine aliyesalia Mbishi hapa Duniani ukiacha Iran na Venezuela?..

Maana Iraq ya Saddam Hussein na Libya ya Moummar Gaddafi tayari zililazimishwa kusalimu Amri...Mafuta yao hawa Walibya na Wa-Iraq yanaijenga Washington na Paris huku Raia wao Wakiteketea....Na Je Venezuela hii ya Wabishi Simon Bolivar, Hugo Chavez na Sasa Nicolous Maduro itasalimika ktk Vita hii?...Time Factor.

"Sipokei wala kutii Amri yoyote kutoka Mataifa ya Kigeni na Sitapokea Daima... siku zote nitapigania Raia wa Venezuela ambao wameamua kuwa huru chini yangu Rais huru katika Nchi huru" - Nicolous Maduro (Rais Venezuela).

[01/29/19]   Marekani imeishtaki kampuni kubwa ya mawasiliano ya China, Huawei na afisa wake mkuu wa maswala ya fedha, Meng Wanzhou kwa madai ya wizi wa teknolojia, ubadhirifu wa fedha na kupinga utekelezaji wa haki.

Marekani imedai kuwa Huawei inapotosha kufanya biashara na Iran kupitia kampuni ya Huawei device USA na Skycom Tech, Kampuni ya Huawei imekanusha madai hayo.

Katika taarifa iliyotoa kampuni hiyo, Huawei imesema kuwa imesikitishwa na mashtaka hayo dhidi ya yake.Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa haikufanya makosa yote yanayodaiwa na marekani na kuongeza kuwa haina ufahamu wa kosa alilotenda Bi Meng.

Kesi hiyo huenda ikazua mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China hali ambayo itaathiri biashara ya kampuni hiyo.

[01/16/19]   WATU 15 WABAINIKA KUFARIKI SHAMBULIZI LA NAIROBI KENYA.....Watu wasiopungua 15 wameuawa katika shambulio la kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabab linaloendelea katika hoteli kubwa ya kifahari ya DusitD2, katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, maafisa wa polisi ambao hawakutaja majina yao wameliambia shirika la Habari la AFP.
"Kwa sasa tuna watu 15 waliouawa katika shambulio, ikiwa ni pamoja na raia wa kigeni," amesema afisa wa kwanza wa polisi, idadi ambayo imethibitishwa na chanzo cha pili cha polisi ambacho kimekumbusha, hata hivyo, kwamba operesheni ya vikosi vya usalama "inaendelea" na kwamba polisi bado haijaweza kufikia katika baadhi ya maeneo ya jengo hilo.
Tayari kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia llimekiri kuwa limehusika na shambulio hilo linaloendelea.
Shambulizi hili, linawakumbusha wengi shambulizi la kigaidi lilitokea mwaka 2013 katika jengo la biashara la Westgate na kusababisha vifo vya watu 67.
Mwezi Aprili mwaka 2015 shambulizi lingine la kigaidi lilitokea katika Chuo Kikuu cha Garissa Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 148, wengi wao wakiwa wanafunzi.
Kenya ilianza kushuhudia milipuko ya kigaidi kutoka kwa kundi la Al Shabab mwaka 2011, baada ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia, kupambana na kundi hilo la kigaidi ambalo linapambana na serikali ya Mogadishu.

23/12/2018

Ndege za Airbus A220 zilikuwa zinafahamika kama Bombardier CS100s kabla ya Airbus kuununua mradi huo wa utengenezaji wa ndege za C Series. Ununuzi huo ulifanikishwa kupitia mkataba wa kibiashara kati ya kampuni ya Airbus na kampuni nyingine mbili: Bombardier Inc na Investment Québec ambao ulianza kutekelezwa 1 Julai, 2018.

Airbus sasa humiliki 50.01% yahisa katika ubia wa utengenezaji wa ndege hizo ambao kirasmi hufahamika kama C Series Aircraft Limited Partnership, huku Bombardier na Investment Québec wakimiliki takriban 34% na 16% ya hisa mtawalia. Makao makuu ya mradi huo wa utengenezaji wa ndege pamoja na karakana zake vyote vinapatikana Mirabel, Québec.

Kutokana na ushirikiano huo, na hali kwamba Airbus inamiliki hisa nyingi, mradi wa C Series huhesabiwa sasa kuwa chini ya Airbus.

Mambo Muhimu Kuhusu Airbus A220-300 :- Ndege hii urefu wake ni mita 38.7, na kwa jumla inaweza kubeba abiria 141. Urefu wake kutoka chini kwenda juu ni mita 11.5, na upana wa mabawa yake ni mita 35.1.

Airbus 220-300 inaweza kusafiri umbali wa 5,920km safari moja, na inaweza kupaa ikiwa na uzani wa tani 67.6, na kutua ikiwa na uzani wa tani 58.7. A220-300 ndiyo ndege kubwa miongoni mwa ndege za familia ya A220 na iliundwa kulenga soko la safari za ndege zinazowabeba abiria kati ya 130-160.

Ni ndege ambayo imeundwa kupunguza gharama ya matumizi yake ya mafuta kwa kila safari na pia kuwa yenye uwezo wa juu. Injini zake zimepunguza matumizi ya mafuta kwa kila abiria kwa asilimia 20 ukilinganisha na ndege za awali za aina yake.

Ndege za A220 zimejengwa kwa vipande vinavyoweza kutengenezwa kwa haraka kiwandani iwapo vitahitajika wakati wa ukarabati. Injini zake pia huwa za familia moja. Marubani waliozoea ndege aina ya A220-300 na A220-100 hawahitaji mafunzo zaidi kuweza kuziendesha.

[12/21/18]   Uchambuzi yakinifu na mwenyekiti wetu ndugu Majid Mjengwa ameangazia suala ya uchaguzi nchini DRC pia amenyambua historia ya wanaowania kiti hicho cha urais akiwemo Emmanuel Ramazani Shadary, Martini Fayulu na Felix Tchisekedi hakika ametutoa matongotongo.

Uchambuzi Wa Habari:

Uchaguzi Mkuu DR Congo Ulioota Mbawa..

- Umesogezwa mbele kwa uchache juma moja.

Imetangazwa jana Alhamisi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Corneille Nangaa, kuwa uchaguzi wa Urais Congo uliotarajiwa ufanyike keshokutwa umesogezwa mbele.
Sababu alizotoa ni za ' Kiufundi' ikiwamo moto wa Kinshasa wa hivi karibuni ulioteketeza baadhi ya masanduku na karatasi za kupigia kura. Mlipuko wa Ebola Kaskazini Mashariki ya Congo na mapigano ya Kaskazini Magharibi hususan maeneo ya Beni.

Tafsiri yake?

Nionavyo Uchaguzi Congo unabaki kuwa kizungumkuti. Kuna karata zinaendelewa kuchangwa. Hazijakaa sawa. Anayezichanga karata hizo ni ni Joseph Kabila.

Zikishakaa sawa uchaguzi utafanyika. Wacongo waendelee kuvuta subira. Kwenye mbio za Urais, namwona mgombea wa Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary kuwa yuko vizuri. Atashinda urais, lakini mbao ya urais inahitaji kumaliziwa kupigwa randa.

Wagombea wa upinzani watabaki kuangalia tu karata hizi za kisiasa zinavyochangwa. Felix Tchisekedi ni ' Jokeli' kwenye mchezo wa karata- albasitini ya Kabila.

Felix Tchisekedi ni karata ya Kabila aliyoitumbukiza mchezoni kuharibu hesabu za Martin Fayulu ambaye ndiye tishio kubwa kwa mgombea wa Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary. Tchisekedi ni mtoto wa mpinzani maarufu wa Congo enzi hizo kule Congo.

Mgawanyiko wa Congo ni upi?

Jibu:

Vita ya kisiasa katika DR Congo inahusu Balingala dhidi ya Baswahili. Inahusu ukabila pia.

Kutoka Lubumbashi Jimbo la Katanga kuelekea Kinshasa ni himaya ya WaAlunda. Watu wa jamii hii wenye kuongea Kilingala wanaamini Congo ni yao. Ukija chini Mashariki ya Congo kuelekea Kaskazini ni himaya ya WaAluba. Ni wenye kuongea Kiswahili. Ndiko iliko asili ya akina Kabila. Ni kutoka Goma hadi Bukavu.
Martini Fayulu ni Mlingala na Emmanuel Ramazani Shadary ni Mswahili.

Kuna mengi ya kuchambua.

Maggid

Whatsapp: 0688373652

Location

Products

NECTA, NACTE,TCU,HSLB REGISTRATION , HP, ACCER,TOSHIBA,DELL,IBM,
PRINTERS,SCANNER,FAX,
INTERNET SERVICES

Telephone