Nzasa II Primary School

Nzasa II Primary School

Comments

Hawa nahonga issa
HABALI ZENU
Dear Team. We are Harmless Group Tanzania a company registered for Occupational Safety services.

We are interested to provide our services to your school for safety of students, staff and assets.

Please contact us through +255 755037079 and visit our website
Dear Team. We are Harmless Group Tanzania a company registered for Occupational Safety services.

We are interested to provide our services to your school for safety of students, staff and assets.

Please contact us through +255 755037079 and visit our website

Share with us and Join to give support in a society Development Maisha bora huanzia kwenye msingi wa Elim bora.

Operating as usual

nzasa2primaryschool.weebly.com 01/11/2015

NZASA II PRIMARY SCHOOL

nzasa2primaryschool.weebly.com HISTORIA YA SHULE KIUFUPI: SHULE YA MSINGI NZASAII NI SHULE YA SERIKALI ILIYOPO WILAYA YA ILALA CHINI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILALA. SHULE ILIANZISHWA MWAKA 1995 NA ILIFUNGULIWA NA MHESHIMIWA...

nzasa2primaryschool.weebly.com 01/11/2015

matokeo ya darasa la saba 2015 (mpya)

Matokeo ya Darasa la saba shule ya Msingi nzasa II new post

nzasa2primaryschool.weebly.comhttp://necta.go.tz/matokeo/xyx_###123/results/shl_p0201010.htm

nzasa2primaryschool.weebly.com 01/11/2015

NZASA II PRIMARY SCHOOL

nzasa2primaryschool.weebly.com HISTORIA YA SHULE KIUFUPI: SHULE YA MSINGI NZASAII NI SHULE YA SERIKALI ILIYOPO WILAYA YA ILALA CHINI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILALA. SHULE ILIANZISHWA MWAKA 1995 NA ILIFUNGULIWA NA MHESHIMIWA...

nzasa2primaryschool.weebly.com 01/11/2015

NZASA II PRIMARY SCHOOL

nzasa2primaryschool.weebly.com HISTORIA YA SHULE KIUFUPI: SHULE YA MSINGI NZASAII NI SHULE YA SERIKALI ILIYOPO WILAYA YA ILALA CHINI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILALA. SHULE ILIANZISHWA MWAKA 1995 NA ILIFUNGULIWA NA MHESHIMIWA...

nzasa2primaryschool.weebly.com 01/11/2015

NZASA II PRIMARY SCHOOL

nzasa2primaryschool.weebly.com HISTORIA YA SHULE KIUFUPI: SHULE YA MSINGI NZASAII NI SHULE YA SERIKALI ILIYOPO WILAYA YA ILALA CHINI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILALA. SHULE ILIANZISHWA MWAKA 1995 NA ILIFUNGULIWA NA MHESHIMIWA...

nzasa2primaryschool.weebly.com 10/09/2015

NZASA II PRIMARY SCHOOL

nzasa2primaryschool.weebly.com HISTORIA YA SHULE KIUFUPI: SHULE YA MSINGI NZASAII NI SHULE YA SERIKALI ILIYOPO WILAYA YA ILALA CHINI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILALA. SHULE ILIANZISHWA MWAKA 1995 NA ILIFUNGULIWA NA MHESHIMIWA...

nzasa2primaryschool.weebly.com 10/09/2015

new

NZASA II

nzasa2primaryschool.weebly.com HISTORIA YA SHULE KIUFUPI: SHULE YA MSINGI NZASAII NI SHULE YA SERIKALI ILIYOPO WILAYA YA ILALA CHINI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILALA. SHULE ILIANZISHWA MWAKA 1995 NA ILIFUNGULIWA NA MHESHIMIWA...

nzasa2primaryschool.weebly.com 10/09/2015

NZASA II PRIMARY SCHOOL

nzasa2primaryschool.weebly.com HISTORIA YA SHULE KIUFUPI: SHULE YA MSINGI NZASAII NI SHULE YA SERIKALI ILIYOPO WILAYA YA ILALA CHINI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILALA. SHULE ILIANZISHWA MWAKA 1995 NA ILIFUNGULIWA NA MHESHIMIWA...

[08/30/15]   HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
SHULE YA MSINGI NZASA II

UTANGULIZI
Shule ya msingi Nzasa II ni shule ya Serikali iliyopo chini ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala. Shule hii ipo eneo la Chanika Wilaya ya Ilala Kusini Magharibi mwa Jiji la Dar es salaam kiasi cha Km 35 kutoka katikati ya Jiji.
Shule hii ilanzishwa mwaka 1993 na wakazi wa eneo hili ikiwa chini ya kanisa la Anglikana. Kuanzishwa kwake kulitokana na uhitaji wa Shule kwa watoto wao kwani shule iliyokuwepo ilikuwa mbali sana eneo la Chanika magenge hivyo watoto wadogo wasingeweza kutembea umbali mrefu kwenda huko. Mwaka 1995 Shule ilisajiriwa rasmi na Serikali kwa namba DS. 1/2/038. Na kufunguliwa na mheshimiwa Fredick Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu wakati huo.

CHANGAMOTO:
MAJI: Shule ipo katika eneo ambalo ni kame halian vyanzo vya maji, wanafunzi na walimu wanapata taabu sana ya maji hakuna maji kwa matumizi ya kawaida , kupikia kwani shule inatoa uji kwa watoto ambao ni bure haulipiwi hivyo shughuli ya kupika uji inakuwa ngumu kutokana na ukosefu wa maji, vilevile usafi wa vyoo kwani haiwezekani kufanya usafi wa vyoo bila maji.

NYUMBA ZA WALIMU:
Shule ina nyumba moja tu ya walimu hivyo walimu wote waliobaki wanaishi mbali na shule na hupata gharama kubwa ya usafiri kwani hakuna usafiri wa daladala walimu hutumia usafiri wa pikipiki(bodaboda) ambao ni ghali sana kulinganisha na bei ya daladala pia ni hatari kwa maisha.

UCHAKAVU WA MAJENGO:
Shule toka ilipojengwa mwaka 1995 haijafanyiwa ukarabati mkubwa hivyo majengo yake yamechakaa, kuta zina nyufa kubwa, mabati yote yameoza na kufanya shule yote kuvuja msimu wa mvua.

MADAWATI:
Ili watoto wote waweze kukaa kwenye madawati yanahitajika madawati 270, madawati yaliyopo kwa sasa ni 187 hivyo kuna upungufu wa madawati 83.

YATIMA:
Shule ina watoto yatima wengi asilimia kubwa ya wanafunzi wa shule hii ni yatima hivyo wanalelewa na walezi k**a babu, bibi, shangazi, n.k na wengi wa walezi hawa ni wazee hivyo kufanya washindwe kuchangia shughuli za maendeleo kunapohitajika kuchangia jambo Fulani kwani uwezo wao ni duni.

UTORO:
Changamoto nyingine ni utoro wa wanafunzi. Utoro huchangiwa na mambo mengi baadhi ya hayo ni kipato duni cha familia walezi huwapa wanafunzi biashara wakauze ili wapate fedha za kujikimu hivyo hawaji shule inavyopasa lakini pia inapotokea kunatakiwa michango kwa ajili ya shughuli ya maendeleo ya shule mzazi anapokosa uwezo wa kulipa hukataza mwanae kuja shule kwa kukwepa kudaiwa mchango hii nayo husaidia watoto kuwa watoro.


SHAMBA LA SHULE: (PORI)
Shule ina eneo kubwa. Sehemu kubwa ya eneo hilo ni pori hivyo inahatarisha usalama wa watoto na walimu kwa kuwa na uwezekeno wa kuwa na wanyama wabaya k**a nyoka n.k.

PLANI:
Kutokana na changamoto hizi uongozi wa shule umeweka mipango ya kupunguza changamoto hizi. Mipango hii ipo ya muda mfupi na muda mrefu.
Mipango hiyo ni:-
1. MAJI: Uongozi wa shule umepanga kuchimba kisima kirefu ili kuondoa tatizo la maji kupata maji ya uhakika kwa matumizi ya wanafunzi na walimu pamoja na jamii inayozunguuka shule. Vilevile shule ina mpango wa kujenga tangi la maji la ardhini litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita 300,000. Matarajio ni kuhifadhi maji ya mvua. Ujenzi wa tangi hili utategemea upatikanaji wa ufadhili kutoka kwa wahisani.

2. NYUMBA ZA WALIMU:
Kuhamasisha wazazi na wananchi kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu na kuomba uongozi wa Manispaa kusaidia juhudi za wananchi.

3. KUTAFUTA WAFADHILI:
Uongozi wa shule unatarajia kutafuta wafadhiri watakaosaidia juhudi za wananchi kutatua changamoto hizi kupitia mikutano ya wazazi na ukurasa wa website ya shule na kuandika write up na kuzisambaza kwa wahisani mbalimbali.
4. Kumuomba Mkurugenzi wa Manispaa ayafanyie ukarabati mkubwa majengo ya shule.

5. KULIMA SHAMBA LA SHULE:
Uongozi wa shule una mpango wa kulima shamba la shule ili iweze kujitegemea kwa baadhi ya mambo k**a malipo ya mlinzi n.k.

6. KUAINISHA VIPAUMBELE:
Uongozi wa shule utaainisha vipaumbele vya mambo muhimu ya kuanza nayo katika hatua ya utekelezaji.
VIPAUMBELE:
1. Kuchimba kisima kirefu.
2. Kutengeneza madawati 100
3. Kulima shamba la shule.
4. Kukarabati majengo.

UTEKELEZAJI:
1. MAJI:
Kisima kirefu kimechimbwa, kimewekwa pampu, umejengwa mnara wa kuweka tangi la maji na tangi la maji limenunuliwa.Bado chanzo cha umeme ambacho kinaweza kuwa sollar power au Generetor

2. MADAWATI:
Kabla ya mpango huu shule ilikuwa na madawati 115 tu hivyo uongozi wa shule kwa msaada wa shirika lisilokuwa la serikari la OCODE yametengenezwa madawati 72 na sasa tunahitaji madawati 100 ili kumaliza tatizo la madawati.
3. SHAMBA LA SHULE:
Uongozi wa shule umejaribu kulima shamba la shule lakini kutokana na ukosefu wa zana za kilimo, kilimo hakikuweza kufanikiwa.

4. UKARABATI WA MAJENGO:
Ukarabati wa majengo bado haujapatiwa ufumbuzi juhudi zinafanywa kutafuta wahisani nab ado tunamuomba Mkurugenzi wa Manispaa aweze kusaidia hili.

MAOMBI:
Tunaomba wadau ,mashirika, Taasisi na watu wote wenye mapenzi mema watusaidie kutatua changamoto zinazotukabili ili kuinua elimu ya watoto wetu ambao ni viongozi wa Taifa hili siku zijazo.

MAKADIRIO YA GHARAMA ZA MIRADI:
Ili kuweza kutatua changamoto hizi tunahitaji fedha ili kuweza kufanya yafuatayo:-
1. MAJI:
Gharama ya kuchimba kisima kirefu:-
1. Kuchimba kisima m85 kwenda chini shilingi milioni nne (Tsh 4,000,000/=)
2. Kununua pump HP 1.5 Shilingi mulioni moja na laki mbili (Tsh 1,200,000/=)
3. Sollar Power shilingi milioni mbili na laki tano. (Tsh 2,500,000/=) Au generator kv 5 shilingi milioni moja na laki tano(Tsh 1,500,000/=)*
4. Tangi la maji la lita 5000 shiling laki saba na hamsini elfu.(Tsh 750000/=)
5. Ujenzi wa mnara wa kuwekea tangi shilingi milioni moja na laki nane. (Tsh 1,800,000/=)

Julma Tsh 10,250,000/=
• Kimojawapo kati ya hivyo.

2. TANGI LA KUHIFADHI MAJI YA MVUA:
1. Kuchimba shimo la urefu wa mitasita (6) kwenda chini na upana wa meta saba(7) kipenyo shilingi laki saba (Tsh 700,000/=)
2. Nondo mm12 pc [email protected] SH15,000/= Kwa shilingi laki saba na elfu hamsini. (Tsh750,000/=)
3. Binding wire roll 2 @sh80,000/= kwa shilingi laki moja na elfu sitini.
(Tsh 160,000/=)
4. Matofali 2500 @ sh 1200/= kwa silingi milioni tatu. (Tsh 3,000,000/=)
5. Cement mifuko 41 @ 13000/= kwa silingi laki tano na elfu thelathini na tatu.(Tsh533,000/=)
6. Ufundi sh 1.466,190
7. JUMLA Tsh 5,909,190/=

3. NYUMBA ZA WALIMU:
1. Shule inahitaji angalau nyumba tatu za walimu na nyumba moja inagharimu shilingi milioni kumi na tano hivyo nyumba tatu nisawa na shilingi milioni arobaini na tano. (Tsh45,000,000/=)

4. MADAWATI:
1. Shule ina upungufu wa madawati 100 gharama ya dawati moja ni sh laki moja na elfu ishirini kwa madawati 100 tunahitaji shilingi milioni kumi na mbili(Tsh 12,000,000/=)

5. UKARABATI WA MAJENGO:
Shule imechakaa kwani haijafanyiwa ukarabati mkubwa tangu ilivyojengwa. Ukarabati uko katika namna mbili kuta na paa. Kuta zina nyufa nyingi kiasi cha kutishia amani ya walimu na wanafunzi lakini paa linavuja maana mabati mengi yameoza vyumba vinne vya madarasa vinavuja, kwa hiyo k**ati imependekeza kuwa kwanza tuezeke vyumba vinavyovuja ambavyo ni vine na kila chumba kinahitaji mabati 52. Hivyo gharama zake ni k**a ifuatavyo:-
1. Mabati 208 geji 28 @ sh 18,000/= kwa silingi milioni tatu laki saba na elfu arobaini na nne.(Tsh 3,744,000/=)
2. Mbao (2x2) pc [email protected] sh 4500/= kwa silingi laki mbili na elfu sabini. (Tsh 270,000/=)
3. Misumari ya bati kg 20 @ sh 5000 kwa shilingi laki moja (Tsh 100,000//=)
4. Misumari ya kawaida kg20 @5000/= kwa silingi laki moja.(Tsh 100,000/=)
5. Gharama za ufundi Tsh 1,301,529/=
6. JUMLA Tsh 5,245,529

6. MRADI WA KILIMO:
Kwakuwa shule ina eneo kubwa tunataka kuanzisha mradi wa kilimo ili shule iweze kujitegemea kwa mabo mengine hasa chakula cha wanafunzi wakiwa shuleni. Ili kuweza kumudu hili tunahitaji vitendea kazi k**a ifuatvyo:-
1. Majembe [email protected] sh 5000/= kwa shilingi laki tano.(Tsh 500,000/=)
2. Panga [email protected]/= kwa shilingi laki moja na elfu hamsini.(Tsh 150,000/=)
3. Reki [email protected] sh 3500/= kwa shilingi laki moja na elfu tano. (Tsh 105,000/=)
4. Water ken [email protected] sh 3500/= kwa shilingi laki moja na elfu tano. (Tsh 105,000/=)
5. JUMLA Tsh 860,000/=
Tunawaomba wadau wahisani mashirika taasisi mbalimbali muweze kutusaidia na kuisaidia serikali yetu kutatua changamoto hizi kwa kuchagua kile ambacho unaweza kutusaidia ili kuweza kufanikisha lengo la Taifa la kuwapatia watoto wetu elimu bora kwani elimu bora inapatikana katika mazingira bora ya kujifunzia yenye mahitaji muhimu kwa mtoto.

Imeandaliwa na Hakimu Ramadhani Belege
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nzasa II

Mawasiriano:-
Mob: 0715425934
E- mail [email protected]
Blog: Nzasa2primaryschool.weebly.com

ASANTE

[08/26/15]   NZASA II PRIMARY SCHOOL
Ni shule ya msingi ya seriakali ya kitanzania iliyopo mkoa wa Dar es salaam wilaya ya Ilala kata ya chanika kijiji cha nzasa imeanzishwa account hii na mkuu wa shule ili kuielezea changamoto zinazoikabili shule ili iweze kupata msaaada kutoka kwa wafadhili au wahisani mbalimbali watakaopenda kujitokeza na kuisaidia changa moto hizo zilizopo Baadhi ya changamoto hizo ni uchakakavu wa majengo, uhaba wa madawati, upungufu wa vitabu, tatizo la umeme ili kuendesha kisima kirefu cha shule kilichochimbwa na mfadhili. hayo ni baadhi ya changamoto kuu zinazoikabili shule.

More information visit: http://nzasa2primaryschool.weebly.com/
or call 0754 425 934 mkuu wa shule.

[08/26/15]   TEASER!!!!!!

"Maisha BORA huanzia kwenye msingi wa Elim BORA"

BY. NZASA II (Admin)

26/08/2015

Nzasa II Primary School's cover photo

26/08/2015

Nzasa II Primary School

Location

Products

PRIMARY SCHOOL SUBJECTS

Telephone