Knowing YOUR SELF

Knowing YOUR SELF

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Knowing YOUR SELF, Education, [email protected], Iringa-Mvumi.

Operating as usual

[01/01/15]   .....
Nitajibu la mdau mmoja"utamjuaje mpenzi wa kweli"..nimepitia mengi kwayo.
Tatizo la kudanganyana kwenye mahusiano huanza kwenye namna mnavyokutana.
Nitakueleza tu kuwa asilimia kubwa ya vijana huamini kuwa wakati wa mapenzi na uchumba ndio wakati wa "kuka bata"
Kumbe si kweli.
Jiyo ni sawa na kusema wiki moja kabla ya mechi upumzike ili siku ya mechi usiwe mchovu.
Ni ujinga mkuu katika mahusiano
Kama ambavyo timu hujitahidi kwa kadri ya uwezo kufanya mazoezi na kujua timu pinzani na kuangalia namna ya kutoumia kabla ya mechi, vivyo hivyo kipindi cha urafiki na uchumba chatakiwa kuwa.
Usiigize wakati huu wa mwanzo wa mahusiano
Ni heri uwe na mtu anayekujua ulivyo kuliko aliyedhani anakujua kumbe sivyo
Onyesha uhalisia wako
Onyesha hisia zako
Weka bayana mipango yako
Usoyumbishwe katika uaminicho na mengine mengi.
Mfano...
Kama unajua fika kuwa hjwezi kubadili dini yako, usiwe na mahusiano ya uchumba na mtu ambaye anamini utabadili dini ili muoane.
Kama huwezi kuishi kijijini, usimpotezee muda mtu anayepanga kwenda kijijini.
La muhimu la kujifunza hapa ni kuwa...BE YOURSELF.
Na hivi ndivyo ninavyowashauri watu wanaoniomba ushauri wa kuingia kwenye uchumba.

Chukua karatasi yako...
Upande mmoja andika mambo yote unayopenda na kujivunia kuhusu wewe
Upande wa pili, andika mambo yote unayotamani yabadilike kuhusu wewe.
Kisha andika mipango yako ya miaka ijayo

Hilo litakusaidia kujua kuwa "Mimi nina matatizo sana kwenye matumizi ya pesa ama nina huruma kupitiliza ama ninapenda sana club. Lakini ni msakaji mzuri wa pesa na nina mahusiano mazuri na watu wote, na ninajituma sana kwenye biashara nk.
Nadhni nikimpata mtu mwenye nidhamu ya pesa lakini atakayenisapoti nifanye biashara na anayethamini familia (atakayesaidia nitakapokuwa kwenye biashara) nk itakuwa poa
Ina maana...
Kutokana na strength na weakness zako, fikiria umhitajiye.
Wapendwa.....nia kuu ya ndoa ni kukamilishana.
Kama hamkamilishani, kma nyote matatizo yenu ni yaleyale (mfano nyote walevi ama mnashinda nyumba za ibada nk) nyumba haitadumu.
Ndio maana hata ndoa za masupastaa hazidumu. Ni kwa kuwa wana strength and weaknesses zinazofanana.

Kwa kumalizia
Kabla hujachagua wa kwenda naye safarini, jua uendako na yeye aendako. Kukishabihiana....ambatana naye

JITAMBUE

07/10/2014

Knowing YOUR SELF

Location

Category

Telephone

Address

[email protected]
Iringa-Mvumi
RLABS
Other Education in Iringa-Mvumi (show all)
Cagrierlo" Cagrierlo"
162
Iringa-Mvumi, YOHANA1204

Preventdrugabusecampany Preventdrugabusecampany
[email protected]
Iringa-Mvumi, +255

Kupiga vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya